MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), amewataka wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushirikiana na wabunge wa upinzani kutunga sheria nzuri.
Aidha, Mbunge huyo ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), amekosoa kile alichokiita utungaji wa sheria kwa nia ya kuwakomoa wapinzani kwa kuwa anaamini ipo siku hata CCM zitawakandamiza watakapokuwa na makosa.
Lissu aliyasema hayo katikati ya wiki iliyopita wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo bungeni mjini hapa.
Katika maelezo yake, Mnadhimu Mkuu huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alilalamikia sheria tatu zilizopitishwa na Bunge kwa nyakati tofauti, kwamba hazikustahili kupitishwa na chombo hicho.
Alizitaja sheria hizo kuwa ni Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016, Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 na Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektoniki.
Lissu alidai Bunge limekuwa likipitisha sheria zisizostahili kwa kutokana na wingi wa wabunge wa chama tawala. Alisema watalawa wanapaswa kukumbuka kuwa sheria hizo zinaweza kuwaumiza siku za usoni kama ilivyo kwa mmoja wa marais wa Ghana aliyepitisha sheria ya kuwaweka watu kizuizini na baadaye sheria hiyo ikatumika dhidi yake.
"Ninyi mlio wengi mkinyamaza, jana ni sisi, leo ni Nape (Nnauye) na kesho ni ninyi. Tafadhalini waheshimiwa wabunge, haya mambo mabaya yanayofanyika nchini, mtashughulikiwa ninyi wenyewe baada ya sisi kushughulikiwa na hakutakuwa na mtu wa kuwasemea maana na sisi tutakuwa tumefungwa," alisema.
"Kuna vitu vinaonyesha tumejisahau.
Katiba ya Kenya ya sasa, vile vifungu vya mwanzo kabisa vinazungumzia alama za taifa. Sisi leo tuna huu ni mwaka wa 66 tangu tupate uhuru. Kwa sheria za Tanzania Waziri atueleze kama Wimbo wa Taifa unatambuliwa kisheria."
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini