Jeshi la Polisi wilayani hapa Mkoa wa Geita, linawashikilia watu wawili Meshack Joseph na Fadhili Fadhili wakazi wa kata ya Uyovu wilayani hapa kwa kosa la kudaganya umma na kujifanya madaktari na kutoa mafunzo ya uuguzi.
Watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti baada ya kuwatapeli watu sita zaidi ya Sh6 milioni za malipo ya ada ya mwaka mmoja kwa ajili ya mafunzo ya uuguzi.
Miongoni mwa watapeliwa mkazi wa Musoma mkoani Mara, Neema Chacha alisema waliambiwa kuna chuo kinachotoa mafunzo ya uuguzi na kuripoti chuoni hapo amabpo walikuwa wakitumia shule ya watoto wadogo ijulikanayo Sengerema Academy wilayani Bukombe.
Amesema baada ya kufika chuoni hapo kilichopo Uyovu alikuta wasichana wengine watatu wakiendelea na masomo lakini fomu za kusajiliwa zilikuwa zimeadikwa majina tofauti.
“Fomu moja ilkuwa imeandikwa Kaisho chuo kiko Karagwe mkoani Kagera, nyingine mkoani jijini Mwanza na ya tatu Korandoto ya chuo kilichopo Shinyanga,” amesema Neema.
Amesema fomu zote tatu zilikuwa na namba moja ya usajili 247409 chuo na alijaza fomu ya Kaisho na kulipia Sh1, 100,000 kwa walimu hao katika shule ya watoto Sengerema Academy iliyopo kata ya Uyovu wilayani Bukombe.
Amesema waliotoa ada ya Sh1,100,000 walikuwa wawili yeye na mwingine Telezia Robert huku wenzao wanne walilipa kila mmoja Sh 990,000 na kuanza kufundishwa wakitarajia kufanya sherehe za kuhitimu masomo ya uuguzi mwaka huu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo amesema mtuhumiwa Meshaki Joseph alikamatwa Aprili 28 nyumbani kwake na mwingine Fadhili Fadhili alikamatwa Aprili 27 akiwa dukani kwake anapouza dawa za binadamu.
Amesema upepelezi bado unaendelea na utakapokamilika watafikishwa mahakamani.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini