Msanii Aslay ambaye hivi sasa ameanza kufanya kazi peke yake nje ya kundi la Yamoto band amefunguka na kusema kundi hilo hapo katikati walikwama na ndiyo maana walirudi nyuma badala ya kusonga mbele zaidi.
Aslay anasema kipindi cha nyuma walikuwa wanapata show nyingi sana jambo ambali lilipelekea kuwa na uwezo wa kufanya video kubwa hata nje ya nchi lakini baadaye mambo yalibadilika na kupelekea kufanya video zao hapa hapa bongo.
"Mimi nafikiri kwamba mipango yetu tu wenyewe, kipindi kile tunatoa ile video ' Madoido' kulikuwa na show nyingi zinaongozana ambazo zilituzuia kwenda kutengeneza video nyingine lakini si unajua tulikuwa tunajenga pia kwa hiyo kifupi ni kama tulijisahau na kuteleza kusema ukweli. Tukarudi tena tukafanya 'Suu' ambayo tuliifanya Zanzibar na tukawa na pesa kabisa ambayo ingetuwezesha kutengeneza video nyingine Afrika Kusini lakini hapo katikati tulifanya vitu fulani mchanganyiko ambavyo siwezi kuvisema vikaturudisha tena nyuma" alisema Aslay
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini