Meya wa zamani wa Jiji la Dar es salaam, Mzee Kitwana Kondo amefariki muda mchache uliopita huko katika Hospitali ya Hindu Mandal, ni baada ya kuuugua kwa muda mrefu.
Akithibitisha taarifa hizo Kupitia ITV, mtoto wa Marehemu Stella Kitwana Kondo, anesena Mzee Kitwana Kondo, amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam na mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa leo 25/5/2017 .
Wakati wa uhai wake Marehemu Kitwana Kondo aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Kigamboni na Meya wa manispaa ya Kinondoni.
Marehemu ameacha mjane na watoto watano .
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini