Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Nay Wa Mitego Afunguka Miujiza Ya Wimbo Wake Wa Wapo Licha Ya Kupata Misukosuko

MWANAMUZIKI Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ anayesumbua na Wimbo uitwao Wapo, hivi karibuni amefunguka namna wimbo huo ulivyomletea mafanikio ndani ya muda mfupi tangu auachie jambo ambalo kwake ni kama maajabu.
Akichonga na Over Ze WikendNay alizidi kufunguka kuwa miongoni mwa mafanikio ambayo wimbo huo uliyompa misukosuko umempatia ni kubadilishwa lugha na ‘media’ mbalimbali za nje zikiwemo BBC na CNN ili dunia nzima iweze kuupata ujumbe alioulenga lakini pia shoo ambazo hazikatiki.
“Tofauti na nyimbo zangu zote, Wapo umenipa mafanikio sana. Naona ni kama maajabu maana kila wiki napiga shoo kuanzia tatu lakini pia umenifanya kuwa karibu na viongozi wa kiserikali na ambao hawapo serikalini. Lakini pia ni kujulikana zaidi nje ya nchi maana media za nje zimenizungumzia sana,” alimaliza

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017