WEMA
Habari kutoka ndani ya chama chake kipya cha Chadema baada ya kuhama CCM zilieleza kuwa, Wema anatarajia kukabidhiwa majukumu ya uhamasishaji kama ilivyokuwa kwa mama yake, Mariam Sepetu ambaye alipewa cheo hicho kwa mtaa wake wa Sinza-Mori jijini Dar.
“Ameshaelezwa nini cha kufanya. Cha muhimu ni kuhakikisha anakuwa mbali na skendo za wanaume na kutengeneza CV kwa kufanya kazi za kijamii.
“Kama mtakumbuka hivi karibuni Wema alikuwa Morogoro kuhamasisha upandaji wa miti akiwa na Mbunge wa Viti Maalum wa Chadema, Devotha Minja. Sasa mwendo ni huohuo na ubunge kwake siyo jambo la kuuliza ifikapo 2020.
“Mbali na kufanya uhamasishaji kupitia shughuli za kijamii, pia anatengenezwa namna ya kuzungumza kwa kujenga hoja kwenye siasa ngumu, tofauti na alipokuwa CCM ambapo huko kuna siasa laini ukilinganisha na Chadema,” kilifunguka chanzo hicho.
Wikienda lilimtafuta Wema ili kupata ukweli wa ishu hiyo ambapo alikuwa akikata simu na kuomba ampigie mwandishi wetu baadaye.
Hata hivyo, alipotumiwa ujumbe mfupi kuelezewa kuhusu ishu hiyo ulionesha kupokelewa lakini hakujibu.
JOKATE
Wakati hali ikiwa hivyo kwa upande wa Wema, Wikienda pia lilidokezwa juu ya Jokate ambaye hivi karibuni alipewa cheo cha Kaimu Katibu wa Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) ikidadavuliwa kwamba huo ni mwendelezo wa harakati zake za muda mrefu za kutaka kuingia bungeni.
“Unajua, kama ilivyo kwa Wema, Jokate ana mvuto wake kwa vijana. Hicho cheo alichopewa ni ili kuzidi kumuweka karibu na viongozi wa chama na kuona utendaji wake. Suala la bungeni 2020 ni lazima, lakini pia amepigwa stop mambo ya sk¬endo za wanaume. Ndiyo maana baada ya kudaiwa kuachana na Ali Kiba hajasikika kuwa na mwanaume mwingine,” kilisema chanzo chetu.
Jokate na Ali Kiba
Akizungumzia ishu hiyo, Jokate alisema kuwa, ndiyo kwanza ameanza kutekeleza majukumu yake hivyo ni mapema mno kuzungumzia ishu hiyo.
“Kwanza mimi namshukuru Mungu kwa nafasi niliyopewa, naamini sitawaangusha vijana,” alisema Jokate kwa mkato.
Hivi karibuni Jokate alikuwa miongoni mwa wanachama 450 wa CCM walioji¬tokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) lakini hakupata nafasi hiyo.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini