Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Sirro Ataja Wanafunzi Wawili Waliofariki Kwenye Ajali Dar Asubuhi

Kamanda Sirro

Watu wawili wamepoteza maisha na wengine 24 kujeruhiwa kutokana na ajali iliyotokea leo (Jumatano) eneo la Superdoll Barabara ya Mwalimui Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema ajali hiyo ya uso kwa uso imehusisha lori aina ya Scania na Bus Eicher lenye lililokuwa likitokea Gongo la Mboto.
Sirro amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Itlam Athuman (mwanafunzi wa shule ya Sekondari Msimbazi kidato cha kwanza) na Sakina Imamu (Mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari Mchikichinj).
"Majeruhi wametibiwa katika Hospitali ya Temeke na baadhi yao wameruhusiwa wamebakia watatu tu. Jeshi la polisi linamshikilia dereva wa lori hilo kwani ajali hiyo imesababishwa na uzembe wake wa kuingia barabarani bila kuchukua tahadhari," anasema Sirro

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017