Kuna taarifa zimeenea kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii zikimhusisha mchezaji wa Serengeti Boys kufanyiwa vipimo na maafisa wa Caf kutaka kujua kama alitumia dawa za kusisimua misuli kabla ya mechi dhidi ya Angola iliyomalizika kwa Serengeti kushinda 2-1.
Licha ya Abdul kutangazwa man of the match alichukuliwa na maafisa wa Caf pamoja na mchezaji mwingine wa Serengeti Boys Kelvin Naftali kwa ajili ya kwenda kufanyiwa vipimo.
“Kwanza niwatoe shaka watanzania kuhusu wachezaji wa Serengeti Boys kuchukuliwa vipimo kwa ajili ya uchunguzi kama walitumia dawa za kusisimua misuli.”
“Hata kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Mali kuna wachezaji wawili wa Serengeti Israel Mwenda (alikua benchi) na Dickson Job walichukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa vipimo, kwa hiyo ni jambo la kawaida.”
“Na haichukui muda kujua majibu, vipimo vinasoma kwenye system na unajulishwa muda huohuo kama kuna shida au mchezaji yupo salama.”
Hadi sasa hakuna mchezaji yeyote aliyekutwa anatumia dawa za kusisimua misuli kati ya wachezaji ambao tayari wameshapimwa.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini