Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Wauguzi Waonywa Kutoa Lugha Chafu Kwa Wagonjwa

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga, Simoni Berege amesema hatomvumilia mtumishi yeyote wa idara ya afya atakae toa lugha chafu kwa wagonjwa.
Onyo hilo lilitolewa na mkurugenzi huyo juzi baada ya Diwani wa Viti Maalum Kata ya Chela, Angela Paul kutoa malalamiko ya wananchi juu ya wauguzi kuendelea kutoa kauli chafu kwa wagonjwa pindi wanapoenda kupata huduma katika vituo vya afya. 
“Bila shaka madiwani ni mashahidi tumefukuza baadhi ya watumishi kidogo nidhamu ipo kwa hali hii sasa uchunguzi utaendelea kwani hawa wananchi ndio wateja wetu ila tuna mpango wa kuanza kuwahamisha waliozoeleka” alisema Berege.
Awali diwani huyo alisema licha ya uhamasishaji unaofanywa juu ya wananchi kujiunga na bima ya afya, lakini wakifika hospitalini katika dirisha la dawa hawapatiwi huduma hiyo kama amabavyo inatakiwa.
“Nimetembelea kata yangu wananchi wanalalamika kuwa dawa hazipo kwanini zisiwepo huku tunaambiwa CHF imeboreshwa, sasa hii huduma ikoje dawa wananchi wananunua maduka binafsi sisi tunaohamashisha kama viongozi tunaonekana waongo hili naomba litatuliwe,” alilalamika diwani huyo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala, Dk. Nyembeya Hamad, alisema wamejipanga kuhakikisha watumishi wa idara ya afya waliodumu kwa muda mrefu katika vituo vya kazi wanaanza kuhamishiwa.
Akizungumzia kuhusu ukosefu wa dawa katika halmashauri hiyo alisema halmashauri haina upungufu wa dawa kwani zilizopo zinatosheleza hadi mwaka 2018.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017