Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo huenda akajikuta akitupwa jela kutokana na mamlaka nchini Hispania kumshutumu kwa kukwepa kulipa kodi kiasi cha dola za kimarekani milioni 16.5.
Waendesha mashtaka wamedai kuwa kodi anayodaiwa mshambuliaji huyo ni kuanzia mwaka 2011 mpaka 2014 na inahusu mapato ya nje na uwanja na haki za picha zake.
Mwezi Desemba, nyaraka zilizovuja zilieleza kuwa Cristiano Ronaldo amekwepa kodi kutokana na kipato chake kuwekwa kwenye akaunti za nje ya Hispania.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini