Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kesi Iliyoamuliwa Mahakama Kuu Tanzania Imetwaa Tuzo Ya Dunia


July 08 2016 Mahakama Kuu ya Tanzania ilitoa hukumu kukubali kwamba vifungu vya 13 na 17 vya Sheria ya Ndoa vinapingana na Katiba ya nchi kwa kuweka umri tofauti wa kuoa/kuolewa kati ya mtoto wa kike na wa kiume.
Hukumu hiyo ilikuja baada ya mwanzoni mwa 2016 Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali, Msichana Initiative linalotetea Haki za Wasichana kupata elimu, Rebeca Gyumi kupitia kwa Wakili Jebra Kambole kupinga vifungu vya 13 na 17 vya Sheria ya Ndoa vinavyoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha Mahakama, na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi.

Sasa good news leo June 7, 2017 ni kwamba kesi hiyo imeshinda Tuzo ya Gender Justice Award-Bronze kati ya kesi 17 zilizokuwa zinashindanishwa duniani ambapoTumewapata Rebeca Gyumi na Mwanasheria wake Jebra Kambole ambao wanatuelezea zaidi.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017