Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Chemical: Sifagilii Masharobaro, Nataka Mgumu Kama Nay Wa Mitego

Lapa wa kike anayefanya vizuri kwenye gemu ya Bongo Fleva, Chemical
Miongoni mwa marapa wa kike wanaofanya vizuri kwenye gemu ya Bongo Fleva, Chemical ni miongoni mwao ambapo hivi karibuni ameonekana kwenye muonekano mpya wa ‘kisistaduu’ tofauti na alivyozoeleka.
Kufuatia wengi kumhoji kuhusu mwonekano huo mpya, mwanadada huyo amefunguka kwamba yeye siyo sistaduu n ahata kwenye suala zima la mapenzi, hawafagilii masharobaro bali anataka mwanaume mgumu kama Nay wa Mitego watakayeendana.
Mwonekano mpya wa sasa wa, Chemical
Chemical ametaja sifa za mwanaume anayemhitaji katika maisha yake pindi atakapokuwa tayari kuingia kwenye mahusiano na kuongeza kuwa akishampata na wakikubaliana,  haraka sana akajitambulishe nyumbani kwao.
“Mimi ni msichana f’lani ambaye napenda mwanaume f’lani hivi mgumu lakini sijui nitakuja kuangukia wapi maana mapenzi hayachagui, lakini napenda sana nikutane na mgumu na siyo sharobaro, awe real kama Nay wa mitego vile,” amesema Chemical.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017