Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Abiria Wapigwa Marufuku Kuzungumza Siasa Safarini.

MAMLAKA YA Usimamizi wausafri wanchikavu na majini (SUMATRA) imepiga marufuku abiria kuzungumza masuala ya siasa, dini na kufanya biashara wawapo safarini.
Agizo hilo limetangazwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuuwa Sumatra, Lingadi Ngewe na kwamba abiria atakayebainika kufanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Agizo hilo linakuja baada ya hivi karibuni kudaiwa kuwapo kwa mvutano wa kupinga kanuni mpya kati ya Sumatra na chama cha wamiliki mabasi yaendayo mikoani (Taboa) na wausafiri Dar es Salaam (UWAMADAR).
Bila kutaja ni sheria na kununi ipi Mkurugenzi huyo amesema ufanyaji wa vitendo hivyo katika mabasi ni kinyume na kanuni za usafirishaji.
“Tutaanza kuzuia wasafiri wa wapo ndani ya mabasi kuacha kuzungumza masuala ya siasa, dini na kufanya biashara. Tukibaini hilo hatua za kisheria zitachukuliwa kwa abiria na dereva ikibidi,” amesema na kuongeza
‘Kwa madereva hasa wa kwenda mikoani, njiani wanapandisha wafanyabiashara na kufanyabiashara ndani ya basi, hatua kali zitachukuliwa kwa dereva na huyo anayefanyabiashara.’

Jana jijini Dar es Salaa mpamoja na kukanusha kuwapo kwa mgomo, Taboa na Uwamadar wamedai kuwapo katika malumbano ya kanuni na sheria mpya zinazotarajia kutumika hivi karibuni baada yamchakato wake kukamilika.
Mwenyekiti wa UWAMADAR, Kismat Dhalla amesema pamoja na mambo mengine Jumatano wiki hii watakaa na Sumatra kujadili masuala kadhaa ikiwamo kanuni na sheria mpya za usafirishaji.
Hata hivyo Mweka hazina wa Taboa, Issa Nkya amesema wapo kwenye msuguano na Sumatra kuhusu kanuni na sheria hizo na kwamba watazipatia ufumbuzi muda si mrefu.
Mkurugenzi wa huduma za sheria wa Sumatra, Tumaini Silaa amesema Sumatra ipo kwa ajili ya kuhakikisha wadau wote wa usafiri wanapata haki sawa.
Amesema sheria na kanuni mpya bado zipo katika mchakato na kwamba haziwezi kuanza hadi hapo wadau wote watakapoku baliana.
‘Kimsingi mambo haya ya kisheria na kanuni mpya haziwezi kuanza kabla ya kujadiliana na wadau wote wa usafiri, hivyo naamini hili haliwezi kuwa jambo kubwa sana na litapatiwa mfumbuzi,’ amesema.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017