Baada ya jana Hanspoppe kuongea kwa hasira kuhusiana na mchezaji Shomari Kapombe kutocheza Simba licha ya Kupona na kisha baadaye Kapombe mwenyewe kuthibitisha kuwa bado anaumwa na daktari amemwambia anaweza kuanza kucheza baada ya mzunguko wa Kwanza wa ligi kuisha.(Mzunguko wa Pili) na kapombe akaenda mbali zaidi na kusema kama Simba wanataka kuvunja mkataba naye yeye yuko tayari ila hawezi kucheza wakati bado ni mgonjwa.
Hanspoppe leo ameamua kuweka wazi kuwa Kuna mambo inabidi yakae sawa kuhusiana na suala la Kapombe kwanza msomaji wa Kwataunit.com amesema Ieleweke kuwa wakati Kapombe anasajiliwa Simba hakuwa MAJERUHI kama ambavyo wengi wanasema na ndiyo maana alishiriki michuano ya COSAFA katika mechi zote kabla ya kuja kupata majeraha akiwa na timu ya Taifa jijini MWANZA.
Hanspoppe ameongezea na Kusema kuwa majeraha aliyoyapata akiwa Simba siyo yale yaliyokuwa yakimsumbua akiwa Azam, yalikuwa ni majeruhi ya kawaida tu ambayo angepona kwa muda mfupi.
Ila Hanspoppe ameenda mbali zaidi na kusema kuwa Kapombe amepona kulingana na Ripoti ya daktari lakini daktari huyo amesema tatizo la Kapombe ni imani za Kishirikina kwani Kapombe anaamini kuwa amerogwa Taifa Stars. Kumbuka Kulike Ukurasa wetu wa Facebook hapo chini kupata mwanzo mwisho wa skata hili.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini