WANAMUZIKI ambao wanakimbiza kwenye gemu la Muziki wa Hip Hop Bongo muda mrefu, Ambwene Yessaya ‘AY’ na Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, wamefunguka kumfikisha mahakamani mtu aliyetupia wimbo wao mpya wa Upo Hapo kwenye Mtandao wa YouTube.
Akipiga stori na Mikito Nusunusu, AY alisema mtu huyo tayari akaunti yake aliotupia wimbo huo wameifahamu na kwamba amefanya hivyo kwa makusudi wakati anajua kabisa wenye haki ni kampuni ya Mkito.
“Kwanza amefanya bila makubaliano maalumu na sisi na hata tulipomtaka kuomba radhi na kuachana na wimbo huo alikataa. “Ni lazima tutamfikisha mahakamani awe mfano kwa watu wengine wanaopenda kutumia nguvu za watu bure,” alisema AY. Hii si mara ya kwanza kwa FA na AY kwenda mahakamani kulalamika kuhusu kazi zao za kimuziki, walishafanya hivyo kwa kampuni moja ya simu nchini na kushinda kesi iliyowapatia mamilioni.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini