Kufuatia Taarifa za wachezaji wa Yanga kuudai uongozi wa Klabu hiyo baadhi ya Malimbikizo yao kama mishahara na Posho hatimaye Uongozi umekuja na Majibu kuhusu taarifa hizo.
Klabu ya Yanga msomaji wa Kwataunit.com kupitia kwa katibu mkuu wake Boniface Mkwasa umesema kuwa Taarifa zinazoenea kuwa kuna wachezaji wanawadai mishahara na posho ni taarifa za kutaka kuleta Uchochezi tu ndani ya Klabu yao.
Mishahara ni suala binafsi siwezi kumsemea mtu, hata serikalini haya masuala yanatokea ya watu kuchelewa kupata mshahara hivi ni vitu vya kawaida, klabu inahangaika kuhakikisha kila kitu kinaenda kwa wakati muafaka, sidhani kama kuna shida posho zao zote, bonus zao zote wamepata kulingana na makubaliano yetu sisi na wachezaji hayo mengine yote yanayozungumzwa ni propaganda za kutaka kuleta uchochezi.
Yanga pia imewaonya wachezaji ambao wapo Yanga kwaajili ya Maslahi zaidi na kuweka wazi kuwa hawatahofia kuachana naye kwani timu inamatokeo mazuri na hawatataka hali hiyo itokee kwenye klabu ya Yanga.
Yanga ambayo inaendelea na mazoezi yake katika uwanja wa Uhuru Dar Es Salaam ikiiwinda Simba imesema Pia wachezaji wake majeruhi wanaendelea vizuri kuelekea mchezo kati yake na Mbeya City November 19, 2017.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini