Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inapenda kuutahadharisha Umma dhidi ya matapeli wanaopita maeneo mbali mbali wakiwaeleza watu kwamba wanauwezo wa kuwapatia Ajira za Afya, huku wakiwataka kutoa rushwa, kitu ambacho si kweli na ni kinyume na sheria na taratibu za nchi.
Katika watu hao kuna mtu anayetumia jina la Godfrey Nyami anaejifanya ni mtumishi wa Idara ya Utawala Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na huchukua fedha kiasi cha shilingi 100,000/ kwa ahadi ya kuwapatia kazi.
Kama kuna mtu yoyote anafanya hivyo na unamfahamu tafadhari toa taarifa katika vyombo vya dola, kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na hatua kali zitachukuliwa.
Imetolewa na ,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya
27/11/2017.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini