Takriban watu wanne wamethibitishwa kuuawa wakati wa mashambulizi kwenye mtaa wa Mathare mjini Nairobi nchini Kenya.
Wakaazi wa mtaa huo wa mabanda wanadai kuwa makundi yaliyokuwa yamejihami kwa panga na silaha zingine yalivamia mtaa huo na kuwaua watu hao ambapo pia waliharibu mali.
Polisi wanasema kuwa wanachunguza kisa hicho na nia yake.
Wakaazi wanasema waliamka kwa mshangao asubuhi walipopata miili ya watu wanne iliyokuwa na majeraha.
Mahakama yasikiza kesi inayopinga uchaguzi wa Uhuru Kenyatta, Kuuliwa kwa watu hao kumesababisha ghasia kusambaa hadi mitaa iliyo karibu huku polisi wakikabiliana na wale waliokuwa wakilalamikia mauaji hayo.
Kamanda wa polisi mjini Nairobi Japheth Koome alithibitisha mauaji hayo na kusema kuwa uchunguzi unafanywa, lakini akatupilia mbali madai kuwa yamesababishwa na ghasia za kikabila kufuatia hali ya kisiasa iliyopo sasa.
Mauaji hayo yanatokea siku moja baada ya watu wengine watano kuuwa wakati wa shughuli ya kumkaribisha kinara wa upinzani ambaye amekuwa ziarani Ulaya na Marekani.
Polisi wanasema kuwa wale waliouawa walikuwa ni wezi waliopigwa na watu waliokuwa na hasira.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini