ASKARI Polisi wa kike amefariki dunia jana mchana wilayani Misungwi baada ya kupatwa na mshtuko kufuatia kutokea kwa tetemeko la ardhi jijini Mwanza lililodumu kwa sekunde zisizozidi 40.
Mganga Mfawidhi Hospitali ya wilaya ya Misungwi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ambapo imeelezwa kuwa tetemeko hilo lilitokea majira ya saa 6:56 hadi saa 6:57 mchana.Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi akizungumzia tukio hilo amesema askari huyo mwenye jina la WP 4674, Detective Kopro Joyce aliyekuwa akifanya mahojiano na mahabusu, wakati tetemeko lilivyotokea alipatwa mshtuko wa moyo hivyo kukimbizwa hospitali ambapo alipoteza maisha.Aidha Kamanda Msangi amesema askari mwingine na mahabusu mmoja walipoteza fahamu ambapo walikimbizwa hospitali kutibiwa.
Katika tukio hilo, watu wengi wameonekana kukimbilia mahala ambapo wanaweza kujistiri ili wasikumbwe na maafa ya tetemeko hilo.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini