Chama Cha Mapinduzi kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuhusu matukio ya Mauaji yanayoendelea katika Wilaya za Kibiti, Mkutanga na Rufiji Mkoani Pwani ili kuepusha mauaji hayo kuendelea kutokea.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, HUMPHEY POLEPOLE, amesema hayo Jijini Dar es salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mauaji yanayoendelea katika Wilaya hizo.POLEPOLE pia amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinaelekeza akili, nguvu zao katika Wilaya hizo kwa kuwa maujia hayo yanasababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo.
Amesema chama kwa muda mrefu kimekaa kimya kikiamini hatua zitachukuliwa kwa kuwa wanachama wake na watendaji wameendelea kupoteza maisha ambapo amesema kwa sasa imetosha.Kuhusu suala la uchaguzi ambao unaendelea ndani ya Chama hicho amesema mauaji hayo yanakiweka Chama katika mazingira magumu ya kufanya chaguzi zake hivyo ni vema hatua zikachukuliwa sasa.
Katika hatua nyingine, POLEPOLE amesema Chama kimeipongeza Kamati Maalum ya kuchunguza Mchanga wa Madini kwa kazi nzuri iliyofanywa sanjari na kuwaomba wananchi kumuunga mkono Rais JOHN MAGUFULI kwa hatua alizozichukua kwa watendaji kutokana na Ripoti ya Mchanga wa Madini.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini