NI wazi sasa siku za wapiga debe katika vikuto vikubwa vya mabasi nchini zinaanza kuhesabika.
Hiyo ni baada ya Serikali kwa kushirikiana na wamiliki wa mabasi, kujiandaa kutumia mfumo mpya wa ukataji wa tiketi kwa njia ya elektroniki na siku za kiganjani.
Hatua hiyo imekuja baada ya wamiliki wa mabasi kukubaliana kwa kauli moja kuwa mfumo mpya ambao sasa uko hatua za mwisho katika makubaliano na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kabla ya kutumika, utaisidia kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zikipotelea mikono mwa wapiga debe.
“Tunaamini ukataji wa teketi kwa njia hii utasaidia kuingiza mapato serikalini, lakini pia kwa wamiliki ambao wamekuwa wakipoteza fedha nyingi kwa mawakala au wapiga debe,”alisema mmoja wa wamiliki wa mabasi hayo.
Akizungumza na Mawingu TZ Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi wa Kampuni ya E-Ticketing Systems (ETS), Martin Kaswahili, alisema lengo la kutumia mashine za EFD ni kuingizia mapato ambayo yatakwenda moja kwa moja kwa wamiliki na serikalini.
Alisema mfumo huo, ni wa kisasa kwa sababu umekuwa ukutumika nchi nyingi duniani.
“Mmliki anaunganishwa moja kwa moja na mfumo wa kodi, abiria akikata tiketi kwa njia ya simu taarifa zake zitaifikia TRA moja kwa moja, huku mmiliki akipata fedha zake bila kupoteza hata senti,”alisema.
Alisema tayari jambo hilo limejadiliwa kwa kina katika vikao kati ya maofisa wa TRA na wamiliki wa mabasi, huki pande ikiafikia kuwapo mfumo huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), Enea Mrutu aliliambia gazeti hili jana mfumo huo mzuri utaokoa fedha nyingi zilizokuwa zikipotea.
“Mfumo huu nakubaliano nao, naamini umekuja wakati mzuri mno, wamiliki tumekuwa tukipoteza fedha nyingi kwa wapiga debe nchi nzima…hili ni jambo jema tunapaswa kuungana wote,”alisema Mrutu.
Alisema tayari wamekutana na Kamishna wa Kodi kutoka TRA, Udani Mwambusi na viongozi wengine wa mamlaka hiyo kujadili jambo hilo kwa kina.
Alisema katika kikao hicho, walijadili mambo mbalimbali ikiwamo jinsi TRA itakavyoweza kupata kodi kupitia mfumo wa EFD moja kwa moja.
Alisema walikubaliana mambo matatu ya kufanya ikiwa ni pamoja na marekebisho juu ya kulipwa asilimia mbili juu ya mtandao huo, kukusanya fedha na mkataba wa muda mrefu ambao awali ulikuwa ni wa miaka mitano, huku wamiliki wakitaka uwe wa muda mrefu.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini