Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Waziri Ndalichako Awapa Onyo Kali Walimu Wanaoshinda ‘Whatsapp’

WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amewataka walimu nchini kutimiza wajibu wao wa kufundisha, badala ya kuutumia vibaya muda wao wa kazi kwa ‘kuchati’ kupitia mitandao ya kijamii ukiwamo wa whatsapp.
Alisema hayo hivi karibuni wilayani Kondoa mkoani Dodoma wakati akifunga mafunzo ya walimu wanaofundisha darasa la tatu na la nne kuhusu mtaala mpya unaozingatia ukuzaji wa umahiri wa stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).
Mafunzo hayo yaliandaliwa na kuratibiwa na Wakala wa Usimamizi wa Elimu (ADEM). Aliwataka walimu kutimiza wajibu wao huku akiwanyooshea kidole walimu wasiotimiza wajibu na badala yake, kutumia muda mwingi kuwasiliana na watu kupitia mitandao ya kijamii ukiwamo wa ‘WhatsApp’.
Waziri Ndalichako alikiri Tanzania kuwa na uhaba wa walimu na kuahidi kulitatua tatizo hilo kwa kuwapeleka katika shule nyingine walimu wa ziada. “Nakiri kweli hili ni tatizo, lakini kuna shule walimu wanagawana ‘topic’ katika somo moja wakati shule zingine hakuna mwalimu hili halikubaliki ila kitaifa unaweza ukaona kama halina tatizo, lakini ni tatizo,’’ alisema.
Aliwaagiza wakurugenzi wote nchini kuangalia jinsi ya kusawazisha ikama ya walimu. Kuhusu madarasa, Ndalichako alisema Serikali imejenga madarasa 1,089.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017