Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Dah! Kumbe Hakuna Hata Panadol Simba, Yanga


MADAKTARI waliotakiwa kutoa huduma kwa wachezaji katika mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga, juzi walijikuta wakiondoka uwanjani bila vifaa vyao wala dawa kutumika jambo ambalo ni nadra kutokea.
Pambano hilo la kukata na shoka kwa watani wa jadi, lilichezwa katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, huku likitawaliwa na utulivu wa hali ya juu kwa mashabiki waliokuwepo uwanjani.
Katika mechi za watani wa jadi, mara nyingi huwa tunashuhudia mashabiki wakizimia au kupigana uwanjani, lakini mchezo wa juzi mambo yalikuwa ni tofauti kabisa kwani hakuna shabiki aliyepata tatizo.
Akizungumzia hali hiyo, Katibu Mkuu wa Chama cha Madakdari wa Michezo Tanzania (Tasma), Nassor Matuzya, alisema ni kutokana na mashabiki kufika uwanjani wakiwa wamejiandaa kisaikolojia.
Alisema uwanja uliotumika kwa mchezo huo unajulikana ni mdogo tofauti na Uwanja wa Taifa ambao hutumika kwa mechi nyingi za Simba na Yanga, hivyo kila aliyetoka nyumbani alikuwa amejipanga kukabiliana na mabadiliko hayo.
Matuzya alisema udogo wa uwanja uliwafanya mashabiki wengi watazame mechi nyumbani kwao kupitia runinga, ndio maana waliofika walikuwa wachache hivyo hofu ilichangia kuwafanya wakae kwa utulivu.
“Leo (juzi) hatujatoa hata Panadol kumtibu mtu, tunarudi na vifaa vyetu kama vilivyokuja kwa sababu hakuna shabiki aliyepata tatizo.
“Tatizo la kuzimia kwa mashabiki halikuwepo, nadhani hali hii imetokana na mashabiki kujipanga kisaikolojia ambapo wengi walibaki nyumbani,” alisema Matuzya.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017