Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kauli Ya Lwandamina Kuhusu Simba Baada Ya Yanga Kuichapa Mbeya City 5 Buyu

Pamoja na ushindi mnono wa mabao 5-0, walioupata jana dhidi ya Mbeya City, Kocha wa Yanga, George Lwandamina, amesema malengo yao ni kuhakikisha mwishoni mwa msimu kupata kile ambacho wamekusudia.
Lwandamina amesema hapendi watu kufananisha matokeo yao na yale ya wapinzani wao Simba, kwasababu kila timu ina mipango mkakati yake kuelekea mwishoni mwa msimu huu.
"Sisi hatushindani na Simba, mashabikiwetu walijue hilo sisi Yanga tuna mipango yetu tumepanga kuifikia ifikapo mwishoni mwa msimu huu, na kilicho cha muhimu kwetu ni pointi tatu hivyo hata kama tunashinda bao moja au mawili matokeo tunayapokea na tunaridhika kwasababu tumefanikisha tulichohitaji," amesema Lwandamina.
Kocha huyo raia wa Zambia amesema mipango yao kwa sasa ni kuendelea kujifua wakijiandaa na mchezo unaokuja dhidi ya Tanzania Prisons mchezo ambao utapigwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Kocha huyo amesema anaamini mchezo huo utakuwa mgumu kwasababu wapinzani wao rekodi zao zinamuonyesha kuwa ni timu nzuri na imara hasa wanapocheza nao hivyo wanajipanga kuona namna watakavyo jipanga na kupata matokeo.
Kwa ushindi wa jana Yanga imepanda hadi nafasi ya tatu, kwa kufikisha pointi 20, katika mechi 10, walizocheza hadi sasa na inazidiwa kwa pointi mbili na vinara Simba pamoja na Azam FC wenye pointi 22.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017