Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Simba yamruhusu Ndemla kwenda Sweden kufanya majaribio


Klabu ya Simba imetangaza kumpa ruhusa kiungo wake Said Hamis Ndemla kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Sweden.

Ndemla anakwenda kufanya majaribio katika klabu ua  AFC ya nchini Sweden, timu ambayo anaichezea Mtanzania mwingine, Thomas Ulimwengu.

Ulimwengu amekuwa kimya kutokana na kuwa majeruhi lakini AFC ndiyo iliyomuuza kutoka katika Academy yake kwenda TP Mazembe.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema ni utamaduni wa Simba kuwapa nafasi wachezaji waliopata nafasi ya majaribio.

"Kama ilivyo kawaida ya Simba, tumetoa nafasi kwa Ndemla kwenda Sweden kufanya majaribio," alisema.

Miezi kadhaa iliyopita, Simba ilimzuia Ndemla kwenda Sweden kufanya majaribio katika timu hiyo kwa madai taratibu hazikuwa zimefuatwa.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017