Kiwango cha kiungo Mudathir Yahya kimezua sintofahamu baada ya klabu ya Azam 'Wanarambaramba' kuonekana kutaka kumrejesha tena kundini huku bado akiwa anaitumikia Singida United.
Mudathir ambaye alitemwa na Azam kwa kigezo cha kushuka kiwango na hatimaye kutua Singida United kwa mkopo, ameonekana kuimarika mara dufu na huenda Azam wakamrejesha kundini katika dirisha dogo la usajili.
Afisa Habari wa Azam FC Jaffary Idd Maganga amesema kama mwalimu Aristica Cioaba atapendekeza kurudishwa kwa Mudathir basi hawatakuwa na namna Kwani bado ni mchezaji wao.
-Mudathir Yahya bado ni Azam FC alikwenda kwa mkopo kwenye klabu ya Singida United, kumpeleka kwa mkopo maana yake ni kwenda kuinua kiwango chake, taratibu zake zote za maisha zipo huku, no halali kwetu akiamua kurudi ni kuwa anarudi nyumbani," Maganga amesema.
Wapo tayari kumuuza.
Maganga amesema kama mwalimu hatokuwa anamuhitaji kwa utaratibu wa kawaida ni kuwa watazungumza na Singida United ili kuweza kumnunua moja kwa moja.
Kwa siku za usoni Mudathir amekuwa na kiwango kizuri hadi kurudishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania, ambapo pia alionesha mchezo mzuri wakati Taifa Stars wanacheza na Benin kwenye mchezo wa kirafiki Jumapili ya Novemba 12.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini