Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Snura Amtunukia Kichuya Bonge La Zawadi

UNAKUMBUKA ile ahadi ya msanii wa kizazi kipya, Snura Mushi, ya kumpa zawadi  winga wa Simba, Shiza Kichuya? Sasa kama hujui ni kwamba ahadi hiyo kaitimiza jana aisee.
Snura alikoshwa na bao alilolifunga winga huyo Februari 25, mwaka huu, dhidi ya Yanga, na kuisaidia Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, ndipo mwanadada huyo uvumilivu ukamshinda na kuamua kumuahidi zawadi ya viatu.
Jana Snura alimvutia waya Kichuya, ambapo walikutana nyumbani kwa mchezaji huyo maeneo ya Mabibo, Wilaya ya Kinondoni na kumkabidhi zawadi ya seti ya viatu vya kuchezea.
“Huwa ahadi ni deni, ndiyo maana nikaamua nitimize kile nilichokiahidi, niliamua kumpelekea nyumbani kwake Mabibo viatu vya kuchezea ambavyo nadhani vitamsaidia msimu ujao.
“Najikisikia furaha sana kutimiza jambo hilo, kwani roho ilikuwa inanisuta, kwani ni muda mrefu umepita ujue tangu niahidi, mwenyewe, kashukuru sana,” alisema.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017