Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kocha Wa Singida UTD Pluijm Amtaja Mchawi Aliyewabania Wasipate Ushindi Dhidi Ya Yanga Asema Bila Uyo Yanga Wangekufa Vzuri Tu


Baada ya matokeo ya suluhu juzi dhidi ya Yanga, kocha Hans Pluijm wa Singida United amemtaja kipa Youth Rostand kuwa sababu ya kuinyima timu yake ushindi.
Akizungumza jana, Pluijm aliyewahi kuifundisha Yanga alisema, Rostand alifanya kazi kubwa katika mchezo wa juzi na kama angeambiwa amtaje mchezaji nyota wa mechi hiyo bila shaka angemtaja kipa huyo raia wa Cameroon.
Usipitwe na Habari Muhimu, Install App  Yetu


Android ===>  Bofya hapa
“Kipa aliiokoa Yanga, japo wachezaji wangu wakati mechi inaanza walikuwa na hofu, lakini kadiri walivyocheza waliona ni mechi ya kawaida na naweza kusema tuliwashika, tulikosa bahati ya kufunga tu,” alisema kocha huyo raia wa Uholanzi na kuongeza kuwa:
“Tulifanikiwa kuwadhibiti wapinzani wetu, lakini narudia tena, kama si yule kipa wao (Rostand) wangetoka uwanjani vichwa chini.”
Hata hivyo, Pluijm amefafanua kuwa tayari amecheza mechi na timu ngumu ikiwamo Azam FC na Mtibwa Sugar na mechi ambayo anaona imebaki ngumu kwake ni dhidi ya Simba pekee.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017