Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kuachana na Nay Kumenipa Akili ya Kujibidiisha Katika Biashara- Siwema

Kuachana na Nay Kumenipa Akili ya Kujibidiisha Katika Biashara- Siwema

MZAZI mwenziye na mwanamuziki Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson amefunguka kuwa kama asingepitia misukosuko ya kimapenzi na mzazi mwenziye huyo mpaka kuachana basi asingepata akili ya kujibidiisha kibiashara.

Siwema mwenye makazi yake jijini Mwanza, alisema baada ya kupata misukosuko alitafakari na kuamua kupiga moyo konde na kusimama kama mwanamke ili afanye kitu ambacho kitamsimamisha na kuendelea na maisha yake.

“Unajua ukikumbwa na misukosuko hasa ya kimapenzi akili inatanuka, nilijiongeza haraka na leo hii nina duka langu kubwa la nguo hapa Mwanza na maisha yanaendelea, ningekaa kulilia mapenzi ningechemka,” alisema Siwema 

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017