Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Video: Steve Nyerere Ampongeza Msama, Aishukuru TRA

Msanii wa Filamu nchini Steve Nyerere amempongeza mkurugenzi wa wa kampuni ya Msama Promotion kwa kuendelea kuwakamata walanguzi wa kazi za wasanii kwa kudulufu.
Akizungumza na waandishi wa habari Steven Nyerere ambaye pia ni mwenyekiti wa kikundi cha Wazalendo kwanza amesema kuwa Wasanii wote wanatakiwa kuungana na Msama ili kuwadhibiti wafanyabiashara ambvao wanafanya biashara ya kuuza kazi za wasanii kinyume na haki.
”Wasanii wote tunatakiwa kuungana na Msama kwa ajiri ya kuwatafuta wafanyabiashara woote wanao dulufu kazi za wasanii Tanzania nzima ili kusudi waweze kunufaika wasanii na kuliingizia taifa kipato” amesema Steven Nyerere.
Hata hivyo, Steven Nyerere amelipongeza Shirika la Mapato Tanzania (TRA) kwa kuwasaidia kumuunga mkono Msama katika Harakati zake za kupigania haki za wasanii wa Tanzania ambao wamekuwa wakikosa mapato yao mengi kutokana wanao uza kazi zao bila kufuata taratibu.
Jana TRA kupitia kamishina wa kodi za ndani Elijah Mwandubya walifanikiwa kuwakamata wafanyabiashara wanao uza kazi za wasanii bila kufata utaratibu na kuwafungia maduka yao.
Tazama Video hapa


Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017