Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Haji Manara ataja Kilichomchukiza wakati Yanga ikiwatoa Ihefu FA cup

Moja kati ya Maafisa habari ambao wamekuwa na Mbwembwe hasa wanapopata nafasi ya Kuandika au Kuongea kuhusu Mpira Haji Manara wa Simba amekuwa Kivutio sana hasa anapoongelea Utani kwa Yanga na Kuisifia Klabu yake ya Simba.
Baada ya Mchezo kati ya Ihefu na Yanga ulioisha kwa Yanga kupata Ushindi kwa Penati 4 kwa 3 dhidi ya Ihefu ya Mbarali mkoani Mbeya Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram alionekana kuchukizwa na Maamuzi ya Refa wa mchezo huo.
Hata Nyani hutamani pilau,mbeleko za baadhi ya maamuzi ni kichefuchefu..ndio maana baadhi ya team zikienda kwenye international competitions wanatutia aibu tu…Ndegelec!!
Refa huyo msomaji wa kwataunit alitoa tuta dakika za Mwisho kabisa mara baada ya Obrey Chirwa kuangushwa kwenye eneo hatari akielekea Kufunga, Penati ambayo iliwekwa kambani na Obrey Chirwa.

Ile Ishu Ya Simba Kuandika Barua Wakitaka Mechi Yao Na Azam Isogezwe Iko Hivi...





Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ni kama imeanza kuingia mchecheto baada ya kuitaka Bodi ya Ligi (TPLB) kusogeza mbele mechi yake dhidi ya Azam iliyopangwa kuchezwe Februari 11 mwaka huu.

Simba yenye pointi 35, inachuana vikali na Azam wenye 30 katika msimamo wa ligi na Mabingwa watetezi Yanga waliovuna 28, katika kuliwania taji hilo la ubingwa la ligi.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Haji Manara alisema ratiba yao inawapa ugumu kutokana na akili na nguvu zao kuzielekeza kwenye michuano ya kimataifa na Simba imepangwa kucheza Gendarmerie Nationale ya Djibouti kati ya Februari 9-11, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Manara alisema, ratiba hiyo inawapa ugumu kwani Simba itacheza na Ruvu Shooting Februari 4 na kucheza na Azam kabla ya kwenda Shinyanga kucheza na Mwadui huku wakiusubiria mchezo wao wa kimataifa.
“Mipango ya Simba ni kufika mbali katika michuano ya Afrika na hiyo ndiyo sababu ya sisi kumchukua kocha Mfaransa, Lechantre (Pierre) ambaye amewahi kuipa ubingwa wa Afcon, Cameroon mwaka 2000.

“Hivyo, basi kama uongozi tumeiomba Bodi ya Ligi kusogeza mbele mchezo wetu dhidi ya Azam ili kutupa nafasi ya kujiandaa na mechi yetu ya kimataifa dhidi ya Wadjibout kwa kuwa tunaona ratiba inabana sana.

“Tupo katika hatua ya mwisho kwa ajili ya kuiandikia bodi ya ligi ili kuwafahamisha mchezo huo usogezwe mbele na kikubwa tunataka kuona Simba ikifanya vema katia michuano hii ya mikubwa Afrika, tunaamini busura itatumika,”alisema Manara.

Kocha Mpya Simba Alia Na Niyonzima , Atoa Kauli Hii…

Kocha mkuu wa klabu ya Simba Pierre Lechantre amesema anahiyanakumuona kiungo wa kimataifa wa Rwanda Harun Niyonzima akirejea dimbani baada ya kupona majeraha ili kuongeza ushindani katika timu.
Kocha huyo raia wa Ufaransa amesema kuwa anamfahamu vyema Niyonzim kuwa ni mchezaji mwenye kipaji lakini anahitaji kukiona uwanjani  ili aweze kumpatia nafasi katika kikosi chake.
“Uongozi na benchi la ufundi la timu ya Simba wamenieleza kuhusu Niyonzi na mimi nakubaliana na walisemalo lakini nahitaji kumkumuona uwanjani akithibitisha yasemwayo. Alisema Lechantre.
Niyonzima amekuwa nje ya uwanja  kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi kitu kinachopelea kuhitaji mazoezi binafsi au mwalimu wa kumnoa kuhakikisha anarejea katika kiwango chake cha awali.

Jikumbushe Wafungaji Bora Wa Ligi Kuu Bara Hadi Baada Ya Mechi 15 Kwa Kila Timu

2017/18
Okwi Simba 12
Habib Haji Mbao 7
Mohammed Rashid Prisons 7
Obrey Chirwa Yanga 7
John Bocco Simba 7
Kichuya Simba 6
Ajibu Yanga 5
Marcel Boniventure Majimaji 5
Asante Kwasi Simba 5 Akiwa Lipuli alifunga manne
Paul Nonga Mwadui 4
Eliud Ambokile Mbeya 4
Mbaraka Yusuph Azam 3
Venus Ludovick Kagera 3
Danny Usengimana Singida 3
Eliuter Mpepo Prisons 3
William Lucian  Ndanda 3
Emmanuel Mviyakure Mbao 3
Hamis Mcha Ruvu 3
Paul Peter Azam 2
Edward Christopher Kagera 2
Laudit Mavugo Simba 2
Mohammed Samatta Mbeya 2
Evarist Maganga Mwadui 2
Abdallah Seseme Mwadui 2
Donald Ngoma Yanga 2
Michael Katsaivro Singida 2
Stamili Mbonde Mtibwa 2
Mzamiru Yassin Simba 2
Jafar Kibaya Kagera 2
Emmanuel Martin Yanga 2
Kelvin Sabato Mtibwa 2
Hassan Dilunga Mtibwa 2
Pius Buswita Yanga 2
Yahaya Zayd Azam 2
Peter Mapunda  Majimaji 2
Omary Mponda Ndanda 2
Salim Hamis Mwadui 2
Claide Wigenge Njombe 2

Elinyesia Sumbi Singida 2

Suala La Kujiamini Ubingwa Mapema, Kocha Simba Awapa Neno La Tahadhari Wanasimba





Kutokana na mwendo wa kikosi cha Simba katika Ligi Kuu Bara, wengi wanaamini lazima kitabeba ubingwa.

Kocha Msaidizi wa Simba Mrundi, Masoud Djuma ametamka kuwa ni ngumu kutabiri Ubingwa wa Ligi Kuu Bara kutua Msimbazi katika mzunguko huu wa pili licha ya kuongoza katika msimamo.

Simba hivi sasa inaongoza katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 35 wakifuatiwa na Azam FC wenye 30 huku Yanga wakishika nafasi ya tatu wakivuna 28.

Djuma alisema bado bingwa wa ligi hajaulikana hivi sasa wakielekea kwenye mzunguko wa pili kutokana na kupishana pointi chache dhidi ya wapinzani wao Yanga na Azam.

Djuma alisema, bado wana kibarua kigumu cha kuhakiisha wanashinda kila mchezo utakaokuwepo mbele yao ili waache kwa idadi kubwa ya pointi wapinzani wao.

“Ili tujihakikishie ubingwa wa ligi kuu, basi tunatakiwa kushinda kila mchezo utakaokuwepo mbele yetu bila ya kuidharau hii timu ndogo au kubwa.

“Hilo tumeshwaambia na tunaendelea kuwakumbusha wachezaji wetu katika vikao tunavyovifanya kila siku kabla ya na baada ya mazoezi kwa kuwasisitiza tupambane ili tujiwekee mazingira mazuri ya ubingwa.


“Kama unavyofahamu tumebakisha kombe moja pekee la ligi kuu, kwani tayari tumelipoteza Kombe la FA, hivyo ili tuuchukue Ubingwa wa ligi ni lazima wachezaji wapambane ndani ya uwanja kwa kupata matokeo mazuri ili tuzidi kuwaacha mbali wapinzani wetu Yanga na Azam waliokuwepo chini yetu,”alisema Djuma.

Ambaka Askari Mwenzake Baada ya Kumringishia Uume Mrefu

Ambaka Askari Mwenzake Baada ya Kumringishia Uume Mrefu
ASKARI wa Uingereza aliyewahi kuwa shujaa wa vita nchini Afghanistan, hivi majuzi alimbaka askari mwenzake wa kike baada ya kujigamba kwamba alikuwa na uume mrefu.

Haya yalisema mahakamani ambapo Luteni-Kanali Chris Davies anashitakiwa kwa kumbaka askari ambaye ni mama wa watoto wawili na  umri wa miaka 53 katika tukio linalodaiwa kufanyika huko Kingston, Ontario,  Canada.


Davies anadaiwa kumwambia mwanamke huyo kwamba: “Nina uume wenye urefu wa inchi nane (sentimita 20.3) ambao unaweza kuubomoa ulimwengu wako.”  Jina na utambulisho wa mwanamke huyo vimehifadhiwa.

Mwanamme huyo anadaiwa alimfuata mwanamke huyo hadi hotelini kwake baada ya mwanamkehuyo ‘kubugia’ pombe mbalimbali za kutosha walipokuwa askari hao na wenzao wakinywa vileo.


Davies na mwanamke mwathirika walikuwa sehemu ya kundi la askari waliokuwa wakinywa vileo baada ya gwaride maalum kwenye kambi ya kijeshi ya Fort Frontenac (pichani).

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Davies alimwuliza mwanamke huyo: “Je, tukajaribu?”  Hii ni baada ya kujigamba kwamba kuhusu uume wake, jambo lililomfanya mwanamke huyo aondoke sehemu hiyo.



Mwanamke huyo aliripoti tukio hilo polisi mjini Kingston, Ontario, nchini Canada ambapo askari hao walikuwa wameungana na wale wa Canada kuadhimisha Mapigano ya Tuta (Ridge) la Vimy katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

Mama Diamond Ampost Wema Aandika Ujumbe Huu "Nyinyi Ongeeni Chambaneni Sisi Tunapiga Pesa"

Mama Diamond Ampost Wema Aandika Ujumbe Huu "Nyinyi Ongeeni Chambaneni Sisi Tunapiga Pesa"

Maneno yamekuwa mengi baada ya Wema Sepetu kupanda kwenye stage na kumuita Diamond Platnumz wakiwa Maisha Basement na wengi  kujiuliza kuhusu ukaribu wao tokea wakiwa Hyatt Regency katika utambulisho rasmi wa msanii Marombosso katika record label ya WCB.

Mama Diamond akaamua kupost instagram sehemu ya video clip Wema akiwa kwenye stage na kuandika “KWA HERUFI KUBWA NYIE ONGEENI CHAMBANENI CC TUNAPIGA PESA”

Kibaka Amuingiza Mjini Pluijm Wamuibia Mkoba wa Fedha

Kibaka Amuingiza Mjini Pluijm Wamuibia Mkoba wa Fedha

MUDA mchache baada ya kushuhudia timu yake ikipata bao la pekee katika dakika za nyongeza dhidi ya Tanzania Prisons juzi, Kocha wa Singida United, Hans van der Pluijm, alijikuta akiingizwa mjini na vibaka kwa kuibiwa mkoba wa fedha wakati akishangilia bao hilo.

Pluijim aliibiwa mkoba huo uliokuwa na simu aina ya Sumsung Pro 9 yenye thamani ya Sh. 1,575,700,  pochi ('wallet'), leseni ya udereva kwa nchi mbili Tanzania na Ghana, fedha za Dola 100 za Marekani, fedha taslimu Sh. 200,000 za Tanzania na funguo za gari lake aina ya Prado.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Isaya Mbughi, alisema baada ya ushindi huo, mashabiki walishangilia sana kiasi cha mhalifu kutumia mwanya huo kuiba mkoba wa kocha huyo hivyo kulazimika kuripoti polisi na msako mkali kuanza.

Askari wakiongozwa na taarifa za kitengo cha makosa ya mtandao kwa kutumia namba ya simu ya Pluijim iliyokuwamo kwenye mkoba, walifanikiwa kupata begi hilo likiwa limetupwa eneo la mtaa wa Kindai baada ya mwizi kubaini anafuatiliwa na polisi. 

Mbughi alisema kweye mkoba huo polisi walifanikiwa kukuta vitu vyote isipokuwa fedha ambazo mwizi alitoweka nazo.

Pluijim alipatiwa vitu vyake vyote isipokuwa fedha, lakini amesema Jeshi la Polisi linaendelea na msako kumbaini aliyehusika na uhalifu huo.

Aidha, jeshi hilo limetahadharisha wapenzi na mashabiki wa soka kujihadhari dhidi ya wezi wanaoingia uwanjani kwa nia mbaya huku wakikusudia kufanya uhalifu wakati wa kushangilia ushindi au bao linapofungwa.

Katika mchezo huo Singida United ilipata bao pekee dakika sita za nyongeza kupitia kwa kiungo mshambuliaji, Elinywesia Sumbi, ‘Msingida’ aliyeingia uwanjani dakika ya 78 kuchukua nafasi ya Deus Kaseke.

 Chanzo Nipashe 

Wastara Amfungukia Mange Kimambi na Wanaomtuhumu Kuwa Tapeli


Msanii wa filamu wa bongo Wastara Juma ambaye hivi karibuni amepewa mchango wa milioni 15 na familia ya Rais Magufuli, amewajibu watu wanaomtuhumu kuwa tapeli kwani hana ugonjwa unaomsumbua.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Wastara amesema kabla ya kuomba michango alijitahidi sana kujitafutia mwenyewe hiyo pesa kwani hakutaka pesa ya mtu mwengine ije imsaidie, kwani alijiona anakuwa mzigo kwa jamii.

Kufuatia kauli hiyo Wastara amesema alishajaribu kujiingiza kwenye biashara ambazo amedai hazina faida, mpaka kufikia hatua ya kuanza kuuza vitu vya ndani, jambo ambalo msanii mwenzake Steve Nyerere alimkataza, na kumshauri aweke wazi matatizo yake iili watu wamsaidie.

Akiendelea kulalamikia kitendo cha watu kumdhihaki, amesema asilimia kubwa ya watu wanaomtuhumu hawajahi hata kwenda kumuona wakiwemo wasanii wenzake, ambao waliamua kumtenga baada ya yeye kuolewa na aliyekuwa Mbunge wa CCM Sadifa.

Baadhi ya wasanii wamesikika wakiongea chini chini kuwa Wastara anajidai kuumwa ili apate hela , pia Mwanadada Mange Kimambi amemlipua Wastara kupitia ukurasa wake wa Instagram 

Aunt, Iyobo Na Tunda Kimenuka, Watupiana Matusi Si Ya Nchi Hii

VIDEO vixen asiyeishiwa stori kwenye mitandao ya kijamii, Tunda ameingia kwenye bifu la aina yake na Aunty Ezekiel na mpenzi wake, Mose iyobo baada ya mdada huyo kusemekana anadaiwa mkwanja ambao alitakiwa kulipia pombe alizokunywa.

Bifu hilo limetikisa jioni ya leo baada ya post kuanza kusambaa wakirushiana maneno makali (mengine tumeyafisha kulingana na maadili ya Kitanzania) jambo ambalo limezua mijadala miongoni mwa mashabiki wao.

Inavyoonekana kutokana, Tunda anadaiwa pesa za pombe na Aunt, kiasi cha Tsh. 100,000/= ambazo kwa maelezo yake anadai alimpa Mose Iyobo. Hapo ndipo tifu likaanza, fuatilia mwenyewe kilivyonuka.

Madee Afungukia Bifu Lake Na Roma

BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, hitmaker wa Ngoma ya Sema, Hamadi Ally ‘Madee’ hatimaye amefungukia kile kinachodaiwa kuwa ni bifu zito lililopo kati yake na msanii mwenzake, Ibrahim Musa ‘Roma Mkatoliki’.


Akipiga stori na Risasi Vibes, Madee alisema suala la uwepo wa bifu kati yake na Roma ni hisia tu zinazo-zushwa na mashabiki kutokana na vijembe wanavyo-tupiana na msanii huyo ambaye kimsingi ni mtani wake.

“Roma ni mtani wangu, mara nyingi huwa kuna masihara kati yangu na yeye, hata familia yake kwa ujumla, vile vijembe ambavyo huwa tunatupiana ule huwa ni utani tu hakuna uhalisia wowote, hatuna bifu kati yetu,” alisema Madee

Barnaba Ataja Kinachomuingizia Mkwanja Mrefu

STAA wa Bongo Fleva mwenye sauti ya kipekee, Elias Barnaba amesema kuwa kitendo cha kuwatungia mastaa ngoma zao hasa wa kike kimemfanya kutengeneza mkwanja mrefu.

Akichonga na Risasi Vibes, Barnaba ambaye kwa sasa amejitoa THT na kuanzisha lebo yake ya Hightable Sound alisema, hawezi kutaja mpaka sasa amepata kiasi gani lakini wasanii wa kike wengi aliowatungia ngoma wamekuwa wakimlipa vizuri.
“Ukiachilia mbali mkwanja ninaoupata kupitia studio na lebo yangu ya Hightable, kazi zangu za muziki, kingine kikubwa ni hawa wasanii ninaowatungia nyimbo, wamekuwa wakinipa mkwanja mrefu,” alisema Barnaba ambaye amewahi kuwatungia nyimbo mastaa kibao wa kike akiwemo Linah, Shilole, Lulu Diva, Recho na wengineo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya January 31



Aliyekuwa Mkurugenzi wa TBC Tido Mhando Afikishwa Mahakamani


Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Mhando anakabiliwa na mashtaka manne ya matumizi mabaya ya madaraka na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887 milioni akiwa TBC.

Tido alifikishwa mahakamani hapo saa 5:22 asubuhi na aliingizwa katika ukumbi wa mahakama ya wazi kabla ya kusomewa mashitaka hayo matano.

Nabii Tito Ajaribu Kujiua....Ashonwa Nyuzi 25

Siku mbili baada ya kukamatwa na polisi kwa mahojiano kwa Tito Machibya, maarufu Nabii Tito, anadaiwa kujaribu kujiua kwa kujikata na wembe tumboni na kushonwa nyuzi 25.

Nabii Tito alikamatwa na polisi mkoani Dodoma kwa kosa la kufundisha mafundisho yaliyo kinyume na dini kwa kuhamasisha watu kunywa pombe kwani si dhambi na kuoa wafanyakazi wao wa ndani ambapo hata hivyo, jeshi hilo lilisema nabii huyo ana matatizo na akili yaliyothibitishwa na daktari wa Hospitali ya vichaa ya Milembe mkoani Dodoma.

Inadaiwa kuwa, jana polisi waliambatana na nabii huyo nyumbani kwake Ng’ong’ona mkoani humo kwa ajili ya upekuzi ambapo aliingia ndani na kutoka akiwa anavuja damu tumboni huku ameshikilia wembe mkononi ambapo iliwalazimu polisi hao kumkimbiza Zahanati ya Polisi ya Mkoa wa Dodoma.

Mmoja wa madaktari wa zahanati hiyo kwa sharti la kutotajwa jina amesema nabii huyo alifikishwa, saa tisa alasiri akiwa na jeraha kubwa tumboni.

“Alifikishwa na kushonwa nyuzi 25 na kuruhusiwa kwani hakuwa na shida nyingine yoyote halafu jeraha lake halikufunguka kwa ndani sana, kwa hiyo hakutoka damu nyingi sana alitibiwa na kuondoka na askari.

Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Gilles Muroto alipoulizwa kuhusu tukio hilo hilo alisema hana taarifa.

Chanzo: Mtanzania
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017