Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter
Showing posts with label BONGO MOVIE. Show all posts
Showing posts with label BONGO MOVIE. Show all posts

Patcho Mwamba Amlipua Vibaya Mama Kanumba

Mwanamuziki na Muigizaji nchini, Patcho Mwamba ameifungukia kauli ya Mama Kanumba ya kushukuru kitendo cha Muigizaji Lulu kufungwa miaka miwili kwa kosa la kumuua bila kukusudia muigizaji Kanumba na kusema kwamba hakuna haja ya kuendelea na 'beef' kwani hakuna haki inayoweza kumrudisha Kanumba hai.

Patcho ambaye alikuwa muigizaji na rafiki wa karibu na Marehemu Steven Kanumba amesema kwamba Mama kanumba anapaswa  kuwa na moyo wa kusamehe kwa sababu binti huyo akimaliza kifungo atarudi mtaani na ataendelea na maisha yake hivyo kujengeana chuki siyo jambo jema.

"Sina la kusema juu ya jukumu ya Lulu, lakini Mahakama imeamua kama ilivyoamua, kwa upande mmoja kuna unafuu kwani kwa kesi ile kufungwa miaka miwili ni bahati, ukija upande wa pili inaumiza sana kwani jela siyo sehemu nzuri sana kwa mtu kuwepo kila mtu anajua hilo hasa ukizingatia   bado ni mdogo hivyo tumuombee Mungu ampe nguvu, uwezo naamsaidie aweze kustahimili hiyo hali" Patcho.

Aidha Patcho ameongeza "Nimemuona mama anasema anashukuru (Mama Kanumba) haki imetendeka, mimi sidhani kama kunahitajika kuwepo na ma Beef. Mwanaye, ambaye pia ni rafiki yetu ameondoka lakini tunaamini ni mipango ya Mungu. Hakuna haki inayoweza kumrudisha Kanumba aishi. kusema naenda kumzika Kanumba upya sidhani kama kuna haja ya kuendeleza ma beef japo yapo. End of the day Lulu atatoka wataongea vizuri?. Sidhani yule mama yangu hivyo simshauri aendee kuwa na kinyongo".

Patcho amemalizia na kusema kwamba "Kusema kufungwa kwa Lulu kutampatia unafuu sidhani  ni uongo yeye aendelee kuwa mama maana ninachoamini Lulu hakumuua Kanumba bali alikuwa shahidi wakati Kanumba anakufa  ndichi ninachokiamini. Baadaye Lulu atatoka jela je  ukimuon utamgonga na gari? au Mama Lulu utaweza kuongea naye na wale ni Wahaya ni kabila moja. Sidhani kama Lulu alikuwa akikaa na kufikiria ipo siku atamuua Kanumba".

KIMENUKA:Mama Kanumba Ageuziwa Kibao

WAKATI msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ akianza kutumikia kifungo chake cha miaka miwili jela kwa kosa la kuua bila kukusudia, wadau mbalimbali wanaonekana kumgeuzia kibao mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa kufuatia kauli zake zinazotokana na hukumu hiyo iliyofanywa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Sam Rumanyika.

Katika kile kinachotafsiriwa kama furaha yake kufuatia hukumu hiyo, katika matukio mbalimbali Mama Kanumba amesikika akitoa maneno kama vile huu ni wakati wa wao (upande wa akina Lulu) nao kupata machungu kama ilivyokuwa kwake wakati kijana wake huyo alipofariki dunia.

Flora Mtegoa akiwa karika kaburi la Marehemu Steven Kanumba.

Mama huyo ameonywa kuwa makini na kauli hizo kwani kibinadamu ni kauli ambazo hazifai kwa kipindi hiki ingawa alipotelewa mtoto wake.

“Mimi namshangaa mama Kanumba, anakosea sana hata kama amefiwa angeonesha ubinadamu tu kwa sababu hata huyo Lulu aliumia kuondokewa na mpenzi wake.

Lile lilikuwa ni tukio la bahati mbaya, hakuna aliyependa litokee,” alisema msomaji aliyejitaja kwa jina la Sara. Mtu mwingine aliyekataa kutaja jina lake, alisema kwa kuwa Mama Kanumba ni mzazi, kwa busara angenyamaza tu kwani machungu aliyoyapata hata Mama Lulu naye ameyapata, japokuwa mwanaye hatorudi lakini ndiyo ashuruku Mungu kwani kwa upande mwingine Mungu amechukua mja wake kama ilivyoandikwa kwenye maandiko yake kuwa kina nafsi itaonja mauti.


“Mama Kanumba kama Lulu alimkosea angeshukuru tu akamuachia Mungu kuliko kuongea maneno hayo, akumbuke kuwa yule ni mtoto na mama yake ana machungu kama yeye alivyopata machungu,” alisema mwanamke aliyejitambulisha kama Mama Aisha.

Kauli nyingine ambayo imewakwaza watu ni pale alipodai kuwa hukumu hiyo imempa furaha kama wao walivyofurahia na kufanya sherehe ya kuzaliwa kwa mdogo wake Lulu, siku moja na ambayo yeye alikuwa akifanya kumbukizi ya kifo cha Kanumba.

Aidha, kauli nyingine ni ile aliyosema kuwa wakati wao walikuwa wakifika mahakamani kwa magari ya kifahari, yeye alikuwa akitumia usafiri wa daladala kwa shilingi elfu moja tu, kitendo kilichosababisha watu wamshushe.

Neno la Mhariri Kwa kuwa Lulu ameshahukumiwa kutumikia kosa alilolifanya, kwa busara kabisa Mama Kanumba sasa angetakiwa kukaa kimya kama alivyosema amemzika mwanaye rasmi, basi ashukuru kama alivyowahi kushukuru kwenye misiba mingine na kuamini kuwa Mungu ametenda.

PICHA: Wema Sepetu Na Muonekano Wa Ujauzito, Mashabiki Wamuombea

Malkia wa filamu nchini, Wema Sepetu ameshare picha katika mtandao wake wa kijamii akiwa na muonekano kama ni mjamzito huku picha hiyo ikionekana wazi kwamba ni ujio wa movies yake mpya.
Wema Sepetu akiwa kazini
Muigizaji huyo mwenye mashabiki wengi katika mitandao ya kijamii, alipost picha hiyo na kuandika ujumbe “Sinema Zetu International Film Festival here we Come… (SZIFF). Download WemaApp only Playstore. Dont mind my Vitunguu,”
Mashabiki wengi wameonyesha kuguswa na picha hiyo kutokana na mwanadada huyo kudaiwa kwamba hashiki mimba kutokana na kukaa muda mrefu bila kupata mimba.
Haya ni maoni ya mashabiki hao.
Aikamtaita: I wish uwe hivyo na Mungu akukuzie .Mungu anajibu maombi.
Angella_elias: Dear wema I play fo u Nitafurahi Siku ukiwa na kibend Wallah yn nitachizika @wemasepetu
Abrina6064: Madam nakuombeaa iwe kwel siku moja in shall Allah 😍😍
Tinnahcosmo: Mungu afungue milango ktk uzazi wako ili siku moja na ww uitwe mama nakupenda na nakuombea mungu akupe mtoto tu jaman najua iyo ndo itakua furaha tosha ya maisha yako
Montanarizy_anny: Mimba imekupendeza naomba mungu akuzidishie ndoto zako siku moja zitimie dada @wemasepetu my love inshalah mungu atakufanyia wepesi

PICHAZ:: Mume Wa Uwoya Azikwa Nchini Rwanda, Mamia Wajitokeza Kumzika

Wachezaji wa timu ya Rayon Sports Ismailla Diarra (kushoto) na Tidiane Kone (kulia),wakiwa wamebeba mwili wa marehemu  Hamadi  Ndikumana Katauti kutoka nyumbani kwake Nyakabanda kwenda katika Msikiti Qaddafi uliopo Nyamirambo, Rwanda na baadaye walifanya mazishi jana jioni.
Baba mzazi wa Ndikumana baada ya kuwasili nyumbani kwa aliyekuwa mwanae, Ndikumana akitokea burundi.
Mama mzazi wa Ndikumana akisadiwa amebebwa baada ya kufika Nyumbani kwa mwanae Rwanda akitokea Burundi.
Majirani wakiwa wanalia.
Watoto wakiwa barabarani kuaga mwili wa Ndikumana wakati ukipelekwa katika Msikiti wa Qaddafi  uliopo Nyamirambo, Rwanda.
…Safari ya Kupeleka mwili wa marehemu msikitini ikiendelea.
Ndugu wa Ndikumana akilia kwa uchungu.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa barabarani wakati wa kusindikiza mwili wa marehemu

Mwili wa nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda, Hamadi  Ndikumana Katauti (39)   amezikwa jana kufuatia kufariki  nyumbani kwake usiku wa kuamkia juzi,  nchini Rwanda katika makaburi  yaliokuwepo kwenye mji wa Nyamirambo, Rwanda.
Ndikumana ambaye  alikuwa mume wa muigizaji wa filamu nchini, Irine Owoya amezikwa na mamia ya wadau wa soka nchini humo wakiwemo mashabiki wa klabu ya Rayon  Sport ambayo alikuwa akifanyia kazi kama kocha msaidizi.

Breaking News: Mume wa Zamani Wa Irene Uwoya Afariki Dunia


Staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya, akiwa na aliyekuwa mume wake Hamad Ndikumana.
ALIYEKUWA mume wa muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya, mchezaji Hamad Ndikumana (39) kutoka nchini Rwanda amefariki usiku wa kuamkia leo, chanzo cha kifo chake kikisemekana ni matatizo ya moyo ambapo jana alikuwa akiendelea na kazi zake kama kawaida.
kujua chanzo cha kifo Bofya hapa
Mpaka anakutwa na umauti alikuwa akicheza katika timu ya APOP Kinyras Peyias FC ya Cyprus. Alizaliwa Oktoba 5, 1978 na mpaka anafariki dunia alikuwa ametengana na Uwoya kwa mingi na alikuwa ndiye mkewe waliyefunga naye ndoa katika Kanisa Katoliki na walibahatika kupata mtoto mmoja ambaye jina lake ni Krish.

Afande Sele Arudisha Majibu Kwa Mrisho Mpoto


Baada ya msanii wa muziki wa asili nchini Mrisho Mpoto kumtaka rapa Afande Sele kuacha kumtaja marehemu Steven Kanumba kwa mambo mabaya, rapa huyo mwenye makazi yake mkoani Morogoro amemtaka Mrisho Mpoto kuacha mambo ya kizamani.

Wawili hao wamefikia hatua hiyo baada ya jana rapa Afande Sele kuandika ujumbe wa kusikitika baada ya kusikia Elizabeth Michael ‘Lulu’ kahukumiwa miaka miwili jela kwa kosa la kumuua aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba bila kukusudia.

Katika ujumbe wa Afande alidai yeye hakuhudhuria mazishi ya staa huyo wa filamu kwa madai alimsababishia Lulu matitizo kauli ambayo ilipingwa na Mrisho Mpoto kwa kudai marehemu hasemwi kwa mabaya.

Baada ya kauli hiyo, Afande Sele amerudi upya na kumjibu Mrisho Mpoto.

Jaji Aeleza Utetezi Dhaifu Ulivyompeleka Lulu Jela


Jaji wa Mahakama Kuu, Sam Rumanyika jana ameeleza jinsi ushahidi wa upande wa utetezi ulivyomfanya Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Rumanyika alisema kuwa ingawa ushahidi wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo ulikuwa ni wa kimazingira, mshtakiwa alikuwa na jukumu la kueleza ni masaibu gani au mazingira gani yalisababisha kifo cha Steven Kanumba kwa kuwa ndiye alikuwa mtu wa mwisho kuwa naye.
Alisema kuwa hata hivyo msanii huyo kwa kuwa ndiye alikuwa mtu wa mwisho kuwa na marehemu hakuweza kutoa maelezo ya kujitosheleza hivyo akamtia hatiani kwa kwa kutumia kanuni hiyo mtu wa mwisho kuwa na marehemu kupatikana na hatia asipotoa maelezo ya kuridhisha.
Baada ya Jaji Rumanyika kumtia hatiani msanii huyo, wakili Peter Kibatala alijitahidi kumuombea msamaha ili apunguziwe adhabu huku akiisihi Mahakama imhukumu kifungo cha nje.
Pamoja na mambo mengine Wakili Kibatala alisema kwamba mshtakiwa ni mara yake ya kwanza kutenda kosa hilo kama ambavyo upande wa mashtaka ulivyosema na kwamba wakati wa tukio hilo alikuwa bado mtoto ambaye alihitaji kuongozwa vema hata na Kanumba.
Wakili Kibatala aliongeza kuwa hata hivyo kwa sasa msanii huyo alishajirerekebisha na kurudi katika mstari na kwamba kwa kuwa ndiye anayetegemewa na mama yake na wadogo zake wengine katika kuwahudumia.
Hata hivyo, utetezi huo hasa wa kuomba afungwe kifungo cha nje haukufanikiwa kwani wakati akitoa adhabu hiyo Jaji Rumanyika licha ya kusema kwamba pamoja na kuzingatia mambo yote hayo, anamhukumu kifungo cha miaka miwili jela.
“Uwezo wa majaji katika kutoa hukumu kimsingi hauna kanuni lakini kuna vitu vya kuzingatia na moja ya vitu hivyo ni kwamba wahalifu kama alivyo mshtakiwa ni zao la jamii,” alisema Jaji Rumanyika na kuongeza:
“Pamoja na mambo mengine Mahakama iliyoyazingatia, ninamhukumu mshtakiwa kifungo cha miaka miwili jela.
Usipitwe na Habari Muhimu, Install App  Yetu


Android ===>  Bofya hapa
Kabla ya kufikia hatua hiyo ya kumtia hatiani na kisha kumhukumu adhabu hiyo, Jaji Rumanyika alianza kwa kufanya uchambuzi wa ushahidi wa pande zote na kisha kuainisha udhaifu wa utetezi wa mshtakiwa huyo.
Alisema ushahidi wa upande wa mashtaka ambao ulitolewa na mashahidi wanne ulikwa ni wa kimazingira tu na kwamba hakuna hata chembe ya ushahidi wa moja kwa moja yaani kushuhudia tukio.
Jaji Rumanyika alisema: “Hata yeye mshtakiwa alikiri kuwa ndiye aliyekuwa mtu wa mwisho kuwa na marehemu, ambaye alikuwa mpenzi wake kwa miezi minne;
Alisema katika ushahidi wa kimazingira isipokuwa mshtakiwa hatatoa maelezo ya kutosheleza kuelezea masaibu au mazingira ya kifo hicho ndo atakuwa na hatia. Hata hivyo alisema msimamo huo wa kisheria hauwezi kuchukuliwa kuwa mshtakiwa ni lazima athibitishe kutokuhusika.
“Ushahidi huo wa kimazingira haumtii hatiani isipokuwa tu kama unaendelea kumnyooshea kidole mshtakiwa kwamba ni yeye pekee ndo alitenda kosa,”
“Nikiangalia maelezo ya mshtakiwa kuona kama yanakidhi viwango shahidi wa kwanza Seth Bosco alisema kile ambacho hata mshtakiwa alikubali kuwa na ugomvi mshtakiwa na marehemu Kanumba.
Alisema kamusi inafafanua kugomba ni patashika baina ya watu wawili huku mmoja aki-resist hiyo hali. Jaji Rumanyika alisema kwa maoni yake hiyo ndio tafsiri ya ugomvi basi mmoja kuanguka ni moja ya mambo yanayotarajiwa au mmoja kumsukuma mwingine;
“Mshtakiwa alisema kuonyesha kuwa marehemu alikuwa mlevi, kama inavyojulikana matokeo ya mlevi ni pamoja na kuanguka. Mshtakiwa ana jukumu la kutoa maelezo ya kujitosheleza lakini alijikanganya;
“Alisema marehemu alimfukuza hadi akamkamata umbali wa zaidi ya mita 27, akafanikiwa kumkamata, kumburuza hadi chumbani. Hakuwahi kusema wakati akimfukuza umbali huo, mlevi huyu alipata kuanguka.|”
Akizungumzia maelezo ya ushahidi wa Josephine Mshumbusi yaliyopokewa mahakamani kama kielelezo cha ushahidi wa mshtakiwa, Jaji Rumanyika alisema maelezo hayo hayana ushahidi mwingine wa kuyaunga mkono na kwamba hivyo unaacha mashaka.
Alisisitiza kuwa maelezo hayo si cheti cha hospitali na hivyo hayana hadhi ya kuchukuliwa huku akisema kuwa haikuwahi kusemwa kuwa Mshumbusi alikuwa ni mmoja wa madaktari binafsi wa Kanumba, isipokuwa Dk Paplas Kagaiya.
Alisema hata ilitarajiwa kuwa Kagaiya angeeleza historia ya Kanumba (kuhusu kuwa na maradhi ambayo yalielezwa katika maelezo ya Mshumbusi)
Alisema hata mshtakiwa kama mpenzi wa Kanumba kwa miezi hiyo minne kuwa anajua historia hiyo ya marehemu Kanumba lakini naye hakuweza kuyaeleza.
Kuhusu madai ya msanii huyo kupigwa na Kanumba alisema kuwa hilo linakinzana na hekima na busara ya kawaida kwamba hakuthubutu kumrudishia kumpiga wala kumsukuma.
“Ni kama alichukua utaratibu wa kibiblia kwamba anayekupiga shavu la kulia unamgeuzia na shavu la kushoto;
“Nini kilitokea tunabaki na watu wawili tu ama yeye mshtakiwa au marehemu lakini hata marehemu akifufuka Mahakama haitakuwa na mujiza wa kuchukua ushahidi wake;
“Pengine mwingine anaweza kusema kuwa wakati ule mshtakiwa alikuwa na miaka 17 hivyo alikuwa mtoto na alifanya asichokijua. Kesi hii ina mazingira tofauti, mshtakiwa alikuwa mtoto lakini kielelezo kinaonyesha aliitwa mke wa marehemu na akiitika;
“Alikuwa anathubutu kufanya kinyume cha maelekezo ya wazazi wake, mshtakiwa ni aina ya mtoto anayeweza kutoka kwa wazazi wake na kwenda kutembea na wenzake usiku wa manane, anakwenda kwa mpenzi wake, hivyo huyu si yule anayelengwa kulindwa na Sheria ya Mtoto,”alisema Jaji Rumanyika na kuongeza
“Kama mtoto kwa umri anaweza kufanya mambo ya watu wazima ipo siku Mahakama hii itajaa watu wazima waliofanya mambo ya watoto wakaomba kinga ya Sheria ya Mtoto.”
Alisema, “sheria inakusudia kuleta udhibiti wa kufanya mambo yasiyo sawa na inapowezekana kuyafanya yafanywe kwa tahadhari kiasi;
“Itoshe tu kusema kwamba mshtakiwa ameleta utetezi wake marehemu alikuwa na wivu uliovuka mipaka usio na msingi ndo ilipotokea kupigwa.”
Jaji Rumanyika alisema hakuna mchezo usio na kanuni kama mapenzi ni mchezo, wivu ni moja ya kanuni hivyo mshtakiwa hakuwa na chaguo, alishaingia kwenye mchezo huo.
“Bahati mbaya wivu wa kimandeleo huleta maendeleo, wivu wa kimapenzi huleta maangamizi”
“Mshtakiwa alishafahamu marehemu alikuwa na wivu, kama alimfahamu kwa kiwango hicho pia marehemu alipomshuku kwa simu ya kimapenzi hakuacha.”
“Hivyo nalazimika kumtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia chini ya kifungu cha 195 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai.”
Jaji Rumanyika alitumia muda wa dakika 50 kusoma hukumu hiyo kuanzia saa 4:15 alianza kusoma hukumu hiyo kwa kutoa muhtasari wa kesi mpaka saa 5:05, alipotamka adhabu hiyo dhidi ya mshtakiwa.
Hukumu hiyo ilisababisha vilio vya huzuni kwa wazazi, ndugu jamaa na marafiki wa msanii huyo kwa upande mmoja, huku mama wa marehemu Kanumba, Florah Mtegoa akiangua kilio kwa furaha akieleza kuwa Mahakama imetenda haki na kwamba sasa anakwena makaburini kumzika rasmi mwanaye.
Msanii huyo aliondolewa mahakamani hapo kupelekwa gerezani katika gereza la Segerea saa 7:38 kwa kutumia gari la Polisi aina ya Toyota Landcruiser, double cabin.
Wakata rufaa
Muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kumuhukumu Lulu, msanii huyo alianza mapambano upya kuhakikisha anarejea tena uraiani kwa njia ya dhamana na rufaa.
Lulu kupitia kwa mawakili wake alianza mchakato wa kujinasua kutoka katika adhabu hiyo, baada ya kuwasilisha mahakamani hapo taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufani.
Mmoja wa mawakili wa msanii huyo, Peter Kibatala alilieleza Mwananchi kuwa hawakuridhika na hukumu hiyo na kwamba tayari waliwasilisha mahakamani hapo taarifa hiyo ya kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga hukumu ya Mahakama Kuu kumtia hatiani na kumhukumu adhabu hiyo.
“Tayari tumeshawasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa mahakamani (Mahakama Kuu) hivyo kilichobakia ni process (taratibu nyingine tu za kimahakama,” alisema Wakili Kibatala.
Kibatala alisema kuwa mbali na kukata rufaa pia watawasilisha maombi ya dhamana ili wakati anasubiria usikilizwaji na uamuzi wa rufaa yake akiwa nje.
Taarifa Zaidi
Kanumba alifariki dunia April 7, 2012, kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo wake lijulikanalo kwa kitaalamu kama Brain Concussion, lililosababisha mfumo wa upumuaji kushindwa kufanya kazi.
Alipatwa na tatizo hilo wakati wa ugomvi ulioibuka baina yao usiku huo nyumbani kwake Sinza Vatcan, kutokana na wivu wa kimapenzi, baada ya kumtuhumu mpenzi wake huyo kuongea na simu na mwanaume mwingine.

Idriss Sultani Aibuka Na Hili ,Aandika Maneno Mazito Kwa Kanumba

Muigizaji na mchekeshaji Bongo, Idris Sultan ameandika barua ya wazi kwenda kwa aliyekuwa muigizaji wa filamu nchini Steven Kanumba.
Katika barua hiyo, Idris ameonyesha kuwa amewahi kuwa shabiki mkubwa wa marehemu na alihudhuria mazishi yake mwaka 2009. Kabla ya kuandika ujumbe huo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, muigizaji huyo aliyepata dili la kuigiza filamu Hollywood alianza kwa kupost video akiwa na muigizaji Elizabeth Michael aliyehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.
Usipitwe na Habari Muhimu, Install App  Yetu


Android ===>  Bofya hapa
Dear Kanumba,
Najua ulikua hunijui ila nilitembea kwa miguu kutoka mbezi kimara mpaka kinondoni kuja kukuzika. Ni mda mrefu sana umekua ukitembea na sisi kuomba upumzishwe, sasa naamini utapumzika kabisa. Allah akufanyie wepesi na milele utabaki mioyoni mwetu. Tulifunga njia, kazi na hata kuhema vizuri wengine tulishindwa na tukapata depression kubwa sanaaaa yote kwasababu ulitugusa katika mfano usioelezeka. Naamini haki yako sasa imepatikana na namuombea sana mama yako apewe nguvu na amani ya moyo. Finally Rested.
Ni mimi wako katika matumaini ya urithi wa ufalme wa movie Tanzania, Idris Sultan

Mange Kimambi Afunguka Baada Ya Lulu Kuhukumiwa Kifungo Cha Miaka Miwili Jela


From @mangekimambi_ - Breaking newzzzzzzzz..... Lulu amekutwa na hatia ya kuuwa bila kukusudia na amehukumiwa miaka miwili jela.......
.
.
.
Dah huyu jaji anawaza kama mimi posti yangu niliyoposti masaaa mawili yaliyopita nilisema ningekuwa jaji ningemkuta na hatia ila ningempa adhabu ndogo mwaka mmoja au miwili jela.......
.
.
Jaji ametenda haki....
.
.
Sio kama nimefurahi Lulu kafungwa nilichotaka ni kuona hakuna double standards, nilitaka kuona haki inatendeka. Na Lulu ana deserve hiyo miaka 2 jela labda itampa muda wa kufikiria how her actions affected Mama Kanumba na familia yake. Labda akitoka atakuwa more humble......
.
.
.
Lakini still mwanasheria wa serikali achukulie hatua za nidhamu na afukuzwe kazi!! Alijaribu sana kusabotage kesi ili amsaidie mtuhumiwa......
.
.

Usipitwe na Habari Muhimu, Install App  Yetu


Android ===>  Bofya hapa

PS: December Magu anatoa misamaha kwa wafungwa, sidhani kama atawasahau wafungwa wa kumpa kiki ya kufungia mwaka kama Lulu na kina Babu Seya maana ile barua ya kina Baba Seya had Bashitel written all over it."

VIDEO:Hali Ya Sasa Ya Vengu Wa Orijino Komedi

kuhusu hali ya afya ya sasa ya Vengu ambae tulimfahamu kwa kazi yake ya uchekeshaji kwenye kundi la Orijino Komedi.
Baada ya Vengu kutoendelea kuonekana hadharani kwa miaka, Seki ambae ni kiongozi wa kundi hilo amesema>>> “Vengu ameshavuka hatua za kukaa Hospitalini na sasa yuko nyumbani anamalizia hatua nyingine ya matibabu ambayo ni nje ya Hospitali“
Tazama hii video hapa chini kupata maelezo zaidi…

Usipitwe na Habari Muhimu, Install App  Yetu


Android ===>  Bofya hapa

Keisha Atoa Ushahidi Wenye Utata Ndoa Ya Dogo Janja, Uwoya



Mwanamuziki Keisha amejichanganya kuhusu suala la ndoa kati ya Dogo Janja na mwigizaji, Irene Uwoya akitoa maelezo tofauti kuhusiana na ushiriki wake katika kufanikisha shughuli hiyo.
Awali Keisha akihojiwa mwanzoni mwa kipindi cha Leo Tena cha leo Ijumaa kinachorushwa na kituo cha Redio Clouds amesema alishiriki kumfuata bibi harusi nyumbani kwao baada ya watangazaji kutaka kufahamu kwa nini ndoa haikufungwa huko.
Keisha akimsaidia Dogo Janja kujibu swali hilo alisema: “Nilikuwa mmoja wa waliokwenda nyumbani kwa kina Irene kumfuata kisha tulimpeleka katika eneo la siri ilipofungwa ndoa, unajua mimi ni kama mama au dada mkubwa wa Abdul ( Dogo Janja) kwa sababu Madee ni kama baba yake asingweza kwenda peke yake.”
Usipitwe na Habari Muhimu, Install App  Yetu


Android ===>  Bofya hapa
Lakini watangazaji walipoendelea na mahojiano Keisha alibadilisha kauli yake akisema hata yeye hakuwa akifahamu anayeolewa ni nani na pia hakuamini iwapo ni tukio la kweli mpaka aliposhuhudia tendo zima.
“Nilipofika nilimuuliza Johari (mwigizaji) ambaye alikuwa mmoja wa mashahidi iwapo ni ndoa kweli na siyo filamu. Johari alisema siwezi kukudanganya hii ndoa kweli. Mimi nimeolewa kwa hiyo niliposhuhudia tukio zima nikajiridhisha kuwa ile ndoa haswa,” amesema Keisha

Mpenzi Mwingine wa Zamani wa Irene Uwoya Amtumia Ujumbe Dogo Janja


Mwanamuziki na aliyewahi kuwa mpenzi wa muigizaji Irene Uwoya, Msami Baby amempongeza msanii mwenzake Dogo Janja kwa kufunga ndoa na muigizaji huyo huku akiwasifu kwamba wameweza kuwabadilisha watu kuhusiana na umri.

Msamii ametoa pongezi hizo leo kwenda kwa wawili hao baada ya Dogo Janja kukiri kwa kinywa chake kwamba tukio linaloonekana kwenye picha mbalimbali siyo kiki kama watu wanavyodhani bali ni ndoa kweli.

Msamii ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba  "Ndoa ni jambo la kheri sana, pongezi kwako Dogo Janja na Irene Uwoya mmefanya watu wajue umri ni 'number' tu ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi" aliandika  Msami

Msami aliwahi kuwa kwenye mahusiano na muigizaji Irene Uwoya ambapo karibuni alipokuwa kwenye kipindi cha FNL kinachorushwa kila Ijumaa alipoulizwa kuhusu mahusiano yake na Uwoya alidai walishaachana na kudai kwamba Uwoya ndiye aliyemtongoza mpaka kufikia kuwa wapenzi.


Uwoya Aamua Kufunguka Kuhusu Kuolewa Na Dogo Janja

MSANII wa filamu nchini Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi juu ya tetesi iliyopo mtaani kuhusu kuolewa na msanii wa muziki wa bongo fleva Dogo Janja na kusema ni kweli ameolewa na msanii huyo kwani ndiye mwanaume wa ndoto yake.
Irene Uwoya.
“Nimeolewa na mwanaume wa ndoto zangu, bado naendelea kulia na kutokwa na machozi ya kwa furaha. Dogo Janja nakupenda sana na nimefurahi kumaliza maisha yangu ya duniani nikiwa na wewe” aliandika Irene Uwoya.

Kufuatia ujumbe huu ni wazi kuwa Irene Uwoya atakuwa amejibu maswali ya watu wengi ambao walikuwa hawaelewi nini kinaendelea kufuatia tetesi kuwa watu hao wamefunga ndoa siku za karibuni.

Mwakyembe Amteua Alberto Msando kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki.


Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amemchagua Mwanasheria na mdau wa masuala ya Sanaa Alberto Msando kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki.

Katika tarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara Bi Leah Kihimbi kuhusu uteuzi huo wa Msando imesema kwamba uteuzi huo umetokana na vikao vilivyofanywa na wadau wa sanaa pamoja Mh. Waziri Mwakyembe.

Kwa upande wa Alberto Msando ambaye amepatiwa nafasi hiyo na serikali ameahidi kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria za nchi zinalinda haki za wasanii na kuhakikisha wasanii wanafaidika na kazi zao.

Msando ameandika  "Ulaya na Marekani wasanii wengi sio masikini. Hapa kwetu wasanii wengi ni majina tu. Wengi wanaishi maisha ya 'naomba nitoe niko vibaya'. ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria zetu zinalinda haki za wasanii".

Ameongeza "Harrison Mwakyembe tutafanya kazi uliyotutuma"

Msando mara nyingi amekuwa mbele katika kuwasaidia wasanii kwenye masuala yanayohitaji msaada wa kisheria. 

Sababu Zilizowafanya Wazee wa Baraza Wamtie Hatiani Lulu Michael

Wazee wa baraza wameieleza Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuwa mwigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu amehusika kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Wakitoa maoni yao jana baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, wazee hao walieleza kuwa Lulu ndiye aliyesababisha kifo cha mpenzi wake huyo wakati wa ugomvi baina yao usiku wa Aprili 7, 2012.

Wakizungumza mmoja baada ya mwingine, wazee Omary Panzi, Sarah Lugoma na Rajabu Mlawa, walihusisha tukio la Kanumba kujibamiza kichwa ukutani na kusukumwa na mshtakiwa.

“Kutokana na sababu na uainishi wa kesi (ushahidi) wa pande zote, mimi kwa upande wangu nimeridhika kuwa Elizabeth (Lulu) ameua bila kukusudia,” alisema mzee Mlawa na kuongeza: “Katika ugomvi, inawezekana hekaheka za kujinusuru, alitumia nguvu kumsukuma Kanumba na kuanguka ukutani. Hivyo, kwa maoni yangu kosa la kuua bila kukusudia kwa Elizabeth limethibitika.”

Akitoa maoni yake, Sarah Lugoma alisema Kanumba alifariki dunia kutokana na ugomvi baina yake na mpenzi wake (Lulu) kwa kuwa ndani kulikuwa giza, Kanumba aliteleza wakati wa ugomvi huo akaanguka.

“Hivyo mshtakiwa aliua bila kukusudia,” alisisitiza Lugoma wakati akihitimisha maoni yake.

Mzee mwingine, Panzi alisema Kanumba aliteleza na kuanguka wakati wa ugomvi huo, mshtakiwa ndiye aliyehusika na kifo chake kwa kuua bila kukusudia.

Hata hivyo, maoni ya wazee hao wa baraza siyo hukumu halisi ya Mahakama bali yanayotokana na mtazamo wao tu katika hali ya kawaida nje ya sheria kwa namna walivyousikiliza ushahidi wa pande zote.

Hivyo, kumtia hatiani mshtakiwa huyo hakumaanishi kuwa tayari ana hatia kwa kuwa maoni hayo hayamfungi jaji katika hukumu yake ambaye huongozwa na sheria husika.

Kwa hiyo, hatima ya msanii huyo kama ana hatia au la itabainishwa na Mahakama Novemba 13 wakati Jaji Sam Rumanyika anayesikiliza kesi hiyo atakapotoa hukumu.

Jaji Rumanyika aliwakumbusha wazee hao muhtasari wa ushahidi uliotolewa na pande zote kabla ya kutoa maoni yao.

Jaji Rumanyika akieleza kwa ufupi kilichozungumzwa na kila shahidi wa pande zote, alitoa mwongozo kwa wazee hao pamoja na mambo mengine, kutoa maoni yao bila kuongozwa na huruma wala kuogopa chochote.

“Mnalo jukumu la kutoa maoni yenu bila kuongozwa na huruma wala vitisho. Mnatakiwa kutoa maoni yenu kwa mujibu wa ushahidi mliousikia,” alisema Jaji Rumanyika.

Aliwaeleza kuwa kama walivyosikia ushahidi wa upande wa mashtaka kuwa umejikita kwenye ushahidi wa kimazingira, mshtakiwa ndiye aliyekuwa mtu wa mwisho kuwa na Kanumba.

Alisema ushahidi wa kimazingira lazima uwe ni vipande ambavyo ni mnyororo (muunganiko) unaomhusisha mshtakiwa kuwa ndiye ametenda kosa.

“Kama mkiona kuwa mshtakiwa ametoa maelezo ya kutosheleza basi mnaweza kusema hana hatia, lakini kama mna maoni tofauti pia mtaniambia,” alisema Jaji Rumanyika na kuongeza:

“Mkiona kuwa kifo hicho kilitokana na ugomvi, basi shtaka lake huwa ni la kuua bila kukusudia, mkishawishika kwa vyovyote na kwa namna yoyote ile mshtakiwa hakuhusika na kifo hiki msisite pia kunipa maoni yenu.”
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017