Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter
Showing posts with label MAAJABU. Show all posts
Showing posts with label MAAJABU. Show all posts

Waombolezaji Watimua Mbio na Kulitelekeza Jeneza Lenye Mwili wa Marehemu

Waombolezaji Watimua Mbio na Kulitelekeza Jeneza Lenye Mwili wa Marehemu

PICHAZ:Hizi Ndizo Barabara 10 Za Hatari Duniani, Zinatisha

Vipo vitu vingi vya kushangaza na kustaajabisha duniani moja wapo ikiwa ni miundombinu mbalimbali iliyotengenezwa kwenye nchi mbalimbali duniani. tunakuletea barabara 10 za hatari zaidi duniani.
10. Sichuan-Tibet – China
Related image
Related image
9. The Stelvio – Italy
Image result for The Stelvio Pass - Italy
Image result for The Stelvio Pass - Italy
8. Los Caracoles – Chile
Image result for Los Caracoles Pass, Chile
Image result for Los Caracoles Pass, Chile
7. Skippers Canyon – New Zealand
Image result for Skippers Canyon Road
Image result for Skippers Canyon Road
6. The Zoji Pass – India
Image result for The Zoji Pass
5. Guoliang Tunnel – China
Related image
Image result for Guoliang Tunnel Road - China
4. The Karakoram – between China and Pakistan
Related image
Image result for The Karakoram Highway, between China and Pakistan
3. James Dalton – Alaska
Related image
Image result for James Dalton Highway, Alaska
2. Jalalabad–Kabul – Afghanistan
Related image
Image result for 2. Jalalabad–Kabul Road - Afghanistan
1. North Yungas – Bolivia
Image result for North Yungas Road
Image result for North Yungas Road

MAAJABU:: Tajiri Bongo Ajiandalia Kaburi Kubwa La Mamilioni..Tazama Picha Zaidi

Mganga wa tiba asili maarufu ‘dokta’ Antony Mwandulami.

IRINGA:Mshangao! Mganga wa tiba asili maarufu ‘dokta’ Antony Mwandulami, mkazi wa kijiji cha Itunduma Wilaya ya Njombe mkoani Iringa ametoa mpya ya kufuru baada ya kuamua kujenga eneo la makaburi yake na wake zake watatu ambayo yakikamilika, yatakuwa yamegharimu kiasi cha shilingi bilioni moja.
Akizungumza na Uwazi, Mwandulami alisema ameamua kujenga kaburi hilo kwa lengo la kuweka kumbukumbu kwa jamii yake, familia na hata kazi yake ya utabibu akiwa na wake watatu na watoto kumi na tisa.
Nyumba yake.
Akizungumzia juu ya kaburi hilo na ujenzi wake, mwandulami alisema litakuwa kama nyumba, ambayo imechimbwa chini ambako kumegawanywa sehemu yenye maeneo manne.
“Ukubwa wa kaburi langu ni heka moja, kwani nimejenga ngome kubwa na ndani yake ndiyo kuna eneo la kaburi lililoko chini ya ardhi. Eneo la kaburi ni kubwa kwa sababu kutakuwa na maeneo tofauti” alisema.
“Ninataka kutunza kumbukumbu za kazi zangu ambazo nimezifanya kwa muda mrefu, sitaki jina langu lipotee, hivyo nataka kutengeneza kaburi la kipekee” alifafanua dokta huyo.
“Hili kaburi nimeanza kulijenga kwa miaka tisa sasa, ninategemea kulimaliza mwaka 2018 kwa gharama ya shilingi bilioni moja. Kwa sasa nimefikia hatua nzuri ya ujenzi, kilichobaki ni kufanya ‘finishing’ tu.
Gari lake.
Kaburi moja lina sehemu nne
Alisema kwenye nyumba hiyo ambayo ni kaburi kuna jumla ya makaburi manne, kaburi moja litakuwa lake na mke wake mkubwa lakini pia kuna sehemu nyingine kutakuwa kuna kaburi la wake zake wawili.
“Kama ambavyo nilivyosema awali, nataka kuacha kumbukumbu, kwa hiyo ili kufika kwenye kaburi langu, kuna sehemu ya mapokezi, na sehemu zingine za kupumzika kwa wageni watakaotembelea kaburini ambalo liko kiasi cha mita 30 chini ya ardhi,” alisema.
Kaburi lake.
“Ninaagiza marumaru mbalimbali kutoka Sweden kwa ajili ya kumalizia makaburi hayo. Hizi zitasaidia kutunza mwili wangu kwa muda mrefu ili vizazi na vizazi waweze kuniona na kujifunza kwa huduma nilizokuwa nazitoa wakati wa uhai wangu” alijigamba dokta huyo.
“Watanzania wana woga sana katika kuzungumzia suala la kifo, lakini mimi na wake zangu tumezungumza na wameridhia na kubariki ujenzi huo wa kaburi letu,” alimalizia mtabibu huyo.
-GPL

Aliyetajwa Kufariki Dunia Ajali Ya Ndege Arusha, Yupo Hai

Mfanyakazi wa hoteli za kitalii za andBeyond Serengeti, Moses Muhina aliyetajwa kuwa ni miongoni mwa abiria waliofariki dunia katika ajali ya ndege ya Shirika la Coastal Aviation, imebainika alibadili ndege muda mfupi kabla ya safari ili kuwahi kazini.


Muhina ambaye ni mwongozaji watalii katika hoteli hiyo, alikuwa aondoke na ndege ya Coastal Aviation saa nne asubuhi lakini viongozi wa hoteli walimbadilishia ndege, hivyo aliondoka na Air Exel iliyofika salama Serengeti.


Akizungumza na gazeti hili, meneja uendeshaji wa Hoteli ya andBeyond Serengeti Under Canvas, Mussa Matala alisema Muhina ambaye anasomeka kwenye orodha ya ndege kama Maina alikuwa apande ndege hiyo lakini walimbadilishia.


Alisema waliomba aondolewe kwenye orodha ya wasafiri wa ndege hiyo lakini kwa bahati mbaya hadi ndege ilipoondoka jina lake lilikuwapo.


Wakati huohuo, raia watano wa kigeni ambao walifariki dunia katika ajali hiyo, akiwamo rubani Dewald Raubenheimer raia wa Afrika Kusini, ambaye kwenye orodha ya awali ya waliofariki jina lake halikuwapo anatarajiwa kusafirishwa leo.


Mhudumu wa chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya mkoa ya Mount Meru, Francis Costa alisema miili mitatu kati ya 11 imechukuliwa na ndugu zao.

Alisema miili iliyochukuliwa ni ya ndugu wawili waliokuwa wakurugenzi wa Masai Wondering, Nasibu na Shatri Mfinanga.

Mwingine ni wa Joyce Mkama ambaye alikuwa mfanyakazi wa Hoteli ya Serena.

“Uchunguzi wa miili ya wageni kutoka nje ya nchi unaendelea na ukikamilika itasafirishwa kwa mazishi katika nchi za Afrika Kusini, Ujerumani na Italia,” alisema.

Ndege hiyo namba 5H-EGG aina ya Cessna Grand Caravan ilianguka baada ya kugonga kingo za creta ya Empakai, umbali wa mita 3,250 kutoka usawa wa bahari ikitoka Kilimanjaro kwenda Hifadhi ya Serengeti.


Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema uchunguzi unaendelea kuhusu ajali hiyo.

Mbwa Wazua Taharuki Kwa Kula Mboga Iliyobandikwa Jikoni


Hali ni tete katika Mji wa Geita baada ya kuwepo ongezeko kubwa la Mbwa wanaozurula mitaani na kutishia usalama wa Wakazi wa mji huo, baada ya mbwa hao kuanza kuvamia makazi ya watu kisha kukamata kuku pamoja na kula mboga iliyobandikwa jikoni kana kwamba hakuna mamlaka zinazohusika.

Mbwa hao wakiwa kwenye makundi makubwa wamevamia familia mbili za wakazi wa mtaa wa Nyanza katika Halmashauri ya mji wa Geita kisha kukamata na kuua kuku watano wa Bw,Benedict James kabla ya kuingia nyumbani kwa Bi,Mariam Agustino kisha  kula nyama kilo tatu iliyokuwa jikoni kwa maandalizi ya  mlo wa mchana hali iliyopelekea familia hiyo kushinda na njaa.

Akiongea kwa njia ya simu,Daktari wa Mifugo wa Halmashauri ya mji wa Geita  Abas Kilonge,mbali na kukiri kupokea malalamiko ya wakazi hao amesema kinachokwamisha zoezi la kuwapiga risasi mbwa hao ni fedha ila akadai mchakato wa  kupata fedha unaendelea.

Walimu Wa Shule Ya Msingi Wajikuta Wamelala Nje


Buchosa. Walimu saba wanaofundisha Shule ya Msingi Soswa wilayani Sengerema wamejikuta wamelala nje pamoja na familia zao huku wawili kati yao wakiwa wamenyolewa nywele kichwani na sehemu za siri.

Mwalimu wa Shule ya Msingi Soswa, Petro Lukas amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamukia leo Jumatano ambapo walimu hao walipokuwa wamelala ndani ya nyumba zao na walipotahamaki usiku walijikuta wamelala nje.

Amesema palipokucha walimu hao walizinduka na kutokuamini kilichotokea na walipoingia ndani ya nyumba zao walikuta damu zimetapakaa vyumbani na sebuleni pia vibuyu vikiwa vimevalishwa shanga nyeupe vikiwa kitandani na chini kitendo kiliwafanya kuhaha kuomba msaada kwa jamii inayowazuguka.

Mwalmu Lukas amesema kati ya walimu hao wawili wameathirika zaidi na tukio hilo na kwa kupata mshituko ambao ni Wape Kisumo aliyenyolewa nywele kichwani pmaoja na Daud Shule ambaye alinyolewa nywele sehemu za siri.

Kutokana na mshtuko huo Kisumo alipelekwa kituo cha afya cha Mwangika kwa matibabu na mwalimu Shule yeye anaendelea na matibabu ya tiba na hali zao zinaendelea vizuri.

Mganga Mkuu Halmashauri ya Buchosa, Dk Ernest Chacha amekiri kumpokea mwalimu Kisumo katika kituo cha afya Mwangika na kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu na baada ya uchunguzi wa kitaalamu kukamilika watatoa taarifa lakini alipofika kituoni alikuwa haongei ila baada ya kupatiwa huduma ya kwanza ameanza kuongea kidogo.

Akizungumzia mkasa huo mwalimu Shule amesema kuwa wao baada ya kupata chakula cha usiku walilala ndani nyumba zao na ilipofika usiku wa manane wakasikia mwalimu mwenzao Wape Kisumo akilia na kulalamika kichwa kinamuuma.

Amesema walipotahamaki walijikuta wakiwa nje watupu na kuona kuwa wamedhalilishwa na kitendo hicho hivyo wanaiomba Serikali iwasaidie kumaliza tatizo hilo.

Mmoja wa wananchi wa Kisiwa cha Soswa, Sumari Diplospa amesema kitendo hicho kinapaswa kukemewa kwa kuwa walimu hao wanasaidia kufundisha watoto wao.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bulyaheke Musa Mwilomba amesema kuwa tukio hilo ni tatu kutokea  katika shule hiyo ambapo mwaka jana mwezi nne walimu walipondwa mawe nyumba zao wakiwa wamelala.

Pia Mei 5 mwaka huu nyumba za walimu zilipondwa tena mawe na usiku wa kuamkia leo wamejikuta wamelala nje na baadhi yao kunyolewa nywele sehemu za siri kitendo ambacho kinapaswa kukemewa.

Kwa upande wake Ofisa Elimu Msingi Halmashauri ya Buchosa, Magareth Kapolesya amesema amepata taarifa ya tukio hilo na kusikitishwa na kitendo hicho na wao kama wasimamizi wa elimu watalishughulikia na kupata ufumbuzi juu ya suala hilo kwa kuwa linawanyima raha walimu na kukosa morali ya kufundisha.

Muhubiri Awalisha Mende Waumini Wake..

Muhubiri mashuhuri anayetumia nyoka nchini Afrika Kusini Penuel Mnguni amewalisha mende ndugu wawili katika mkusanyiko wa kanisa lake akidai kwamba wadudu hao walibadilika na kuwa jibini kwa mmoja wao na kiungo kwa mwengine.
Kisa hicho kinajiri takriban miezi mitano baada ya Mnguni katika ibada ilioandaliwa na Muhubiri wa Nigeria TB Joshua, na kukiri kulingana na bwana Joshua kwamba kuwalisha watu haijaandikwa katika biblia.
Kanisa la Bwana Mnguni lilichapisha katika mtandao wa facebook kuhusu kisa hicho cha kula mende mapema mwezi huu akisema kuwa muhubiri huyo alimwita mende kuja katika kanisa hilo.
Baadaye aliwaita wafuasi wa kanisa hilo kujitokeza mbele na kula….ndipo ndugu wawili walijitokeza na kula pamoja…na walipokuwa wakila bwana Charles alihisi anakula jibini huku Bwana Eric akihisi kula kiungo, chapisho hilo lilisema.
Nabii huyo aliyejitangaza alizua utata nchini Afrika Kusini 2015 baada ya kushutumiwa kwa kuwalisha nyoka wafuasi wake.

Auawa Kwa Kupigwa Risasi Akisafirisha Ng'ombe Anayeaminiwa Kuwa Ni Mungu

Viongozi wa kijamii katika mji wa Rajasthan nchini India wanasema mtu mmoja ambaye ni muislam ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaoamini ng'ombe kuwa mungu wao.

Ummar Khan alikua akisafirisha ng'ombe yeye na mwenzake katika kitongoji cha Alwar wakati walipovamiwa na wahindu.

Wanasema kwamba mwili wa kijana huyo ulitupwa karibu na reli kuharibu ushahidi.
Usipitwe na Habari Muhimu, Install App  Yetu


Android ===>  Bofya hapa
Polisi katika mji wa Rajasthan wameanzisha upelelezi juu ya tukio hilo.Umekuwa ni utamaduni wao tokea enzi na enzi

Wahindu huamini kuwa ng'ombe ni mungu kwao na huwachukulia kwa namna ya upekee sana.


Zaidi ya watu kumi wameuawa tokea mwaka 2015 kwa sababu kama hizo.

Wanafunzi Wawili Watangaza Kuuza Bikra Zao Sh.Mil 52 Mtandaoni Ili Kulipia Ada Ya Chuo...Ingia Hapa Utie Dau

Wanafunzi wawili wa kike kutoka nchini Uholanzi wametangaza kuuza bikira zao mtandaoni ili kuweza kulipia ada ya chuo
Lola amesema amekosolewa na wasichana wenzake mtandaoni lakini amesema haogopi hilo kwani wanawake wengi hawajaolewa na wanaume waliowatoa bikira ndio maana haitaji kuitunza hadi kuolewa.
“Wenzangu wananicheka ila kwa uelewa wangu ni kwamba sijawahi kusikia mwanamke kaolewa na mwanamme aliyemtoa bikira hivyo nimeamua kuuza tu usichana wangu ili nisijekuumizwa na mtu ambaye ataniacha baadaye.“amesema Lola.
Kwa upande rafiki yake na Lola, Monica (20) yeye amesema kuwa haoni mtu anayestahili kumpatia bikira yake hivyo ni bora akaiuza ili aweze kulipia masomo yake ya chuo.
Hata hivyo wataalamu wa masuala ya kisaikolojia nchini Uholansi wanasema kuwa wanaamini wasichana hao sio mabikira kama wanavyodai bali wanafanya udanganyifu taarifa ambazo zinapigwa na mmiliki wa mtandao wa  Cinderella Escorts ambaye amesema kuwa ameshawafanyia vipimo kwa njia ya mtandao na kuwaona ni mabikira.
Hatua ya wasichana hao imekuja baada ya msichana mmoja mwanafunzi kutoka nchini Uingereza aliyetambulika kwa jina la Jasmin kuuza bikira yake kwa dola $100,000 mwaka jana.
Majina ya wanafunzi hao yaliyotumika kwenye habari sio sahihi kwa ajili ya usalama hata chuo pia hakijatajwa. Unaweza kuingia HAPA kupanda dau kwa wewe mwanaume mwenye milioni 52

Fahamu Historia Ya Kijana Aliyezaliwa Bila Mapaja.

Kijana anayefahamika kwa jina la Nathan Hirdlicka ambaye hivi karibuni ametawala mitandaoni kutokana na hali yake ya ufupi na kuzaliwa bila kuwa na mapaja kama watu wengine, na kumuoa msichana wa kinaigeria ambaye ni mrefu.
Nathan mwenye umri wa miaka 34 Raia Santa Fe Mexico na amepatwa kuumwa huo ugonjwa aina ya (Proximal focal deficiency) ambapo imemsababishia akawa hivyo.
Hata hivyo anavyotembea huwa hatakiwi kutembea kwa umbali mrefu sana kutokana na tatizo lake kwani akietembea kwa muda mrefu anaweza kupata maumivu makali.
Aidha watu wa aina hiyo Duni anzima wapo 25 na ni jambo linalomfanya ajisikie vizuri na kujiona yupo wa kipepee tofauti na watu wengine kutokana na wao kuwa wachache.
Kijana huyo huchukizwa na watu wanaomshangaa kutokana na hali na kumtfautisha na watu wengine kutokana na hali ya ufupi wake na kutokuwa na mapaja kama walivyo binadamu wengine.
Hivi karibuni alimuoa Msichana kutoka Nigeria alifahamika kwa jina la Chelsee Stuart ambapo Msichana huyo aliuleza mtandao mmoja wa habari kuwa mwanzo ilikuwa ngumu kwake kukutana na mtu mfupi kama huyo.
Lakini anajisikia furaha kuolewa na mtu huyo na amesema haoni shida kuishi na Nathan akiwa mume wake.

LAANA:Simba wa Jinsia Moja Waliopigwa Picha Wakifanya Mapenzi Nchini Kenya Wazua Gumzo Mtandaoni

Picha zilizosambaa mtandaoni nchini Kenya zilizopigwa kutoka mbuga ya wanyama ya Masai Mara, zikionesha madume mawili ya Simba yakishiriki mapenzi zimezua gumzo mtandaoni nchini Kenya.

Simba hao walionaswa na mpiga picha maarufu duniani, Paul Goldstein zimeleta gumzo nchini Kenya wengi wakishangaa kitendo hicho wakiamini kuwa haijawahi kutokea kwa wanyama.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mkuu wa Bodi ya Uanishaji wa Filamu nchini humo, Dr Ezekiel Mutua amesema ameziona picha hizo na ni kweli tukio hilo limetokea kwenye Mbuga ya Masai Mara huku akikiri kuwa endapo tukio hilo limefanyika kwa Simba hao basi dunia itakuwa hatarini kupoteza baadhi ya viumbe kwa siku za usoni.



Dkt. Mutua amesema kuwa ataagiza wanasayansi kuwachunguza Simba hao na kuwatenga kwenye mbuga hiyo ili kuepusha vitendo kama hivyo kwa Simba wengine.

“Hawa wanyama wanatakiwa wafanyiwe ushauri, huenda walishawahi kuwaona watu wakifanya mchezo huo mchafu hususani watalii mbugani hapo. Wanastahili kutengwa kwenye mbuga hiyo wabaki wenyewe.“amesema Dkt. Mutunga kwenye mahojiano yake na mtandao wa Nairobi News.

Hata hivyo Dkt. Mutunga amesema Bodi yake haihusiani kabisa na masuala ya wanyama lakini kwa tukio hilo hawezi kukaa kimya kulizungumzia.

“Bodi ya (KFCB)  hatusimamii wanyama lakini hatuwezi kuacha kuongelea tukio hilo kwani haijawahi kutokea nchini Kenya kuona simba wawili wanaume wakifanya mapenzi. Kunauhitaji wa tafiti za kina kufanyika ili kuweza kubaini kama Simba hao ni kweli walikuwa wanaume wote.“amesema Dkt. Mutua.

Dkt. Mutunga amedai kuwa vitendo hivyo huwa vinaenea kwa njia ya filamu au Tv, ila anashangaa kwa wanyama kama hao wamewezaji kufikia maamuzi ya kufanya mapenzi ya jinsia moja huku akiamini kuwa kuna nguvu ya shetani imefanya kazi kwa wanyama hao.

“Wapi ulishawahi kuona wanyama wa jinsia moja wakishiriki mapenzi? Nadhani ni nguvu ya kishetani imeingia kwa simba hao.“amesema Dkt. Mutunga.



Mpiga picha wa tukio hilo, Goldstein amesema wakati yupo Masai Mara aliona simba wawili wakilaliana mwanzoni alijua ni jike lakini alipokaribia akakuta yote ni madume na kudai kuwa alishikwa na butwaa kwa kile alichokiona.

“Lilikuwa ni tukio la kustaajabisha machoni mwangu niliwahi kusikia tu kuwa lilishawahi kutokea Botswana lakini kwa niliyoyaona ni mageni mashoni mwangu.“amesema Goldstein.

TUKIO HILO LA WANYAMA WA JINSIA MOJA KUINGILIANA KIMWILI LINAELEZWAJE?

Wanasayansi na Wataalamu wa masuala ya wanyama na wadudu wanasema kuwa kuna baadhi ya wanyama huingilia kimwili bila kujali jinsia.

Mwanazoloji, Petter Bockman akirejea kwenye nadharia za Darwin amesema kuwa wapo wanyama na ndege zaidi ya aina 450 hufanya mapenzi ya jinsia moja ila kwa vile binadamu huwa hatufuatilii ni ngumu sana kuwakuta kwenye hali kama hiyo.

Akitoa mfano wa wanyama na ndege hao amesema kuwa ni Paka, Simba, kuku, kware, Nyangumi na wengine wengi.

Cheki baadhi ya maoni ya wadau mitandaoni baada ya kusambaa kwa picha hizo nchini Kenya.




VIDEO:Mwimbaji Wa Gospel Mbeya Akiimba Kwa Kujimwagia Matope Na Kujipiga Matofali

Aliko ni mwimbaji wa nyimbo za injili kutokea Tukuyu Mkoani Mbeya Tanzania na hii ndo staili yake ya uimbaji anapokuwa jukwaani popote pale kwenye kuimba nyimbo za injili.
Usipitwe na Habari Muhimu, Install App  Yetu


Android ===>  Bofya hapa

Video Fupi Iliyosambaa Mtu Akikata Mitaa Kwa Kuogelea “Maisha Ya Bondeni Life Is No Life”

Tumeshuhudia mara nyingi jinsi hali inavyobadilika kwa watu wanaoishi mabondeni pale mvua inaponyesha Dar es salaam, hii ni moja ya ripoti kutokea upande huo ikimuonyesha mmoja wa Wakazi akiogelea kwa kukatiza mitaa.

Soma Maajabuu Ya Kanisa Linalobatiza Watu Kwa Kutumia Pombe.

Askofu akiwa kashika mizinga ya bia
                                          
Haya ni maajabu na ni ngumu kuamini unaweza sema hivi, kutokana na Kanisa linalo tambulika kwa jina la Gabola limekuwa likibatiza watu kwa kutumia aina  mbali mbali za pombe.
Kanisa hilo lipo nchini Afrika kusini ambapo linaongoza na mtu anaye jiita Askofu Tseitsi Makiti  na ndiye muanzilishi wa Kanisa hilo.
Kwa mujibu wa chanzo cha habarii kinasema Mtu huyo ameeleza anafanya hivyo na kuwakumbusha watu kwamba Yesu alibadili maji na kuwa waini hivyo watambue kuhusu hilo.
“Watu tunaokunywa pombe siku zote tuna furaha na amani hivyo hata watu wanaokuja kwangu kusali wanafuraha muda wote na wanafurahia huduma yangu” amesema

Amesema wamepokea watu kutoka kwenye jamii na wanaendelea kupokea ambapo watu wamekua wakifika kanisani hapo kubatizwa na kuapokea ibata na huku wakiendelea na utaratibu wao wa kunywa pombe.

Msichana Aliyebakwa na Waalimu India Mahututi Baada ya Kuavia Mimba

Msichana Aliyebakwa na Waalimu India Mahututi Baada ya Kuavia Mimba

Msichana wa India ambaye alidaiwa kubakwa na waalimu wawili wa shule katika kipindi cha wiki tatu yuko katika hali mahututi baada ya kulazimishwa kuavia mimba.
Madaktari wameiambia BBC idhaa ya Hindi kuwa ubongo wake umeharibika.
Polisi imemtioa nguvuni Mkuu wa shule yake na mwalimu wake katika jimbo la kaskazini mwa India la Rajasthan.
Polisi wanasema kuwa alipoteza fahamu baada ya washukiwa skumlazimisha kutoa mimba katika hospitali ya kibinafsi.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 18 alilazwa hospitalini baada ya kuhisi maumivu makali ya tumbo na wahudumu katika shule yake wakabaini kwamba alikuwa mjamzito.
Mwathiriwa wa ubakaji wa miaka 13 India aiomba mahakama kutoa mimba

Hali yake ya afya ilianza kuwa mbaya kwa haraka baada ya kuavia mimba, lakini haijafahamika wazi ni nini hasa kilichoifanya hali yake kuwa mbaya,alisema polisi katika wilaya ya Sikar said.
Shule hiyo iliyopo wilaya ya Sikar, imefungwa kwa sasa na mamlaka katika eneo hilo.
Polisi wanaamini kuwa masomo ya ziada yanayotolewa katika saa ambazo si za kawaida yalitumiwa kuwaita wanafunzi ili kuwezesha vitendo kama hivyo vya unyanyasaji kufanyika.
Bado polisi hawajaweza kurekodi taarifa kutoka kwa muathirika.
"Hili ni tatizo baya na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika ,"alisema afisa wa polisi Kushal Singh.

Mwanamke Mwizi Aiba Gari Ya Polisi Baada Tu Ya Kukamatwa…Ilikuaje?Soma Hapa

Katika hali ya kuchekesha kama si ya kushangaza hivi karibuni, mwanamke mmoja  huko Texas nchini Marekani aitwaye Toscha Fay Sponsler mwenye umri wa miaka 33 aliyekuwa amekamatwa na polisi na kufungwa pingu kisha kuwekwa kwenye gari ya polisi hao alijifungua pingu alizokua amefungwa na kuondoka na gari hiyo kwa mwendo wa kasi.
Kabla ya tukio hilo mwanamke huyo alikua amekamatwa kwa kosa la kuiba vitu dukani yaani wakati anafanya shopping na baada ya polisi kumkamata kwa kosa hilo na kumwingiza kwenye gari yao hiyo wakiwa wamemfunga pingu na askari hao kuendelea na shughuli zao nyingine, walishangaa kuona baada ya dakika chache gari yao inaondolewa na mwanamke huyo.
Maaskari hao walijaribu kukimbiza gari hiyo kwa kutumia gari nyingine na baada ya mwendo wa dakika ishirini mwanamke huyo alishindwa kuendelea kuendesha gari hiyo na ndipo maaskari hao walipomkamata na kumtia mbaroni tena.

Bomu la Vita Kuu ya Dunia Yatenguliwa na Wataalamu

Bomu la Vita Kuu ya Dunia Yatenguliwa na Wataalamu

Wataalamu wa kutegua mabomu mjini Frankfurt, Ujerumani siku ya Jumapili walifanikiwa kutegua bomu kubwa ambalo halikuwa limelipuka ambalo liliangushwa wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Bomu hilo la tani 1.4 kutoka Uingereza liligunduliwa katika eneo la ujenzi Jumatano.

Habari hizo zilipokelewa kwa shangwe na watu zaidi ya 65,000 ambao walikuwa wamehamishwa maeneo yao kwa sababu za kiusalama baada ya bomu hilo kuteguliwa.

Hiyo ilikuwa idadi kubwa zaidi ya watu kuhamishwa tangu kutokea kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia nchini Ujerumani, na shughuli hiyo ilihusisha mamia ya maafisa wa serikali.

Maeneo ambayo watu walihamishwa yalikuwa katika mtaa wa Westend, na ni pamoja na hospitali kadha, nyumba za kuwatunza wagonjwa na hata katika Benki Kuu ya Ujerumani.

Inaaminika kwamba kuna mamia ya maelfu ya mabomu ya wakati wa vita ambayo hayakulipuliwa ambayo yametapakaa kote Ujerumani.
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017