Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter
Showing posts with label UJASIRIAMALI. Show all posts
Showing posts with label UJASIRIAMALI. Show all posts

Edward Lowassa Afungukia Kuhamia CCM....Afunguka Haya


Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hana mpango wa kurejea CCM kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Lowassa alisema jana Jumanne  kuwa  amepata taarifa za uvumi unaosambazwa kuwa kuna watu amewatuma kuomba arudi CCM jambo ambalo ni uongo.


"Huu ni uongo wa kutunga, wamekuwa wakitunga vitu vingi juu yangu, mimi sina mpango wa kurejea CCM," alisema Lowassa,ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema  .


Alisema uongo mwingine ambao unasambazwa ni kuwa Serikali imezuia watu kumtembelea nyumbani kwake jambo ambalo anaamini ni maneno yanayotungwa.


"Watu wanazuiwa kuja nyumbani kwangu, eti Serikali imezuia hivyo wanakuwa wanaogopa huu ni uongo Serikali haiwezi kuzuia watu kutembeleana," alisema

Siri 5 kubwa Za Mafanikio Bila Utegemezi

Kila binadamu ameumbwa na kiu ya kufanikiwa katika kila kitu anachofanya. Mafanikio ndio kilele cha mlima mkubwa wa maisha ambao umejengwa kwa misingi na ngazi za mihangaiko na mitihani ambayo unapaswa kuivuka ili upumzike kwenye kilele hicho.
Kwa bahati mbaya, unaposema ‘mafanikio’ wengi hufikiria kuhusu ‘utajiri’. Lakini ukweli ni kuwa kuna tofauti kati ya kuwa tajiri na kufanikiwa kiuchumi. Unaweza kuwa tajiri lakini ukawa bado hujafanikiwa. Kwa kuwa watu wanawaza utajiri kuwa ndio kigezo cha mafanikio hujikuta wakijiingiza kwenye vitendo vya ajabu kwa lengo la kujizolea mali lakini mwisho huwa wanagundua kuwa hawajafanikiwa japo jamii inahisi wamefanikiwa.
Nanachoamini mimi, kufanikiwa kweli ni kutimiza malengo yako kwa ufanisi na kwa wakati, lakini mafanikio hayo yakupe amani moyoni mwako (peace of mind).
Usipitwe na Habari Muhimu, Install App  Yetu


Android ===>  Bofya hapa
Vinginevyo, utafanikiwa kwa mrundikano wa fedha huku ukitengeneza tatizo kubwa zaidi la msongo wa mawazo na ukosefu wa amani ya moyo. Hivyo, mafanikio ya njia ya mkato ni mafanikio feki yanayokuja na matatizo mengi mazito zaidi.
Kwa utangulizi huo mrefu, naamini utanielewa zaidi napokupitisha kwenye hizi ‘siri za wazi’ za mafanikio ya kweli katika maisha.
1. Jiamini
Mafanikio ya kweli yanaanza na wewe. Hivyo, kujiamini ni msingi mzuri utakaokufanya utambue uwezo wako katika kufanya jambo fulani. Amini uwezo wa kufanya jambo hilo uko mikononi mwako. Usijishushe, jipime kwa mengi mazuri unayoweza kufanya, ikatae roho ya kujiona huwezi.
2. Thubutu
Neno hili pia ni msingi wa pili mkuu wa mafanikio. Uoga wa kuthubutu ni kikwazo kikuu kinachowarudisha wengi nyuma na kujikuta hata kuanza safari ya mafanikio hawawezi. Jambo lolote zuri na kubwa huwa gumu kufanya na ni rahisi kuhisi haliwezekani. Usikubali kushindwa bila kujaribu. Thubutu kwa dhati na weka nguvu yako na akili yako yote katika uthubutu huo. Hata hivyo, katika uthubutu huu, unapaswa kupima vizuri ili uchukue ‘calculated risk’ na sio ‘just risk’.
3. Panga na tekeleza kwa vitendo
Kumbuka, ukishindwa kupanga ujue umepanga kushindwa. Kuwa na mipango inayopimika na kutekelezeka kwa kiwango cha juu. Usiwe na mipango tu mikubwa ambayo hata utekelezaji wake hauwezekani. Unapopanga fikiria wapi utapata rasilimali na jinsi ya kutelezeka, lakini pia mpango wako ukupe uwezo wa kuutathmini na kujipima mwisho wa kazi hiyo. Hata hivyo, mipango haitakuwa na maana kama hautaitekeleza kwa ufanisi. Ukishindwa kutekeleza mpango wako, rudi angalia ulipoteleza ili urekebishe na sio kuufuta mpango mzima bila sababu za msingi.

4. Tengeneza mtandao na wasiliana
Mtandao ni kama daraja au miundombinu ya kuyafikia mafanikio. Hakikisha haujifungii kwenye dunia yako peke yako. Hakikisha kila unaekutana naye na kupata nafasi ya kumfahamu kama mtu anayeweza kuwa sehemu ya daraja bora kwa namna moja au nyingine, anakuwa sehemu ya mtandao wako.
Lakini kuwa na mtandao wa watu pekee hautoshi kama hautawasiliana nao. Kuwasiliana na mtandao huo ni kuufanya uwe ‘active’ ili isionekane kama unawatafuta wakati ukiwa na shida tu. Aidha, unapaswa kujipima kwa kuangalia watu wangapi wanakufahamu wewe zaidi ya watu wangapi unaowafahamu. Kwa mfano: wewe unamfahamu Mkurugenzi wa kampuni ‘A’, Jiulize, je, yeye anakufahamu? Kama hakufahamu basi yeye sio sehemu ya mtandao wako.
Lakini pia, angalia mawasiliano yako ya siku, wangapi umeongea nao kuhusu wazo la biashara au kazi.
5. Kuwa mkweli na Mwaminifu
Hii ni siri kubwa zaidi ya zote, japokuwa nimeiweka mwishoni kati ya hizi tano. Usipokuwa mwaminifu na mkweli huku unaona mambo yako yanaenda vizuri unapaswa kushtuka mapema. Wewe ni kama mtu anaevuka ng’ambo ya pili huku akilivunja daraja. Mwisho wa siku utajikuta unaporomoka kabla hujafika unakotakiwa kufika.
Uaminifu utaimarisha mtandao wako kwa hali ya juu zaidi na utatafutwa kwa kuwa wewe utakuwa sehemu ya sababu ya mafanikio ya watu wengine. Kwa mfano, angalia namba ulizonazo kwenye simu yako ya mkononi. Je, ukitaka kumpigia simu dereva taxi majira usiku au hata muda wa kawaida utatumia vigezo gani? Bila shaka uaminifu na ukweli vitatangulia zaidi.
Kuwa mwaminifu na mkweli kwa kila mtu utakayefanya nae kazi, biashara au hata wakati mnafanya mambo ya kawaida ya kijamii kunakupa nafasi ya kuwa chaguo la kwanza kwa watu wanapohitaji huduma, bidhaa au rasilimali ambayo unayo.
Ukifuata kwa uhakika haya matano huku ukimkumbuka Mungu wako kwa kila jambo utafanikiwa kweli na kubaki na amani ya moyo.
Amini katika kile unachoamini na kifanyie utafiti kujiridhisha kabla haujakubali kuyumbishwa kwa tamaa za haraka haraka ili uwe na sababu za kutosha za kukataa au kukubali jambo lolote.

Ufafanuzi Wa Benki Kuu ( BOT ) Kuhusu Kushuka Thamani Fedha Ya Tanzania Dhidi Ya Dola



MBUNGE Goodluck Mlinga Azidi Kutetea Diamond Kuchongewa Sanamu la Heshima Aliyoipa Tanzania



Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Mh #GoodluckMlinga amezidi kutetea hoja yake ya kuwa wasanii waliofanya vizuri na kuiwakilisha nchi nje vizuri, kupewa heshima kama kujengewa sanamu na baadhi ya mitaa na barabara kupewa majina yao.
.
.
Kipindi cha nyuma Mbunge huyo alisimama Bungeni na kusema kwa namna msanii #DiamondPlatnumz anavyoiwakilisha nchi vizuri kimataifa anastahili kujengewa sanamu, na kupendekeza ikibidi sanamu la askari posta Dar es Salaam liondolewe na kuweka hilo la #Diamond.
.
.
#GoodLuckšŸ‘‰“Na sikumtaja Diamond pekee, niliwataja wasanii wengi kama wakina Mr Nice ambao wameiwakilisha Tanzania sana nje lakini mpaka leo hii wamepotea hawana alama, inakuwa hawawezi kuwahamasisha wasanii wengine, lakini tunapoweka alama kila msanii anapofanya vizuri tunahamasisha wengine na ndiyo utaratibu katika nchi za wenzetu,” ameiambia Habari Xtra ya Times Fm
.
.
Na kuongezašŸ‘‰“Kuna mchezaji mmoja wa mpira alitoka Kenya (Victor Wanyama) kuja Tanzania siku ya pili alipewa mtaa, sasa vile vitu ndio tunatakiwa tuvifanye kwa wasanii wetu wanaoibeba nchi. Sasa wewe fikiri mtu katoka nje ambaye anawakilisha nchi nyingine tunampa mtaa, lakini kwetu ni msanii gani alishawahi kuacha alama hata akapewa Barabara, hakuna!!!,” .
.
.
JE UNAMUUNGA MKONO MBUNGE HUYU AU UNAMPINGA??

Mmoja Wa Wakurugenzi Wa Kampuni Ya Acacia Ambaye Ni Mtanzania Wa Hapa Hapa

Image may contain: 1 person, text
Balozi Juma Mwapachu ni mmoja wa Wakurugenzi wa ACACIA, kampuni ya kuchimba na kusafirisha Mchanga wa Dhahabu ambaye imekuwa kwenye matatizo makubwa na Rais Magufuli kwa kutuhumiwa kulidanganya Taifa na kutuibia jumla ya Tsh. Trillioni 108 katika Miaka 17 iliyofanya biashara hapa Tanzania.

Jinsi Shamba la Mbowe Lilivyong’olewa Mitambo, Mwenyewe Afunguka ya Moyoni

Mkuu wa Wilaya ya Hai, aking’oa miundombinu ya shamba la Mbunge wa Hai (CHADEMA), Freeman Mbowe kwa madai lipo ndani ya chanzo cha maji.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbowe amethibitisha shamba lake kuvamiwa na viongozi wa serikali ya Wilaya na kuharibiwa miundombinu ya shamba hilo huku akidai anajua yote hayo yanafanyika kutokana na misimamo yake ya kisiasa na kudai hawawezi kumbadili.
Freeman Mbowe amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii huku akikiri wazi kuwa siku ya Alhamisi ya tarehe 7 mwaka huu walipokea barua kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira -NEMC ambayo ilikuwa inadai kilimo wanachofanya kilikuwa kinaharibu mazingira hivyo hawapaswi kuendelea na kilimo hicho.
“Ni kweli nimepata taarifa ya kuwa mkuu wetu wa wilaya ya Hai, akiambatana na askari wa mgambo akiambatana na watu wengine ambao sijaweza kuwafahamu wakiwemo vile vile waandishi wa habari, walikwenda kwenye mradi wetu wa Kili Vegies ni mradi wa kilimo cha kisasa cha mboga mboga (Green house), tukilima mboga na matunda, tukilima mboga kwa sababu ya ‘local market’ na wakaanza kuharibu miundombinu, ikiwemo kuharibu ‘Green houses’, kukatakata mabomba , kuharibu mimea na uharibifu mwingine mwingi” alisema Mbowe n kuongeza;
“Ni kweli tulipokea barua ya NEMC siku ya Alhamisi tarehe 7, iliandikwa tarehe 7 lakini tuliipata tarehe 8, tulijibu hiyo hoja ya NEMC, kwamba tunaamini wamekosea sheria kwa sababu kilimo chetu hakiharibu mazingira wala shutuma zilizotolewa kwamba ni kwenye chanzo cha maji sio kweli, wanadai kwamba shamba hilo limeanzishwa kwenye chanzo cha mto Weruweru jambo ambalo sio kweli, mto unaoitwa Weruweru unaanzia mlimani kabisa National Park Kilimanjaro”
Mbowe anasema kitendo hicho kilichofanywa na viongozi hao ni kitendo cha kufedhehesha na cha kukatisha tamaa hivyo anasikitishwa sana na kitendo hicho, huku akisema anatambua kuwa yote hayo anayofanyiwa ni kutokana na misimamo yake kisiasa, na misimamo ya chama anachokiongoza.
“Najua haya yanatokea kwa sababu ya misimamo yangu ya kisiasa kwa sababu wa muelekeo wangu wa kisiasa na uthabiti na uimara wa chama ninachokiongoza, sasa mimi siwezi kuwa kondoo, nimesema siku zote, haya mambo ya duniani anayeyalipa ni Mungu,hawatabadilisha mawazo yangu kwa kuharibu mali zangu, wanaweza kuharibu zote hata wakitaka roho yangu waichukue, waichukue tu lakini haitanisababisha nibadili msimamo wangu katika kuamini ninachokisimamia, ninachokipigania katika Taifa” alisisitiza Mbowe
Mbali na hilo kiongozi huyo amedai kuwa hakuna wingi wa mali zake zinaweza kuharibiwa zikamfanya yeye akapige magoti kama watu wengine wanavyofanya, anadai yeye hawezi kupiga magoti bali atasimama kwenye ukweli na haki siku zote.
Hili ni tukio la pili kwa mwaka huu kutokea kwenye shamba hilo, mwezi wa kwanza mwaka huu serikali ilimtaka kiongozi huyo kusimamisha kilimo kwenye shamba hilo ikidai kuwa lipo kwenye chanzo cha maji.

EWURA Yapandisha Bei Za Mafuta Kuanzia Leo Juni 7


Mamalaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Nchini (EWURA) imetangaza bei mpya elekezi za mafuta zitakazoanza kutumika maeneo yote nchini kuanzia leo Juni 7, 2017.
Katika bei hizo mpya zilizotolewa jana na Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa EWURA, Titus Kaguo alisema kuwa kunaongezeko la bei katika mafuta ya petroli na dizeli huku mafuta ya taa yakishuka bei.
Kaguo alisema kuwa, ongezeko hilo la bei linatokana na sababu ya mabadiliko ya bei ya mafuta katika soko la dunia sambamba na kuimarika kwa thamani ya dola ya Marekani dhidi ya shilingi ya Tanzania.
Kwa upande wa mafuta ya dizeli yameongezeka Tsh 43 kwa lita huku mafuta ya petroli yakiongezeka Tsh 25 katika kila lita moja.
Aidha, afisa huyo alisema kuwa, bei hizo mpya haziwahusu wateja kutoka mkoa wa Tanga ambao wao wataendelea kutumia bei za mwezi uliopita kutokana na mkoa huo kuwa na bandari inayotumika kushushia na miundombinu ya kuhifadhi mafuta kiasi cha kuwa na akiba kubwa ya mafuta yaliyoingia nchini mwezi uliopita.

Wabunge Walilia Bei Ya Bia Na Soda Zisipande Bei Kwenye Bajeti Kuu Ya Serikali Itakayosomwa Kesho


WAKATI Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 ikitarajiwa kuwasilishwa bungeni kesho, baadhi ya wabunge wametoa maoni yao wakisisitiza haja ya sekta ya maji na sekta ndogo ya umeme kupewa fedha nyingi.

Aidha, Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) amependekeza kupunguzwa kwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), na kuondolewa kwa kodi hiyo katika malighafi za kilimo zinazozalishwa nchini, na kusiwepo upandishaji wa ushuru wa vinywaji baridi na bia.

Wabunge wametoa maoni hayo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ikiwa katika mashauriano na serikali kwa siku ya tatu kuhusu hoja zilizojitokeza wakati wa kujadili bajeti za kisekta bungeni.

Kamati hiyo ya Bajeti chini ya Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia (CCM), imekuwa katika majadiliano hayo na serikali ili kuboresha maeneo ambayo wabunge walitaka yafanyiwe kazi kabla ya Bajeti ya Serikali kusomwa kesho.

Kesho asubuhi, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango atawasilisha bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi nchini kabla ya jioni kuwasilisha Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18.

Akizungumza na gazeti hili, Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi (CCM) alisema suala la maji ni muhimu, hivyo serikali haina budi kuongeza fedha badala ya kupunguza, kama ilivyofanya bajeti ya wizara hiyo kutoka zaidi ya Sh bilioni 900 hadi zaidi ya Sh bilioni 600.

Aidha, Chumi alilitaja eneo jingine ambalo serikali inatakiwa kulitazama ni kuchangia katika ujenzi wa maboma ya zahanati, vituo vya afya na madarasa. “Serikali ilihamasisha wananchi wajenge maboma hayo na wao watamalizia, kazi hiyo imefanyika lakini serikali haijaweka fedha katika maeneo mengi, hii inaweza kukatisha tamaa wananchi siku nyingine watakapoombwa kuchangia,” alieleza Chumi.

Lakini, pia alitaka serikali itenge fedha kwa ajili ya Mfuko wa Mazingira hasa baada ya hali ya sasa ya mabadiliko ya tabianchi, ambayo yameathiri maeneo mengi nchini. “Fedha hizi zitasaidia katika kutoa ruzuku kwa maeneo yenye kufanya vizuri katika uhifdhi wa mazingira na hivyo kuchochea watu wengine kupanda miti kwa wingi na hivyo kurejesha hali ya kijani,” aliongeza Chumi.

Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel (CCM), alitaka kuwapo kwa msamaha wa kodi kwa watu wenye ulemavu hasa katika vifaa vyao. Mollel alisema mbali ya msamaha huo, pia serikali kuimarisha Mfuko wa Watu wenye Ulemavu hasa baada ya kuunda Baraza la Watu wenye Ulemavu nchini.

Aidha, Mollel alipendekeza kwa serikali kutenga asilimia mbili kutoka katika asilimia 10 iliyotengwa katika halmashauri kwa ajili ya mifuko ya vijana na wanawake, iende kusaidia watu wenye ulemavu.

Mbali ya hayo, alitaka wizara nyeti ikiwamo ya Nishati na Madini kuongezewa fedha hasa wakati huu, ambao amesema Rais John Magufuli anapambana kuhakikisha rasilimali za Taifa yakiwamo madini yanawanufaisha Watanzania badala ya wachache kunufaika.

Kwa upande wake, Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM), alisema maji na nishati ya umeme ni muhimu na akapendekeza kuundwa kwa Mfuko wa Maji Vijijini. Ndassa alisema kama ilivyo kwa umeme ambako kuna Wakala wa Umeme Vijijini (REA), ni muhimu kuwa na Mfuko wa Maji Vijijini ambao utawezeshwa na tozo ya mafuta kupandishwa kutoka Sh 50 hadi 100.

“Fedha hizi zitakazopatikana ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 360 ziwekwe zisiguswe kwa kazi nyingine, zitumike kwa ajili ya Mfuko wa Maji Vijijini, maji ni muhimu pengine kuliko umeme,” alieleza Ndassa.

Alishauri serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri ya ukusanyaji wa kodi na kuwa na vyanzo vyake vya kuaminika vya mapato ili Taifa lijitegemee lenyewe. Mbunge wa Bukombe, Dotto Biteko (CCM) pia alikazia suala la maji, umeme, kilimo na ardhi, akisisitiza fedha nyingi zielekezwe katika miradi ya maji nchini kwani maji ni muhimu kwa matumizi ya binadamu na kilimo.

Biteko alisema kuwapo kwa maji ya kutosha yatawezesha kufanyika kwa kilimo cha umwagiliaji, hivyo kuzalisha malighafi nyingi kwa ajili ya Tanzania ya viwanda. Katika kilimo alipongeza serikali kwa kuondoa tozo zilizokuwa na kero kwa wananchi, kama ilivyofanya katika ardhi, hivyo kuwataka wananchi watumie fursa hiyo kujiongezea uzalishaji wao na kujiletea maendeleo.

Kuhusu umeme, alisema serikali imeahidi kuvipatia umeme vijiji vyote nchini mwaka huu, hivyo akataka Bajeti ya Serikali itenge fedha kuharakisha azma hiyo. Hoja ya umeme na maji pia ilitolewa na Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), akisema maji ni kila kitu, ni vyema kuongeza fedha katika sekta hiyo na umeme.

Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (CCM) pia alizungumzia suala la maji, akisema maenep mengi nchi yana tatizo kubwa la maji, hivyo akashauri fedha za bajeti ziongezwe ili kuhakikisha miradi mingi ya maji inaanzishwa au inakamilishwa kwa haraka.

Nkamia pia alitoa pendekezo la kuanzishwa kwa dirisha maalumu la serikali katika Bandari ya Dar es Salaam ili kurahisisha utoaji wa vifaa vya serikali bandarini. Kwa upande wake, Bashe alipendekeza katika bajeti ya kesho serikali ipunguze VAT hadi kufikia asilimia 16 kutoka 18 ya sasa na iondoe kodi hiyo katika bidhaa zinazoagizwa kutoka nje.

Bashe pia alitaka VAT iondolewe katika malighafi za mazao yanayozalishwa nchini, na kusiwapo na ushuru wa bidhaa katika pembejeo za kilimo. “Kwa kufanya hivyo, uzalishaji utaongezeka, serikali itapata kodi nyingi (kodi ya makampuni, VAT na kodi ya ushuru wa forodha).

Hii pia itaongeza ajira na hivyo kusaidia kupata kodi ya PAYE,” alieleza Bashe. Akijibu swali bungeni juzi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alieleza kuwa serikali itawasilishwa katika bajeti yake mapendekezo ya kufuta misamaha ya kodi isiyo na tija.

Dk Kijaji alisema mpango wa serikali ni kuhakikisha misamaha ya kodi inashuka mwaka hadi mwaka na katika mwaka ujao wa fedha, serikali italeta mapendekezo ya marekebisho ndani ya bajeti itakayosomwa kesho.

Machi 29, mwaka huu, Dk Mpango alisoma mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na kiwango cha ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa 2017/18. Kwa mujibu wa Dk Mpango, serikali katika bajeti hiyo inatarajia kuwa na ukomo wa Sh trilioni 31.6.

Katika fedha hizo, za maendeleo zimeongezeka kutoka Sh trilioni 11.8 katika mwaka 2016/17 hadi Sh trilioni 11.9 katika mwaka wa bajeti 2017/18. Ongezeko hilo ni kiasi sawa na asilimia 38 katika bajeti hiyo tarajiwa.

Credit -Habari Leo

Vyakula Vya Kuepuka Kuanza Kula Wakati Wa Kufuturu


Kufuturu ni jambo linalofanywa kila siku na waumini wa dini ya kiislamu wanaofunga katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Lakini kiuhalisia kufuturu au kula chakula baada ya mfungo wa siku nzima, ni jambo linaloweza kufanywa na yeyote, na si lazima iwe kipindi cha mfungo. Baadhi, kama wakristo hufunga wakati wowote mtu anapotaka kwa ajili ya maombi yake.
Lakini wakati wa kufuturu, si vyakula vyote unashauriwa kuanza kuvila wakati tumboni mwako hamn kitu. Kuna baadhi ya vyakula hutakiwi kuvila kwanza, na hapa chini tutaelezea baadhi.
Juisi ya matunda yenye kiwango kingi cha sukari
Juisi zenye kiwango kikubwa cha sukari haushauri kuzitumia mara tu unapofuturu kwani inaongeza kiwango kikubwa cha sukari ndani ya mwili wako ambayo kwa wakati huo hauitumii.
Lakini pia ukianza kula chakula chenye sukari nyingi mbali na kuongeza kiasi cha sukari mwili kutakufanya ujisikie kushiba kwa muda mfupi, ambapo kama kesho yake utafunga tena njaa huenda ikakusumbua.
Kawaha au Chai
Najua hii ndio hutumiwa na watu walio wengi sana ambao husema wanapasha tumbo joto baada ya mfungo ndipo waweze kula kitu kingine. Kunywa caffeine ambayo hupatikana kwenye kahawa au chai wakati tumbo lako halina kitu huweza kukuletea matatizo ya tumbo yanayoweza kukupelekea kutapika
Amira
Ulaji wa baadhi ya vyakula venye amira mfano donati au ‘pastry’ za nyama huwa na amira ambayo huweza kukusababishia kuvimbiwa au kulifanya tumbo lako lisiwe sawa. Mbali na tumbo kutokuwa sawa pia inaweza kukupelekea kutoa ushuzi mara kwa mara.

Picha Za Awali Kutoka Kwenye Maandalizi Kumuaga Ndesamburo, Moshi


Baada ya kuripotiwa kifo cha Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro Philemon Ndesamburo May 31, 2017…zilizonifikia leo June 5, 2017 ni shughuli za kumuaga mwanasiasa huyo mkongwe.
Nimezipata picha 5 kutoka Uwanja wa Majengo ambako shughuli za kuuaga mwili wa Ndesamburo zitafanyika leo June 5, 2017.

Hii Ndo Kauli Ya Mo Dewji Baada Ya Kukutana Na Bill Gates

Tajiri kijana namba moja kwa Afrika, Mohammed Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya METL amefanikiwa kukutana na tajiri namba moja duniani, Bill Gates na kufanikisha moja ya ndoto zake ambapo wameweza kubadilishana mawazo juu ya biashara zao.
Dewji na Bill ambaye ni Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, wamekutana wiki hii katika mkutano mkuu wa Giving Pledge. kupitia mitandao ya kijamii, Dewji ameonekana kufurahi zaidi baada ya kukutana na tajiri huyo namba moja duniani.
“Ninafarijika na kuhamasika kujifunza kutoka kwa #BillGates hasa leo kwenye mkutano mkuu wa #GivingPledge, pia kupata maarifa juu ya namna ya kuboresha maisha ya wahitaji duniani,” ameandika katika mtandao huo.

Maneno Ya Idriss Sultan Kwa Mrembo Jokate Baada Ya Kutajwa Na Forbes

Ndani ya miaka 5 she has done so much more than any celebrity in Tanzania kwenye jamii.

Naomba nihamishie upepo kwake kwa shukrani zote kwa yote aliyoyafanya kuinyanyua jamii ya watanzania na naomba msamaha kwa niaba ya watanzania kwani tulikua busy tunaangalia nani anatoka na nani na nani kagombana na nani na nani kaposti uchi leo, tukasahau kua umebadilisha maisha ya vijana zaidi ya laki 5 ndani ya miaka miwili tu.

Ingekua muamuzi ni mimi ungekua Forbes because ni celebrity pekee uliyesimamisha brand product yako kwa jina lako and yes African boy ya Jux inakuja pia. Uliyoyafanya kwenye jamii yako bila kulazimishwa ni zaidi ya baadhi viongozi tuliowachagua kufanya kazi hizo tunazowalipa kufanya.

If am allowed may I please say you are "THE FLOWER  OF TANZANIA" if you ask me why its because you are beautiful and you make us smell good werevaa you go.

Idriss Sultan


Mrembo Jokate Mwegelo Afunguka Haya Baada Ya Kutajwa Na Jarida La Forbes

Jokate Mwegelo ameonyeshwa kufurahishwa baada ya kuchaguliwa na jarida la Forbes Africa la kuwa miongoni mwa vijana walio na umri chini ya miaka 30 wenye mafanikio katika sekta mbalimbali kwa mwaka 2017.

Mrembo huyo ameonyesha furaha hiyo katika mtandao wa Instagram, wakati alipoweka picha ya cover la jarida hilo na kuandika, “Looks whose on the cover of Forbes Africa with some other amazing young Africans doing amazing things to create wealth and transform our economies? God is so amazing.

“Never underestimate your own strength. You were born for a purpose and are blessed with an ability to achieve it. Mpaka kieleweke , ameongeza katika picha nyingine aliyoiweka katika mtandao huo.

Naye Lavie Makeup ni mrembo mwingine kutoka Tanzania aliyetajwa na jarida hilo pamoja na Jokate.

Angalia Mishono Mipya Ya Kitenge !!! Iko Bomba Sana Inawahusu Wote, Badilika Kuwa Mpya











  
   
 
 
 
  
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017