Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter
Showing posts with label KILIMO. Show all posts
Showing posts with label KILIMO. Show all posts

Chama Cha Wakulima Tanzania (TASO) Wamwangukia Rais Magufuli Baada Ya Kupokwa Sherehe Za Nane Nane

Sherehe za wafanyakazi (Mei mosi) zinasimamiwa na vyama vya wafanyakazi zikiratibiwa na TUCTA.
Sherehe za wafanyabiashara sabasaba zinaratibiwa na TANTRED NA TCCIA.

Sherehe za wakulima (wakulima, wafugaji na  wavuvi) zinaratibiwa na TASO

Mh.Raisi/ waziri mkuu upo uvumi ulionea na uliotangazwa na katibu mkuu wizara ya kilimo,ufugaji na ushirika kwamba chama cha TASO kimefutwa na  maadhimisho ya sherehe ya wakulima (NANENANE) ziratibiwe na watumishi (sekretarieti za mikoa).Kwa nini Mh.Raisi/waziri mkuu kama chama cha TASO kimefutwa kwa nini sherehe za nanenane zisifutwe?
kuliko kusimamiwa na wasiohusika.

Sisi wanachama wa TASO tumesikitishwa sana na jambo hili kwani hatuelewi chama chetu kimefutwa kwa taratibu zipi,mbona hatujashirikishwa kupitia vikao vyetu kwa mujibu wa KATIBA ?

Pamoja nakuwepo au kutokuwepo jambo hili hivi vyama vya wafanyakazi vikifutwa TASO Au TANTRED wanaweza kuratibu nakusimamia sherehe za wafanyakazi?.Kinachotusikitisha zaidi hao watumishi wa UMMA walioteuliwa kuratibu nakusimamia wana WELEDI kiasi gani na shughuli za wakulima?

Mh Raisi/waziri mkuu sisi wakulima ambao ndio kundi kubwa nchini tunanyanyasika sana na hawa watumishi wa UMMA ambao hujiona kwamba wana WELEDI mkubwa kuliko sisi wakulima  kama ambavyo msajili wa vyama hiari (mambo ya ndani)alivyoamua kwa makusudi kutofuata taratibu nakufuta chama chetu bila kutushirikisha kwakua sisi ni mambumbumbu kama wanavyotuita kitendo ambacho tunakilaumu sana .

Mh .Rais/Waziri mkuu hawa sekretarieti zamikoa wametupangia viingilio vikubwa kuingia kwenye viwanja ambavyo ni mali yetu TASO mfano  kiingilio uwanjani mtu mzima Tshs 2000/ na  mtoto 1000/ hivi Mh tunaenda kufanya biashara au kujifunza mbona wenzetu wafanya kazi wanapopeleka matatizo yao kwako huingia bure?
uwanjani?

Jambo jingine ni kwamba sisi TASO tulikua tunatoa kiingilio kidogo kupata pesa zakuendesha chama je hizi sekretarieti za mikoa hizo fedha watakazokusanya wanapeleka wapi?
Jingine Mh .hawa watumishi walioteuliwa kuratibu shughuli za NANENANE wametoka kwenye vituo vya kazi takribani mwezi kuanzia tarehe 01/07/-9/8/2012 je wananchi wanapata wapi huduma zao na kauli mbiu ya awamu ya TANO ni HAPA KAZI TU,sasa kusimamia sherehe za nanenane ni kazi inayowalipa mishahara na huku wanalipwa posho kila siku je nisahihi.

Tunafikisha kilio chetu kwako juu ya swala hili kwani wewe ndio Mkombozi Wetu wakulima tumechoka kunyanyasika hasa katika awamu ya Utawala wako.

Soma Hii: Tajirika Na Kilimo Cha Nyoka, Kina Pesa Zaidi Ya Dhahabu


Kilimo cha nyoka ni moja ya kilimo yenye faida sana ,mmoja anaweza akaanzisha kilimo hichi ukizingatia thamani ya “snake venom” ipo juu sana.Sumu ya nyoka inatumika kwa wingi kwenye viwanda vya famasia na viwanda vya vipodozi hivyo thamani ya “snake venom ” ipo juu sana kutokana na uhitaji wake. Gram moja ya “snake venom ” kwa soko la kimataifa inauzwa $1880 ,na kwenye soko la Afrika kusini inauzwa kwa makadirio ya Rand 25,000

Kama unafikiria kuanzisha shamba lako la nyoka ,yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kupata faida ya kutosha kutokana na venom wanayozalisha Nyoka

1.Zingatia hali ya joto na hewa .
Nyoka wanahitaji joto ya kiwango cha 24-29 degrees Celsius nyakati ya siku na 21-24 nyakati za usiku,
2.Mabanda na nyumba za nyoka zinahitaji kusafishwa mara kwa Mara
Hali hiyo itasaidia kukuza uzalishaji wa nyoka kwa wingi.Nyoka wanahitaji kuwekwa mahali salama kuzuia matatizo yeyote ile ya kiafya kuwapata.
3.Nyoka kwa kawaida hula panya 3-4 na hulishwa kwa wiki 3-4 . Nyoka hula panya walio hai lakini wanaweza kula waliokufa pia ,Nyoka hupenda kucheza na panya mwanzo kabla ya kuwala hivyo ni vema kuwapatia walio hai.
Faida 3 za ufugaji wa nyoka

1.Uzalishaji wa venom ambayo ukiuza unapata kiasi kikubwa cha pesa.
2.Hupunguza na kutokomeza wadudu waharibifu kama panya nk.Nyoka chakula chao kikuu ni panya hivyo husaidia kutusafishia shamba au nyumba kwa kuwamaliza wadudu hawa.
Dawa ya kuua sumu ya nyoka itengenezwayo kutoka kwa sumu ya nyoka, yaani anti-venom, ndiyo tiba bora pekee ya kuumwa na nyoka. Mwisho nawashauri ndugu zangu sio kila tukiwaona nyoka tunawaua ,nyoka ni rafiki zetu na sio maadui. Tuwatumie ipasavyo watatusaidia sana.

Muongozo Wa Jinsi Ya Kulima Kilimo Bora Cha Papai


Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa na faida mbali na afya, katika kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Pia linawezakuwa chanzo kikubwa cha pesa za kigeni kwa kuuza nje ya nchi.

Uzalishaji wa papai nchini Tanzania ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mahitaji ya watumiaji, hivyo inahitajika nguvu zaidi katika uzalishaji wa zao hili.
KUHUSU MPAPAI
Kijinsia mpapai umegawanyika katika aina tatu
i) Mpapai wenye maua kiume tu ii) Mpapai wenye maua kike tu iii) Mpapai wenye maua ya jinsia zote (Hermaphrodite papaya)





Katika uzalishaji kila aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda. Mpapai wenye maua ya jinsia zote hauhitaji mpapai wenye maua ya kiume maana uweza kujirutubisha wenyewe.

Kutokana na jinsia ya maua mpapai huweza kutengeneza matunda yenye maumbo tofauti. Matunda yanayotengenezwa kutoka katika mpapai wenye maua ya kike tu huwa na umbo la mviringo zaidi au yenye umbo la yai na matunda yanayotokana na mpapai wenye maua ya jinsia zote mbili huwa na umbo la refu zaidi au umbo la pear.
UZALISHAJI WA ZAO LA PAPAI
Miche ya mpapai
Katika uzalishaji wa miche ya mpapai kuna aina mbili za mbegu ambazo huweza kutumika: -
1. Mbegu za Kawaida (Local seeds)
Hizi ni mbegu ambazo huweza kukusanywa toka katika mipapai ya kienyeji. Aina hii ya mbegu ni vigumu kujua kati ya mbegu ni ipi dume, jike ama yenye jinsia zote. Hivyo itakulazimu kung'oa baadhi ya mipapai dume pindi itakapo weka maua hivyo kuacha majike na yenye jinsia zote mbili. Mapapi yenye maua ya kiume uachwa kwa uwiano wa 1:50 ya mipapai yenye maua ya kike.
2. Mbegu chotara (Hybrid seeds)
Aina hii ya mbegu ni nzuri kwa sababu mbegu zote huwa ni ya mipapai nyenye maua ya kike na ya kiume pamaoja (Hermaphrodite papaya)na pia hukua haraka na kutengeza miti mifupi yenye uzao mkubwa ukilinganisha na ile ya kienyeji. Mfano. Red royolen F1, MALAIKA F1 n.k.
Upandaji
Panda mbegu moja tu kwa kila kiriba chenye udongo uliochanganywa vizuri na kujazwa robo tatu. Kisha weka viriba vyako venye mbegu chini ya kivuri kisha mwagilia maji. Baada ya kumwagilia unaweza pulizia kiasi kidogo cha kiuwatilifu (fungicide & Insecticide) kwenye udongo wako ili kuzuia wadudu na fungasi wasiathili mmea wako.
Mbegu ya papai uweza chukua siku 8 hadi 15 kuchomoza toka kwenye udongo. Hivyo hakikisha unamwagilia maji kila siku kwa kiasi. Usimwagilie maji mengi sana. Mpapai huweza kuamishwa toka kwenye kitalu baada ya wiki sita hadi nane.
Kitalu cha mipapai
BAADHI YA SABABU MUHIMU ZINAWEZA ATHILI UKUAJI WA MIPAPAI
Mpapai upendelea zaidi udongo unaopitisha maji na mzuko wa hewa kirahisi na wenye makadilio ya Ph 6.5.
Inapowezekana zuia kupanda mimea yako kwenye udongo wa mfinyanzi na wenye magadi.
Kiaisi cha maji kilichopo kwenye udongo huweza kuonyesha ukubwa wa matunda. Eneo lenye udongo wenye unyevunyevu mwingi huweza tengeneza matunda makubwa na yalioja maji maji na eneo lenye unyevunyeku kidogo hutengeneza matunda madogo na magumu.
Mpapai hawezi kuvumilia upepo mkali, maji yaliotwama pamoja na ukame.
UANDAAJI WA SHAMBA
Njia ya kuandaa shamba itategemea na eneo (topography), aina ya udongo, vifaa vinavyotumika kuhudumia shamba.
Nafasi
Nafasi kati ya mmea na mmea ni mita 2 hadi 2.5 na kati ya mstari na mstari ni mita 2.5 hadi mita 3.
Andaa mashimo yenye upana na urefu wa sentimita 60. Tenga udongo wa chini na wa juu. Kisha changanya udongo wa juu na mbolea ya samadi. Katika kurushisha kwenye shimo tanguliza udongo ulochanganywa na mbolea ya samadi chini na juu malizia na udongo uloutoa chini wakati wa kuchimba shimo.
NB: Kiasi cha mmea huwa kati ya 1000 hadi 2000 kwa hekari ( 400 hadi 800 kwa ekari)
Kupanda mimea shambani
Baada ya hizo wiki sita hadi nane hamishia mimea yako shambani. Kazi ya uhamishaji wa mimea ufanyika wakati wa asubuhi sana, jioni ama kukiwa na mawingu ili kuzuia madhara ya jua kwa mimea.
shamba la mipapai
Uwekaji wa mbolea.
Zuia matumizi ya mbolea zenye chlorine maana mipapai uathiliwa na chlorine. Wiki moja baada ya kuhamisha miche yako weka mbole gramu 28 kwa kila mche. Tumia mbolea yenye phospate kwa kaisi kikubwa. Mfano; - 12:24:12. (NPK)
Baada ya hapo kila baada ya wiki mbili weka mbolea yenye Nitroni kwa kiasi kikubwa kiasi cha gramu 56 kwa mmea. Mfano. 20:10:10 (NPK)
Potassium inahitajika kwa maua na kuweka matunda hivyo tumia mbolea yenye potassium kiasi kikubwa mara baada ya kuona mmea wako umeanza kuweka maua, kiasi cha gramu 114 cha mbolea huitajika, fanya hivyo kila baada ya mwezi. Mfano. 12:12:17 + 2 (NPK) . Weka mbolea ya majani yenye virutubisho vidogo vidogo ikiwemo boron kila mweze. Boron ni mbolea ya muhimu katika kupata matunda mazuri.
Umwagiliaji
Maji ni sehemu ya muhimu sana katika maisha ya mmea kwa kipindi chote. Maji niya muhimu sana katika kuweka maua, matunda na ukuaji wa matunda. Katika ukuaji wa matunda hakikisha unaweka lita 23 kwa kila mmea kwa wiki.
Magugu
Hakikisha unazuia magugu kipindi cha mwanzo ili kuzuia ushindani kati ya mimea na magugu kwa virutubisho na maji. Na pia kuzuia magugu kubeba vimelea na wadudu wanaoweza kuathili mazao yako.
HATUA ZA UKUAJI WA MPAPAI
Kitalu - Wiki 1 - 6
Hatua ya ukuwaji wa haraka baada ya kuamishiwa shamba - wiki 7 -16
Maua na kuweka matunda - wiki 17 - 21
Kukua kwa matunda - 22 - 26
Mavuno ya kwanza - Wiki 37 nakuendelea .................

Jifunze Kuzalisha Malisho Ya Wanyama Kwa Njia Ya Kitaalamu "Hydroponic Fodder"



Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

HYDROPONIC ni sayansi/sanaa ya kuotesha mazao bora yenye tija kwa muda mfupi zaidi bila kutumia udongo kabisa, kwa kutumia maji na virutubisho (Hydroponic Nutrients).

Hydroponic fodder Ni nzuri zaidi kwa sasa maana Ni nafuu kulinganisha na vyakula vingine vya mifugo.

Hydroponic fodder Ni uoteshaji wa mbegu pasipo kutumia udongo kwa muda wa siku 5- 7 tu kilo moja ya mbegu za ngano au mtama au shayiri au Mshindi zinaoteshwa na kumwagiliwa virutubisho maalum (HYDROPONIC NUTRIENTS) na kuongezeka kutoka kilo moja hadi kilo 10 za CHAKULA cha kuku.

 Kwakuwa kuku mmoja hula gram kati ya 100-120gm hivyo kilo moja ya mbegu ikitoa kilo kumi za fodder zinatosha kulisha kuku wakubwa 100 kwa siku Hydroponic fodder Ni CHAKULA cha Mifugo wa aina zote chenye faida nyingi sana.

FAIDA ZA CHAKULA CHA HUDROPONIC FODDER KWA MIFUGO

  1. Ni nafuu sana kulinganisha na garama za CHAKULA cha madukani au viwandani
  2. kina virutubisho na vitamini mara 3 zaidi ya CHAKULA cha kawaida cha Mifugo
  3. Hupunguza magonjwa ya mfumo wa hewa kama vile mafua kwa mfugaji na Mifugo kwani hakina vumbi kabisa.
  4. kina protein na Energy/nishati nyingi zaidi mara 3 ya inayopatikana kwenye vyakula vya kawaida vya Mifugo kama kuku.
  5. mifugo hukua haraka sana kutokana na wingi wa protein ambayo hufanya Kazi ya kujenga mwili na kukua
  6. CHAKULA hiki Ni laini sana na kitam kwa kuku na Mifugo yote (palatable)
  7. mmeng'enyo wa chakula hiki huongezeka kutoka 30% kwa CHAKULA cha kawaida hadi 95% kwa CHAKULA cha hydroponiki hivyo chakula kingi kutumiwa na mwili wa mifugo na kupunguza kinyesi na usumbufu wa usafisaji banda
  8. kinyesi hupungua na kuwa kati ya 5%-10% tu kwani CHAKULA kingi humeng'enywa na kutumiwa na mwili wa Mifugo
  9. mazao kama mayai au maziwa huongezeka kwa 40% kulinganisha na chakula cha kawaida.
  10. kiini cha yai la kuku anayelishwa hydroponic fodder huwa cha njano sana hata kama Ni kuku wa kisasa
  11. Hupunguza garama za ufugaji kwenye manunuzi ya chakula kwa 50-75% hivyo kuongeza faida.                      


 UZALISHAJI WA MALISHO KWA TEKNOLOJIA YA HYDROPONIC

HATUA KWA HATUA KATIKA KUZALISHA HYDROPONIC
Kwa kufata hata hizi unaweza kuzalisha malisho yako mwenyewe nyumbani.

  1. Chagua mbegu ambazo hazijaanza kuchipua, na hazina kemikali ama dawa ya aina yoyote.
  2. Loweka mbegu katika mchanganyiko wa maji na Chlorine kwa masaa mawili kuepusha kuvu/uvundo ama vimelea vya magonjwa kumea na kukua.
  3. Zitoe mbegu kwenye maji, zioshe kasha ziloweke kwenye maji safi kwa masaa 24 kuwezesha mbegu kufyonza maji vema.
  4. Katika kupanda mbegu, pima kilo mbili za mbegu kwa kila trei yenye urefu wa Cm 80 kwa upana wa Cm 40.
  5. Sambaza mbegu kwenye trei kwa usawa, (zisizidi Cm 3 kimo) ili kuwe na nafasi ya kutosha kwa kila mbegu kuchipua (kuota).
  6. Hakikisha trei zina matundu kwenye kitako (chini) ambayo yamesambaa kwa usawa kuwezesha maji ya ziada kutoka.
  7. Hamishia trei kwenye chanja ulizotengeneza. Mbegu zitaanza kuota katika hatua hii. Fanya hii ni siku ya kwanza.
  8. Nyunyizia maji (kwa pampu) toka siku ya kwanza hadi ya sita, kwa mara nne katika kila masaa 24.


ZINGATIA.
Mbegu zenye dawa au sumu yoyote ni hatari kwa wanyama. zinaweza kuwadhoofisha ama kuwaua. hakikisha hautumii mbegu zenye dawa.

Jinsi ya kulisha
Kuku: kwa kuku 100 wanaotaga (layer) wape kilo 8  za hydroponics na waongezee kilo 4 za chakula cha ‘layer’ (layer mash) kwa siku.

Nguruwe: katika unenepeshaji wape kilo 2 za hydroponics na 1.5 za chakula kikavu (nafaka) kwa nguruwe mmoja kwa siku.

Ngómbe, mbuzi: wanaweza kutegemea majani haya tu na kuwa na uzalishaji mzuri bila nyongeza ya mchanganyiko wa nafaka. Kama uzalishaji wa maziwa ni mkubwa sana (zaidi ya lita 12 kwa siku) ni vema kuwaongezea nafaka.

Sungura: wanaweza kutegemea majani haya tu lakini ni vema kuwapa nyongeza ya mchanganyiko wa nafaka (angalau kwa uwiano wa 50%).                      

 UZALISHAJI WA MALISHO KWA TEKNOLOJIA YA HYDROPONIC

Hydroponic ni nini?
Ni mbinu ya kukuza mimea kwa kutumia mchanganyiko wa virutubisho vya madini katika maji bila kutumia udongo. Mchakato huu huchukua siku 6 hadi nane kukamilika.
Kilo moja ya mbegu huzalisha wastani wa kilo 6 hadi kumi za majani na mizizi.
Faida za Teknolojia hii.

i. Malisho huzalishwa ndani ya muda mfupi katika eneo dogo.
ii. Chakula hiki hulika chote kwa mifugo. Wanakula najani yote pamoja na mizizi. Hakuna upotevu wa chakula.
iii. Mahitaji ya maji ni madogo na maji yanaweza kutumika tena na tena.
iv. Gharama za uendeshaji wake ni mdogo; hakuna kuandaa ardhi, palizi na gharama za uvunaji.
v. Uwezekano mdogo sana wa wadudu ama magonjwa kushambulia.

Faida katika ulishaji
i. Chakula hiki ni laini hivyo mmengényo wake katika mifugo ni mkubwa hivyo sehemu kubwa hutumika katika mwili wa mifugo na uzalishaji.

ii. Mazao ya mifugo uboreka zaidi na kuendana na mahtaji ya soko. Mfano:

  • Mayai ya kuku huwa na kiini cha njano zaidi wanapokula majani.
  • Maziwa huwa na uwiano mzuri wa Omega 3 na Omega 6 amino acid ambazo hujenga afya imara ya mlaji.


iii. Hupunguza gharama za chakula na hivyo kuongeza faida.
iv. Virutubisho vingi hasa vitamin ambazo huchangia afya ya mifugo kuimalika.
v. Kinapolishwa kwa mchanganyiko na vyakula vingine kwa uwiano tutakaoutoa hapo mbele, uzalishaji na ukuaji wa mifugo huwa mzuri zaidi.

Vifaa mihimu
  • Sehemu/chumba cha kukuzia.
  • Nguzo na fito za kutengeneza chanja kwa ajili ya kupanga trei.
  • Trei za plastiki/aluminiamu.
  • Dawa yenye Chlorine (kama Waterguard) ama JIK kuua vijidudu katika maji na mbegu.
  • Virutubisho (nutrients): wengine hutumia buster za mazao (hakikisha haina madhara kwa mifugo).
  • Pump (sprayer) kunyunyiza maji.
  • Mbegu.
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017