Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter
Showing posts with label WASANII. Show all posts
Showing posts with label WASANII. Show all posts

Wastara Amfungukia Mange Kimambi na Wanaomtuhumu Kuwa Tapeli


Msanii wa filamu wa bongo Wastara Juma ambaye hivi karibuni amepewa mchango wa milioni 15 na familia ya Rais Magufuli, amewajibu watu wanaomtuhumu kuwa tapeli kwani hana ugonjwa unaomsumbua.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Wastara amesema kabla ya kuomba michango alijitahidi sana kujitafutia mwenyewe hiyo pesa kwani hakutaka pesa ya mtu mwengine ije imsaidie, kwani alijiona anakuwa mzigo kwa jamii.

Kufuatia kauli hiyo Wastara amesema alishajaribu kujiingiza kwenye biashara ambazo amedai hazina faida, mpaka kufikia hatua ya kuanza kuuza vitu vya ndani, jambo ambalo msanii mwenzake Steve Nyerere alimkataza, na kumshauri aweke wazi matatizo yake iili watu wamsaidie.

Akiendelea kulalamikia kitendo cha watu kumdhihaki, amesema asilimia kubwa ya watu wanaomtuhumu hawajahi hata kwenda kumuona wakiwemo wasanii wenzake, ambao waliamua kumtenga baada ya yeye kuolewa na aliyekuwa Mbunge wa CCM Sadifa.

Baadhi ya wasanii wamesikika wakiongea chini chini kuwa Wastara anajidai kuumwa ili apate hela , pia Mwanadada Mange Kimambi amemlipua Wastara kupitia ukurasa wake wa Instagram 

Aunt, Iyobo Na Tunda Kimenuka, Watupiana Matusi Si Ya Nchi Hii

VIDEO vixen asiyeishiwa stori kwenye mitandao ya kijamii, Tunda ameingia kwenye bifu la aina yake na Aunty Ezekiel na mpenzi wake, Mose iyobo baada ya mdada huyo kusemekana anadaiwa mkwanja ambao alitakiwa kulipia pombe alizokunywa.

Bifu hilo limetikisa jioni ya leo baada ya post kuanza kusambaa wakirushiana maneno makali (mengine tumeyafisha kulingana na maadili ya Kitanzania) jambo ambalo limezua mijadala miongoni mwa mashabiki wao.

Inavyoonekana kutokana, Tunda anadaiwa pesa za pombe na Aunt, kiasi cha Tsh. 100,000/= ambazo kwa maelezo yake anadai alimpa Mose Iyobo. Hapo ndipo tifu likaanza, fuatilia mwenyewe kilivyonuka.

Madee Afungukia Bifu Lake Na Roma

BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, hitmaker wa Ngoma ya Sema, Hamadi Ally ‘Madee’ hatimaye amefungukia kile kinachodaiwa kuwa ni bifu zito lililopo kati yake na msanii mwenzake, Ibrahim Musa ‘Roma Mkatoliki’.


Akipiga stori na Risasi Vibes, Madee alisema suala la uwepo wa bifu kati yake na Roma ni hisia tu zinazo-zushwa na mashabiki kutokana na vijembe wanavyo-tupiana na msanii huyo ambaye kimsingi ni mtani wake.

“Roma ni mtani wangu, mara nyingi huwa kuna masihara kati yangu na yeye, hata familia yake kwa ujumla, vile vijembe ambavyo huwa tunatupiana ule huwa ni utani tu hakuna uhalisia wowote, hatuna bifu kati yetu,” alisema Madee

Barnaba Ataja Kinachomuingizia Mkwanja Mrefu

STAA wa Bongo Fleva mwenye sauti ya kipekee, Elias Barnaba amesema kuwa kitendo cha kuwatungia mastaa ngoma zao hasa wa kike kimemfanya kutengeneza mkwanja mrefu.

Akichonga na Risasi Vibes, Barnaba ambaye kwa sasa amejitoa THT na kuanzisha lebo yake ya Hightable Sound alisema, hawezi kutaja mpaka sasa amepata kiasi gani lakini wasanii wa kike wengi aliowatungia ngoma wamekuwa wakimlipa vizuri.
“Ukiachilia mbali mkwanja ninaoupata kupitia studio na lebo yangu ya Hightable, kazi zangu za muziki, kingine kikubwa ni hawa wasanii ninaowatungia nyimbo, wamekuwa wakinipa mkwanja mrefu,” alisema Barnaba ambaye amewahi kuwatungia nyimbo mastaa kibao wa kike akiwemo Linah, Shilole, Lulu Diva, Recho na wengineo.

Man Fongo Kufikishwa Mahakamani Kisa....


SIKU chache baada ya familia ya mwanamuziki, Mbaraka Mwinshehe, kutoa ruhusa kwa Vanessa Mdee kunakili vionjo vya wimbo wa baba yao (Jogoo la Shamba) na kuviweka kwenye wimbo wake wa Pumzi ya Mwisho, msanii wa Singeli, Aman Hamis, amejikuta matatani baada ya kunakili vionjo vya wimbo wa nguli huyo wa dansi bila kuitaarifu familia.
Mtoto wa Mbaraka Mwinshehe, Kipande Mbaraka, ameliambia Papaso la Burudani kwamba, wao na bendi ya Morogoro Jaz wana hakimiliki ya wimbo huo na endapo watashindwa kuelewana, basi watamburuza mahakamani msanii Man Fongo.
“Sisi tunahitaji kuzungumza naye, tusipofikia mwafaka basi sheria itachukua mkondo wake, wimbo ameutumia umekaa vizuri ila tatizo hatukufanya makubaliano naye,” alisema Kipande.
Man Fongo naye ameliambia Papaso la Burudani: “Nawaomba sana ndugu zangu, mimi sikuyajua hayo wala wasidhani sisi wanamuziki wa Singeli tuna pesa kama Bongo Fleva, ndiyo kwanza tunapambana kuufikisha muziki mbele na niliimba ili na wazee nao wasikilize Singeli wasidhani ni muziki wa wahuni na vibaka kama inavyodhaniwa,” alisema Man Fongo aliyepata matatizo hayo baada ya kutoa wimbo unaoitwa Lau Nafsi.

Steve Nyerere Amvaa Polepole Baada ya Kumkataa Wema Sepetu......." Hiki chama hujakianzisha wewe"

Muda mfupi baada ya muigizaji wa filamu nchini, Wema Sepetu kutangaza jana jioni kuwa ameamua kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM), Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole  alisema chama hicho hakina taarifa rasmi kuhusu Wema kutaka kurudi.

Polepole kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika kuwa, katika kujenga nidhamu ya chama, na kuepuka kukifanya chama daladala kwamba unapanda na kushuka wakati unaotaka, kuna taratibu za kufuatwa mtu anapotaka kujiunga na chama, na sio kutangaza mitandaoni.

“......Chama chetu sio Daladala mtu anaweza kupanda na kushuka wakati wowote, ni heri akabaki hukohuko ama akaanzie kule ambako alichukulia kadi yetu,” aliandika Polepole. 

Kauli hiyo imemuibua Staa wa Filamu aliyekuwa rafiki wa karibu wa Wema kabla hajahamia Chadema, Steve Nyerere ambaye amemtolea povu Polepole na kuijibu kauli yake hiyo akiandika;

“Hiki chama hujakiunda wewe wala kukianzisha wewe, umekikuta kama tulivyokikuta wote, kina waasisi wenye uchungu nacho na wako kimya.

“Wewe ni nani ukatishe watu moyo kukitumikia kama vile ndio unakimiliki, tulia polepole chama cha wote hiki, usilete ubinafsi kwenye kutumikia na kujenga ngome, hatuhitaji wenye cement na nondo tu, acha hata mwenye jiwe lake aweke kikubwa nyumba isimame, ni mchango pia”
 


Wema Sepetu ajivua uanachama Chadema, Atangaza kurudi CCM

Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu ametangaza rasmi kujivua uanachama wa Chadema na kurudi kwenye chama chake cha zamani cha CCM.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema Sepetu amesema hawezi kuishi kwenye nyumba inayomkosesha amani ya nafsi.

“Siwezi Kuendelea kuishi kwenye Nyumba inayo nikosesha amani… Peace of mind is everything for me… Natangaza Rasmi kuondoka Chadema na Kurudi Nyumbani“ameandika Wema Sepetu kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mapema mwezi Februari mwaka huu mrembo huyo alitangaza kuihama CCM na kujiunga Chadema akisema “Nimeamua kufanya uamuzi wa kuhama chama cha Mapinduzi na hivi sasa nataka kuhamia Chadema. Sitaki ionekane kwamba labda nimepata hasira kulingana na hizi tuhuma za hapa katikati ambazo zimenikabili. Lakini nataka nionekane nimefanya maamuzi kama binadamu yeyote ambaye angeweza kufanya. Nadhani wote mnajua kuwa nilishawahi kuwa kada wa Chama cha Mapinduzi, nilikuwa nalisema kwa kujiproud nikiwa nina uaminifu mkubwa kwamba mimi nitasimama kama kweli kada wa Chama cha Mapinduzi”

Alikiba awapa zawadi mashabiki Kwa Kuachia Video Mpya.....Itazame Hapa

Msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Seduce me' Alikiba ameamua kuachia video ya wimbo wake wa zamani ambao ulivuja kama zawadi kwa mashabiki wake katika siku yake ya kuzaliwa.

Alikiba ambaye jana alikuwa anasherehekea kumbukumbu ya mwaka wa kuzaliwa aliamua kuachia video ya wimbo wa 'Maumivu Per Day' kama njia ya kusherekea siku hiyo na mashabiki zake.

"Nashukuru sana watu ambao wamenitakia kheri katika siku yangu ya kuzaliwa, nimejaliwa, kupendelewa na kupendwa pia nashukuru sana kwa jambo hilo, nawapenda wote na nitafanya kazi kwa nguvu zote kuwafanya mjivunie uwepo wangu. 

"Maumivu Per Day ni kati ya nyimbo zangu za zamani zinazopendwa nimeamua kuitoa japo siyo rasmi ili kusherehekea kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa na mashabiki zangu" alisema Alikiba

Wema Sepetu achoshwa....Atamani Kifo

Muigizaji mwenye nyota yake bongo na Afrika Mashariki Wema Sepetu, amesema kuna muda anatamani Mungu amchukue afe ili aweze kupumzika na mambo ya dunia ambayo yanamnyima raha.

Wema Sepetu ameyasema hayo kwa kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram, akisema ingawa anajua ipo siku atakufa, lakini anatamani ingetokea sasa ili aweze kupumzika na mambo yanayomuumiza nafsi yake ikiwemo kutukanwa bila sababu za msingi kwenye mitandao ya kijamii.

Wema Sepetu amendeelea kusema kuwa kutokana na mambo ambayo anayapitia anatamani hata asingetokea duniani, na kuamua kukaa nje ya mitandao ya kijamii kwa muda.

"Ipo siku nitakufa, hakuna anaeishi milele... Sijui mtaendelea kunisema kwa kejeli na kunitukana matusi ya nguoni au ndo itakuwa, “Maskini ya Mungu, Dada wa watu alikuwa hivi na vile, Mungu ailaze Roho yake mahali pema...” Kuna muda mwingine huwa natamani Allah Subhannah wata’allah anichukue tu... Ya Duniya ni mengi sana", ameandika Wema Sepetu.

Wema ameendelea kuandika akisema.." Kuna muda mwingine nakufuru mwenyezi Mungu na kutamani labda hata nisinge exist... Ila acha niendelee kumtegemea yeye... Kila jambo hutokea kwa sababu.... Hili nalo litapita... I think I need a Time Off Social Media... Kwa mara nyingine Tena.... Siwezi jamani".

Licha ya hayo Wema Sepetu hajaweka wazi moja kwa moja ni jambo gani ambalo limemkwaza zaidi, kwani kitendo cha kutukanwa na kusemwa vibaya kwake sio jambo geni. 

Mwanamuziki Nikki wa Pili Aguswa na Matokeo ya Udiwani...Afunguka Haya


Baada ya Matokeo ya Uchaguzi wa Madiwani Mwanamuziki Nikki wa Pili ameandika haya:


Democrasia ni uhuru wa watu kushiriki kujiamulia hatma ya maisha yao, sio kushiriki kupiga kura alafu baada ya hapo hatma inakuwa mikononi mwa watu wachache wanaa amuwa wapendavyo na wengi hawana kauli hamna hata nafasi ya kuhoji #illusion ya democrasia wakilishi

Kajala Aonyesha Umahiri Wake wa Kumtega Shemeji Yake

Video mpya ya 'Omulilo' ambayo ni kazi yake mwanamama Saida Karoli imeachiwa rasmi, huku Kajala akiigiza muhusika aliyeimbwa kwenye wimbo huo.

Video hiyo inamuonyesha Kajala akiwa anaishi kwa shoga yake kipenzi, lakini licha ya kumsitiri anafanya kitendo kibaya cha kumtaka shemeji yake kimapenzi kwa kumtega kwa kumvalia mavazi ya kumshawishi.

Kazi hiyo ambayo imefanywa na mikono ya Hanscana, ni moja ya kazi zilizoachiwa hivi karibuni na Saida karoli tangu arudi rasmi kwenye game, baada ya kishindo cha wimbo wa 'Orugambo'. 

Mama Kanumba Afungukia Cheko Lake Mahakamani

Nawashangaa Wanaonishangaa Mimi Kucheka Mahakamani Wakati Lulu Anaukumiwa Hata Mimi Nililia Wakati Wengine Wakila Bata- Mama Kanumba
MAMA wa aliyekuwa mwigizaji mahiri wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefungukia cheko alilolitoa mahakamani wakati wa hukumu ya mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Mama Kanumba aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, anawashangaa wanaomshangaa yeye kucheka, lakini akawataka wakumbuke kuwa hata yeye alilia mno wakati werngine wakila bata.
Mama Kanumba alisema kuwa, baada ya Lulu kuhukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka miwili kwa kusababisha kifo cha Kanumba bila kukusudia, alijikuta akicheka, lakini hakumaanisha kuwa anafurahia Lulu kwenda jela kwa sababu yeye ni Mkristo hivyo hapaswi kushangilia mabaya ya mwanadamu mwenzake.
“Nawashangaa wanaoona nilivyocheka ilikuwa kosa, kwani mimi nililia mara ngapi?” alihoji mama Kanumba.

Hamorapa Kwishaaa! Meneja Wake Afunguka Mazito

Athuman Omary ‘Hamorapa’.

UBUYU wa leo unatakiwa uumun’gunye taratibu, ukipenda unaweza kushushia na maziwa maana unaambiwa mzee wa kiki ambaye alijizolea umaarufu miezi kadhaa iliyopita, Athuman Omary ‘Hamorapa’, kibarua chake tayari kimeota mbawa kwa meneja wake, Irene Sabuka. Irene Sabuka ndiye yule meneja wake aliyemsaidia kumtoa kisanii na zile mbwembwe zote, lakini sasa unaambiwa mambo ‘kwishnei’.

TUJIUNGE NA MLETA UBUYU WETU
Chanzo chetu makini ambacho ndicho mleta ubuyu wetu kilipepeta mambo kuwa, mwanamuziki huyo aliliamsha dude la meneja wake huyo baada ya kujitokeza kwa promota na kudai kuwa anaweza kumsaidia kupata shoo mbalimbali mikoani. Chanzo hicho ambacho ni mkereketwa na ubuyu wa mastaa kilizidi kutonya kuwa, baada ya promota huyo kuanza kumchukua Hamorapa na kufanya shoo mikoani, hakukuwa na mrejesho wowote wa fedha kwa meneja huyo badala yake walidai kuwa shoo hazikufanya vizuri.
IRENE ADAI KUTUMIA MIL. 70
“Yaani huyo promota na Hamorapa kila wanapokwenda mikoani, wakirudi hawana fedha wakati Irene alishatumia karibia shilingi milioni 70 kwa ajili ya kumtoa mwanamuziki huyo na kuwa juu kisanaa,” alisema sosi huyo.

MENEJA ATIBUKA ZAIDI
Mleta ubuyu huyo anasema kuwa, jambo hilo ndilo lililomtibua zaidi meneja huyo ni baada ya mwanamuziki huyo kuchukuliwa tena na promota huyo bila taarifa yoyote juu ya ni wapi walikokwenda. “Sasa kitu ambacho kilimfanya Irene akasirike zaidi ni kuwa promota huyo alimchukua Hamorapa, bila taarifa na kuondoka naye hivyo kumkasirikia na kumtaka amchukue moja kwa moja na asiwe tena chini yake,” kilifunguka chanzo hicho. HUYU

HAPA IRENE
Ijumaa Wikienda, kama kawaida yake, baada ya kupata ubuyu huo lilimtafuta Irene ambapo alipoulizwa kuhusu hilo
alisema kuwa, anachojua kuwa yeye alichukuliwa na promota huyo kwa kurubuniwa hivyo na yeye aliamua kunyanyua mikono ili aendelee naye. “Ninachojua huyo promota alijifanya anataka kumsaidia kumbe alishaona amepata jina, akataka kumrubuni na mimi nimeamua kumuacha tu kwa sababu ninajua ni wapi nilipomtoa,” alisema Irene.

HAMORAPA ASOMEWA MASHTAKA
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Hamorapa na kumsomea mashtaka yake ambapo alidai kuwa, yeye anachojua bado Irene ni meneja wake na kama siyo ataliweka wazi baadaye. “Kuna vitu vimetokea kweli ila ninachojua Irene bado ni meneja wangu na ninamuomba Mungu tumalize tofauti zilizopo,” alisema Hamorapa.

NENO LA MHARIRI
Kama anavyosema Hamorapa ni jambo la kumuomba Mungu ili wamalize tofauti zao kwani wote wawili wametoana mbali

Baba Ndiku Abariki Irene Uwoya Kuolewa

Staa mkubwa wa filamu Bongo, Irene Uwoya.
WAKATI staa mkubwa wa filamu Bongo, Irene Uwoya akirejea nyumbani kutoka Rwanda alikoenda kwa ajili ya kuhani msiba wa mume wake Hamad Ndikumana ‘Ndiku’, baba mzazi wa mwanaume huyo, amebariki mkwe wake kuolewa na mtu mwingine, Risasi Jumamosi linakuwa la kwanza kukujuza.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwepo katika kikao cha mwisho cha kuagana, Mzee Ndikumana alimwambia mama huyo wa mtoto mmoja kuwa anaweza kuolewa, kwani baada ya mwanaye kufariki, anajua upweke atakaokuwa nao.
Baba mzazi wa mwanaume Irene Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Ndiku’ akifanya maombi.
“Ninachoweza kukuambia ni kwamba Uwoya sasa yupo huru kuolewa, wazee huku wala hawana tatizo naye, ni yeye tu na kwa jinsi nilivyomuona, anaonekana amefurahi sana kwa tamko hilo,” kilisema chanzo hicho ambacho kipo karibu na muigizaji huyo.
Akizungumza na Risasi Jumamosi juu ya ishu hiyo, Uwoya alikwepa kwenda moja kwa moja, lakini akasema aliagana vizuri na familia ya marehemu mumewe na kuwa baba mkwe wake, alimpa faraja kubwa na kuonyesha wazi upendo wao kwake kwani wanamkubali na hakuwa na matatizo nao tangu akiwa na mumewe.

“Jamani alichonifanyia baba yake Ndikumana ni kikubwa sana kwangu, naamini kabisa baraka alizonipa zitanisaidia sana katika maisha yangu kwa sababu hata siku moja sikuwahi kukwazana na familia hiyo na nilikuwa nawaheshimu kama wazazi wangu siku zote” alisema Uwoya.

Uwoya alizidi kufunguka kuwa anawashukuru wazazi hao kwa sababu walimpokea vizuri na kumpa heshima zote kama mkwe yeye pamoja na wazazi wake na mtoto wake Krish kitu kilichomfanya kujisikia vizuri sana.

“Nilikuwa na majonzi sana lakini kwa jinsi walivyonionyesha ukarimu wao mkubwa, nilijisikia vizuri sana na nilijiona mtu mwingine tofauti kabisa na nilifarijika mno” alisema Uwoya ambaye akiwa huko, mtu wake wa karibu alikuwa ni aliyekuwa mpenzi wa sasa wa Ndiku, Asma.

Risasi Jumamosi lilimtafuta mmoja wa watu wa karibu waliosafiri na muigizaji huyo, Mike Sangu ambaye pia ni msanii ambaye alipoulizwa kuhusu ishu ya wakwe kumpa baraka za kuolewa Uwoya, alisema anachokumbuka ni baba mzazi wa Ndiku kumwombea dua, akimtakia safari njema
.
“Hayo mengine mimi siwezi kuyazungumzia, ninachofahamu mzee alimuombea dua na kumtaka aende salama, alimtaka akaendelee na maisha yake, ila asisahau kuikumbuka familia yake, awe anampeleka mtoto Krish huko, walisema wao hawana kinyongo naye kabisa. Walisema tofauti zao na mzazi mwenzake ni mambo ya kawaida katika ndoa, wao hawawezi kuziingilia, ila wanamtambua kama mkwe wao,” alisema Mike.

Marehemu Ndikumana alifariki dunia usiku wa Novemba 14, mwaka huu baada ya kuelezwa kuwa jioni yake alikuwa mazoezini na klabu yake ya Rayon Sports, ambako alikuwa ni kocha msaidizi

Nimeirudisha heshima ya Bongo Movie kama enzi za Kanumba – Wema Sepetu


Msanii wa filamu nchini Tanzania, Mrembo Wema Sepetu ambaye yupo nchini Rwanda tangu Jumatano ya wiki hii, amesema ndiye aliyeifufua tasnia ya Bongo Movie iliyokufa baada ya kifo cha Kanumba.

Wema amesema marehemu Kanumba alipofariki  hata kiwanda cha Bongo Movie kilionekana kuyumba kwani alikuwa ndiye nguzo muhimu kwenye ramani ya filamu Tanzania.

“Zamani Bongo Movie ilikuwa inafanya vizuri sana enzi za marehemu Steven Kanumba, alivyofariki kama na yenyewe ikafa. Tumekuwa tukiomboleza kifo chake na kifo chake kimetusababishia mazingira mabaya sisi kama waigizaji  kwa sababu tuko kwenye fani moja. Wengi wetu tumejikuta watu wanaona Bongo Movie haina mashiko.“amesema Wema Sepetu kwenye mkutano na Waandishi wa Habari jijini Kigali nchini Rwanda na kuelezea jinsi alivyoinyanyua Bongo Movie baada ya kifo cha Kanumba.

“Kwa bahati nzuri mimi nimeweza kuirudisha tena Bongo Movie back to where it was (ilipokuwa enzi za Kanumba) baada ya kutoa filamu yangu ya Heaven Sent. Bongo Movie kama Bongo Movie zilikuwa zimelala kiukweli kabisa mpaka nilipozindua filamu yangu hiyo na nimeweza kuiweka kwenye application yangu kumekuwa kuna muhemko, yaani waigizaji wengi hata mkiwaona kwenye mitandao ya kijamii wanashoot, wanafanya vipindi, yaani Bongo Movie haijafa ni kazi nzuri tu tumeshindwa kuziweka sokoni. Tukiwa tuna kazi nzuri tukafanya vitu ambavyo vitapendwa na watu Bongo Movie itakuwa imara tena Inshallah!“.

Steven Charles Kanumba almaarufu The Great alifariki katika mazingira ya kutatanisha mnamo mwezi Aprili 2012 akiwa chumbani kwake na mpenzi wake Elisabeth Michael ‘Lulu’ ambaye mwezi huu amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kumuua Kanumba bila kukusudia.

Msikilize hapa Wema Sepetu akizungumza na Waandishi wa Habari nchini Rwanda ambako alienda kwenye  tamasha la KFM Instagram Party ambalo limefanyika jana ijumaa

Mama Wema Aonywa na Hakimu Kisa Mwanae Kushindwa Kufika Mahakamani

Mama Wema Aonywa na Hakimu Kisa Mwanae Kushindwa Kufika Mahakamani

MAMA wa Miss Tanzania 2006 na msanii wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu, Miriam Sepetu, leo alionywa na hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba baada ya mwanae huyo kushindwa kufika mahakamani ambapo anakabiliwa na kesi la matumizi ya madawa ya kulevya.

Katika kesi hiyo Wakili wa Serikali Agustino Michael aliitaja kesi hiyo mbele ya hakimu Simba kuwa ndiyo iliyokuwa ikitakiwa kuendelea lakini mama Wema alinyoosha kidole kuashiria kuwa na neno.

Hakimu huyo alimkaribisha mama Wema kusema jambo alilotaka kusema ndipo akaanza kutoa hudhuru na kuiambia mahakama hiyo kuwa Wema alishindwa kufika mahakamani hapo kufuatia kufiwa na shangazi yake.

“Mheshimiwa Wema amefiwa na shangazi yake hivyo ameenda kushughulikia suala la mazishi ndiyo maana hakuweza kufika hapa mahakamani mimi ndiyo  nimekuja kumuwakilisha” alisema Mama Wema.

Baada ya mama huyo kutoa hudhuru huo hakimu alianza kumbana maswali ambapo alimuuliza kama Wema amepatwa na msiba uliomfanya ashindwe kufika mahakamani imekuwaje yeye mama yake apate muda huo yeye ashindwe?

Aliuliza hakimu huyo kisha kumuonya mama Wema kwa kumuambia siku nyingine asichukulie masihara suala la mshitakiwa huyo kuripoti mahakamani.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Desemba 14 mwaka huu. 

Wema Sepetu Aongelea Mpango Wake Wa Kurejea CCM

Mrembo wa Tanzania na Muigizaji Wema Sepetu amemfunga mdomo muigizaji mwenzake Steve Nyerere kwa kumwambia hana mawazo ya kurudi CCM kama jinsi ambavyo wengine wanavyofanya.

Wema amefanya tendo hilo kwa kujibu ujumbe wa Steve Nyerere aliokuwa ameuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram akimkaribisha ndani ya CCM, Wakili Alberto Msando ambaye mapema jana alitangaza kujiunga na CCM.

Steve aliandika "Sasa utakuwa mzalendo wa kweli , Msando naheshimu maamuzi yako maana ni maamuzi sahihi, kwako pamoja na family yako , rafiki zako nasi tupo pamoja nawe, soon na yuleeeeeeeee rafiki yetu , dada yetu , msanii mwenzetu , naye yupo njiani kurudi nyumbani"

Hata hivyo Wema Sepepetu baada ya kuona ujumbe huo ambao alihisi kama inamlenga yeye, alijibu chini ya ujumbe huo kwa kuandika "I hope hauniongelei mimi... Maana mawazo hayo sina"

Muigizaji Wema Sepetu alihama ndani ya chama cha mapinduzi Februari mwaka huu kwa madai kuwa ameamua kujiunga na Chadema kupigania demokrasia ya kweli.

Dr. Shika Kushiriki Kwenye Video Ya Dogo Janja?


 Kila siku umaarufu wa Dk.Luis Shika unazidi kuongezeka na hata baadhi ya watu na makampuni wameanza kumtumia katika biahara zao, hii ni pamoj na picha zilizoanza kusambaa zikimuonyesha yupo na msanii wa muziki Dogo Janja.

Kutokana na picha ambazo zimeanza na zinaendelea kusambaa mtandaoni zikimuonyesha Dk.Shika au Mzee wa 900 Itapendeza akiwa katika muonekano wa kipapa na huku akiwa ana kula bata na warembo, jambo linalohisiwa kuwa huwenda kukawa na video mpya ya muziki kutoka kwa msanii Dogo Janja hivyo ametumika kama muhusika mkuu.

Dk. Luis Shika amejipatia umaarufu kutokana na sakata la kuuzwa kwa nyumba za mfanyabiashara Said Lugumu, ambapo aliingilia katikwa kutaja kiwango kikubwa cha pesa ili aweze kununua nyumba hicho ila cha kushaa baada ya kuibuka mshindi hakuwa na 25% za kumfanya aweze kuwa mmiliki halali wa nyumba hizo na kufanya polisi wamkamate na kumuweka ndani ambapo alitoka baada ya siku kadhaa na kuanza kupata umaarufu mara dufu.


Wasanii Wa Tanzania(Off Side Trick) Wasababisha Kufungwa Kwa Tamasha Kenya


Kundi la wasanii wa muziki wa Tanzania kutoka visiwani Zanzibar, Off Side Trick, wamesababisha kufungwa kwa tamasha la utamaduni la Lamu huko Mombasa nchini Kenya, baada ya kucheza mtindo usiofaa wenye kukiuka maadili.

Taarifa kutoka Mombasa zinasema kwamba kitendo hiko kililalamikiwa na wakazi wa eneo hilo, viongozi wa dini na viongozi wa utamaduni wa Kenya, baada ya kuangalia kile kilichokuwa kikiendelea jukwaani na kulazimu tamasha hilo kufungwa.

Baadhi ya watu walijaribu kuwaonya kundi hilo kuacha kucheza michezo hiyo ya uchafu ambayo sio maadili lakini walijifanya kutosikia, na ndipo waandaaji wa tamasha na viongozi wa eneo hilo kupanda jukwaani na kuwashusha kwa nguvu .

Baada ya tukio hilo Mkurugenzi Msaidizi wa Nyumba ya Maonyesho wa Kenya, Bwana  Athman Hussein, amesema kuna haja ya kuwahakiki wasanii kabla hawajapanda jukwaani, kwani kitendo hiko kimedhalilisha jamii ya hapo na mji wa Lamu kiujumla, kwani mji huo ni maarufu kwa utalii na pia uko chini ya Urithi wa dunia wa UNESCO.

Maneno Ya Mama Lulu Baada Ya Mwanae Kwenda Jela

Elizabeth Michael ‘Lulu’.


SIKU tano baada ya mwanaye ambaye ni staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ mama yake mzazi, Lucresia Karugila, kwa mara ya kwanza amefunguka baada ya mtoto wake huyo kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia staa mwenzake, Steven Kanumba aliyekuwa pia mwandani wake.

Awali, kulienea lawama nyingi mitandaoni baada ya Lulu kuhukumiwa kuwa huenda kuna mahali wazazi walikosea malezi ndiyo sababu ya mtoto wao huyo kujihusisha na masuala ya kimapenzi akiwa na umri wa chini ya miaka 18 ambao hakubaliki.

Kufuatia hali hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta mama Lulu ili kujua mtazamo wake juu ya mwanaye kwenda jela na madai ya mitandaoni ndipo akafunguka mazito. Mama Lulu aliliambia gazeti hili kuwa, kwa sasa hapendi kuzungumza hovyo na watu na anahitaji muda mwingi wa kupumzika kwa kuwa hayuko vizuri. “Nafikiri kwa kipindi hiki nahitaji zaidi kupumzika kwa muda mwingi na sipendi kuzungumza hovyohovyo, siko vizuri kabisa,” alisema mama Lulu kwa sauti ya unyonge.

Lulu akiwa na mama yake Lucresia Karugila.
Akiendelea kuzungumza, mama huyo alisema kuwa, tangu apate majanga ya mtoto wake huyo hadi kwenda jela hayupo vizuri na wala hapendi kuongea kwa sababu hajisikii kufanya hivyo kwani anahisi anaiona dunia chungu. “Najua watu watanishangaa sana, lakini ndiyo nimeamua kuwa hivyo, siko sawa na sijisikii vizuri kabisa. “Sidhani kama kuna mzazi yeyote anaweza kupata usingizi wakati mwanaye yupo kwenye mateso kama ilivyokuwa zamani, kiukweli ninaumia sana,” alisema mama Lulu.

DAKTARI NAYE ANENA!

Naye daktari wa magonjwa ya binadamu, Dk Godfrey Chale, akizungumzia hali ya Lulu baada ya hukumu hiyo alisema kuwa, kuna magonjwa ambayo huweza kumpata mtu mwenye matatizo ya kimaisha ikiwemo kufungwa jela ikiwa ni pamoja na kuwa kichaa kutokana na msongo.

Dk Chale alisema mara nyingi watu ambao hupatwa na majanga makubwa kama la Lulu, huwa kwenye uwezekano mkubwa wa kukumbwa na msongo ambao husababisha mpangilio mbovu wa homoni kiutendaji na mhusika kuchanganyikiwa endapo atashindwa kukubaliana na mazingira ya tatizo.
Alisema kuchanganyikiwa kwa watu wenye matatizo kama ya Lulu, hutokana na kuzidiwa na huzuni na mgandamizo wa hisia (depression) hivyo kushindwa kabisa kuzuia mfumo wa kufikiri na kutafakari na ndiyo maana unakuta mtu anaongea peke yake au kufanya vitendo vya ajabu kama kuokota vitu mbalimbali kama sehemu ya kujifariji na hapo ndipo tatizo la kuchanganyikiwa huanzia.

Tatizo kubwa jingine ambalo linaweza kumpata Lulu ni kupoteza popularity momentum (nguvu ya umaarufu) na kushuka kwa uchumi atakapomaliza kifungo kwani kwa kipindi ambacho yuko jela atapoteza mikataba yake ya kikazi kama matangazo na uigizaji, vitega uchumi ambavyo vilikuwa vikimuingizia kipato cha kuyaendesha maisha yake
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017