Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter
Showing posts with label MAPENZI. Show all posts
Showing posts with label MAPENZI. Show all posts

Mauaji Ya Kutisha Dar… Mume Afanya Unyama!

Matau Ngosha na Upendo Jonathan, enzi zao.
“KWa kweli ni mauaji ya kutisha! Wakati wakiingia chumbani kwao kulala, hakuna aliyetarajia leo (Ijumaa iliyopita) kama tungeamka na kuambiwa Ngosha na Pendo ni marehemu,” ndivyo walivyokuwa wakisema majirani wa Matau Ngosha na Upendo Jonathan ambao walikuwa mume na mke waliokutwa na umauti usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita.
TWENDE MADALE
Tukio hilo la kutisha lilitokea katika Kijiji cha Nyakasanga, Madale, nje kidogo ya Jiji la Dar ambapo mume, Mat alidaiwa kumuua mkewe kwa kumnyonga chumbani kwao kisha naye alikwenda kujiua kwa kujinyonga kwa shuka kwenye nyumba ya mwalimu iliyokuwa inajengwa.
Ijumaa Wikienda lilifika eneo hilo la tukio muda mfupi baada ya miili ya wawili hao kuondolewa na polisi na kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo, Dar.
Pendo Jonathan enzi za uhai wake.
DADA WA MAREHEMU ASIMULIA
Akisimulia tukio hilo lililoibua taharuki na simanzi nzito kijijini hapo, dada wa marehemu, Jennifer Mponzi alisema:
“Nilikuwa kazini asubuhi ya leo (Ijumaa), nilipigiwa simu nikaambiwa kuna tatizo limetokea hapa nyumbani, hawakutaka kuniambia ni tatizo gani hadi nilipofika na kukuta mdogo wangu amekufa.
“Nimeumia sana maana mdogo wangu hakuwahi kuniambia kama ana mgogoro na mumewe. Lakini mwanaume anahusishwa na mauaji ya mkewe maana funguo za chumba chao alikuwa nazo mfukoni.
Ndugu wa marehemu.
“Nashindwa kuamini maana jana (Alhamisi) nilipishana na Pendo mjini akiwa kwenye bodaboda na alionekana mwenye furaha kama kawaida.
“Hata jioni majirani waliwaona Pendo na mumewe wakiwa hawana shida yoyote. Kwa hiyo inawezekana ni wivu wa kimapenzi lakini Pendo alikuwa msiri sana maana hajawahi kuniambia chochote kama kuna tatizo.

Ndugu wakiwa wameketi.
“Lakini pia kinachoumiza zaidi mtoto wao wa umri wa miaka minne alikutwa ndani akiwa amelala usiku kucha na maiti ya mama yake akidhani mama amelala usingizi wa kawaida, inauma sana jamaniii…!”

Ndugu wa marehemu.
MWENYEKITI NYAKASANGA
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mwenyekiti wa Nyakasanga, Peter Bilevera aliliambia Ijumaa Wikienda kwamba, tukio hilo ni mwendelezo wa matukio kama hayo kwenye eneo lake kwani miezi kadhaa iliyopita kijana mmoja naye alidaiwa kujinyonga.
Mwenyekiti wa mtaa.
“Nilipata taarifa, nikafika eneo la tukio, nikatoa taarifa polisi kwenye kituo kidogo cha Madale ambao walifika na kuiondoa miili ya marehemu na kwenda kuihifadhi Lugalo.
“Bado familia zote hazijapanga utaratibu wa mazishi hivyo tunasubiri, lakini ukweli ni kwamba kuna watu wanasema kulikuwa na mambo ya wivu wa kimapenzi,” alisema mwenyekiti huyo.

Tendo La Ndoa Ni Tiba Kiafya..Je Linatibu Magonjwa Gani? Soma Hapa


Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Wataalamu wanasema kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75. Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.

Kuongeza mwendo wa damu
Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili, hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji. 

Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.

Hupunguza mafuta yenye kileo (Cholesterol)
Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha mafuta yenye kileo mwilini.

Kupunguza maumivu
Wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo hupunguza maumivu kama vile kuvimba sehemu za viungo (arthritis) maumivu ya shingo (Whiplash) na maumivu ya kichwa.

Ulinzi wa tezi ya kibofu (mwanaume)
Majimaji yanayozalishwa katika tezi ya kibofu (prostate) yakizidi husababisha kuleta matatizo mwilini. Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji hayo yenye madhara. Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa huelekea kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate.

Kupunguza mfadhaiko wa moyo
Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini. Watu wenye kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.

Huongeza uzalishaji wa homoni za kiume(testosterone) na za kike (Oestogen). 
Faida nyingine inayopatika ni kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za kike likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi. Hata hivyo, baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kiume/ kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.

Kuishi muda mrefu huku ukionekana kijana
Wakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima. Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka. Kutokana na elimu hiyo DHEA ni kemikali yenye nguvu duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu, kuimarisha mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo (Cardiovascular).

Hupunguza baridi na mafua
Elimu inaonesha kuwa wanaofanya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki huongeza 30% ya uzalishaji wa chembe chembe hai za mwili ziitwazo Immunogloulin A ambazo huwa na kazi ya kuulinda mwili dhidi ya magonjwa. Hizo ni faida chache tu za kufanya tendo la ndoa. 

Wakati mwingine nitawaletea hasara za kufanya tendo hilo mara kwa mara. Jambo kubwa la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa. Ndiyo maana nikasema ni maalum kwa wanandoa tu.


UTAMU::Amtosa Mumewe Mzungu, Achukuliwa Na Kiserengeti Cha Gambia

Mama mwenye watoto tisa Heidi Hepworth (44) akiwa na mpenzi wake wa sasa Mamadou Jallow.

MWANAUME mmoja mkazi wa Uingereza Andy Hepworth, amesimulia kwa huzuni jinsi mkewe Heidi Hepworth (44) alivyomtosa, akamwachia watoto tisa na hivi sasa anajirusha na kivulana cha kutoka Gambia, Afrika.

Mwanamke huyo anaishi na kijana huyo anayejulikana kama Mamadou Jallow (30) baada ya kufahamiana kupitia Mtandao wa Facebook ambapo aliamua kumfuata hukohuko Gambia na mpaka sasa anaishi naye huko.
Jinsi alivyokolewa na mapenzi hayo mapya, sasa Heidi anadai talaka na kusema kuwa amempata ampendaye zaidi.

…Enzi ya ndoa yao na mume wake Andy.
“Ni jambo la ajabu, alianza tabia ambazo sikuzifahamu. Alianza kwenda gym, akakodisha vitanda maalum vya kuotea jua kwenye fukwe, akaanza kujichora tattoo na kuvaa nguo za ajabu,” anasema Hepworth na kuongeza: “Amekuwa mtu wa ovyo. Mwanzoni alikuwa mama mwenye upendo na anayejua majukumu yake.


Hivi sasa ni kama shetani ameukamata mwili wake. Kijana aliyenaye ameivuruga akili yake ambapo na yeye anafuata kila kitu.” Heidi naye anasema: “Nimekutana na kijana mpya, jambo ambalo si la kushangaza.
…Akiwa na mume wake Andy.
Ndoa yetu imekuwa na matatizo kila mara. Tulijikuta hatuna uhusiano mwema,” Andy na Heidi walikutana mnamo miaka ya 1990 na wameishi kwa miaka 23 na kuzaa watoto tisa. Andy anasema: “Tulikutana akiwa na watoto watatu kutoka kwa mwanaume mwingine lakini niliwachukua kama wangu.

Afukuza ambapo mimi na yeye tulizaa watoto tisa.” Anaongeza kwamba alianza kuyaona mabadiliko kwa mkewe huyo tangu Machi mwaka huu baada ya kugundua majina ya marafiki wa kiume kutoka Afrika na Asia kwenye kompyuta yao ya nyumbani na alipomwuliza alikana.
Hivi sasa Heidi na Mamadou wanaishi jijini Banjul na mama huyo amekanusha kwamba anatumiwa na kijana huyo ili apate pasipoti ya kuingia Uingereza. “Hilo halipo kabisa, nimempenda, basi! Hakuna mwingine. Kuhusu watoto, bado nawakumbuka sana. Sidhani kama nitaondoka hapa, lakini watoto wangu bado nawakumbuka,” alisema Heidi.

Utafiti Usio Rasmi:Majina Ya Wasichana / Wanawake Na Sifa Zake Katika Mapenzi..Angalia La Demu Wako Sasa

1::Nancy -Muongo
2::Julieth -Kicheche
3::Mary -Anapenda waume wa kitambo kirefu
4: Caroline-Anapenda kusikilizwa kuliko kusikiliza
5:: Hellen- Anabusara anapozugumza na mpenzi wake
6::Rose-Anapenda wanaume wenye pesa
7::Eunice- Hapendi ndugu wa mume wake
8::Agness-Anaupendo wa dhati na akipenda amependa kweli
9::Eveline -Hana vigezo vya mwanaume anaemtaka
10:: Catherine- Mbinafsi ktk mapenzi anajijali pekee kuliko mpenzi
11::Mariam-Anapenda kuwa kuwa rafiki na mpenz wake
12::Loveness-Akitendwa anachukia mapenzi kwa muda mrefu
13::Monica-Anajivunia mpenzi wake popote
14::Mellisa-Hapendi kuonyesha huzuni kwa mpenzi wake hata kama amekereka
15::Elizabeth-Hapendi kujihusisha na mahusiano
16::Emy-mtaalamu wakutongozea marafiki zao
17::Fabiola -Anapenda sifa za wanaume
18::Theresia-Mvumilivu ktk mapenzi
19::Eve -Hana mwanaume maalumu
20::Hilda -Muumiza mioyo ya wanaume wengi
21::Jackline -Ni mlipiza kisasi
22::Lydia -Anapenda mtu ili apate kitu fulani
23::Carol -Nimuongo kupitiliza na still anaaminika
24::Josephine -Hataki mpenzi but anataka mume
25::Grace -Anapendwa na wanaume wengi japo hataki hata mmoja ktk hao wengi
26::Anna -Anaishia kwenye sogea tuishi bila ndoa
27:'Beatrice -Ana maringo mpaka wanaume wanamuogopa
28::Rehema -Anapenda waume za watu
29:: Brenda -Akipenda amependa kweli
30::Frida-Amezubaa anaweza hata kuibiwa mpenz wake na anaangalia tu
31:'Ruth -Ni msaliti kwenye mahusiano
32::Rachel - Ni mwepesi kuachana na mwanaume hata kwa kosa dogo tu
33::Neema -Akiachwa mara moja anakata tamaa
34::Aneth -Hana maamuzi sahihi kwenye mahusiano yake
35::Esther -Anaamini kuwa kwenye mahusiano yakimapenzi ni dhambi
36::Violeth -Mkorofi
37:: Sylvia -Mkimya sana awapo na mpenzi wake
38::Christine -Hajali chochote kinachoendelea kwenye mahusiano yake
39::Julieth -Ana aibu sana kwenye mapenzi
40::Magreth -Anapenda sana ila anaumizwa sana 


Yanayosababisha Kutokuwa Sawa Katika Tendo La Ndoa

WIKI hii mpenzi msomaji wangu tutaangalia jinsi tatizo hili la kutokuwa sawa katika tendo la ndoa linavyotokea. Tatizo hili tunaliweka katika makundi manne. Kwanza ni kutokuwa na hamu na hisia ya tendo la ndoa au kitaalamu tunaita Sexual Desire Disorder.

Hapa hamu na hisia zinaweza zisiwepo kabisa, yaani usiwe kabisa na hamu au hisia ya tendo. Hii ni hali ya jumla lakini, wengine hutokewa na hali ya kupoteza hamu na hisia kwa mpenzi aliye naye tu ila akienda kwa mwingine hufurahia, hali hii inaweza kutokea kwa mwanaume au mwanamke.

Mtu pamoja na kuwa katika hali hii, lakini inaweza kutokea mtu akawa na hamu kidogo sana au ikawa inatokea kwa vipindi fulanifulani baadaye ikapotea. Hii inatokana na upungufu wa vichocheo vya Estrogen kwa wanawake tu na Testosterone kwa wote wanaume na wanawake.

Vyanzo vingine katika hili ni umri mkubwa hasa kwa wazee, uchovu wa mwili kutokana na kazi au ulevi, hali ya ujauzito, matumizi ya baadhi ya madawa na magonjwa ya akili. Pili ni kutokuwa na msisimko wa tendo la ndoa hali iitwayo kitaalamu Sexual Arousal Disorders.

Hali hii kwa mwanamke huitwa ubaridi wa hisia za mwili na kwa mwanaume huitwa ukhanithi ambapo kwa sasa mwanaume mwenye hali hii ya kutokuwa na msisimko ni yule ambaye uume wake hausimami kabisa kwa kuwa hana msisimko wa mapenzi.

Kutokuwa na hisia na msisimko, maumivu wakati wa tendo husababisha usifike kilele cha tendo la ndoa. Kutokuwepo msisimko wa kutosha katika uume na ukeni kutokuwa na majimaji
ya kulainisha uke huwa ni tatizo linalotokana na magonjwa katika viungo vya uzazi na vichocheo. Magonjwa sugu kama kisukari, moyo, kansa, ini, figo huchangia hali hii ya kupoteza msisimko.


Tatu ni uume kutokuwa na nguvu au Erectile Dysfunction. Uume ukikosa nguvu maana yake huwezi kufanya tendo la ndoa. Hali hii husababishwa na magonjwa ya mishipa ya fahamu ya uume na mengine yote sugu ambapo tumeyaelezea ambayo huathiri msukumo wa damu katika uume. Uume kukosa nguvu husababishwa na tatizo la kisaikolojia au la mwili kwa ujumla.

Nne ni tatizo la kuwahi kumaliza tendo la ndoa kitaalamu tunaita Premature Ejaculation. Tunaposema kuwahi kumaliza tendo la ndoa ni pale mwanaume anatoa manii kabla ya mwanamke unayeshirika naye hajafikia kileleni, ingawa hakuna muda maalumu wa kumaliza tendo la ndoa, ila inatakiwa mwanaume asimalize tendo la ndoa yaani usitoe manii chini ya dakika mbili. Endapo utamaliza tendo chini ya dakika hizo mbili basi tunasema una tatizo hili la Premature Ejaculation.

Tatizo hili linaweza kuwa sugu kwako kama hutazingatia ushauri wa kujitibu kwa njia mbili za kujizuia kuwahi, muone daktari wa masuala ya uzazi akusaidie jinsi ya kuwa imara na usiwahi ingawa mazoezi ya kegel ndiyo tiba kubwa. Pamoja na matatizo haya makuu manne, yapo pia mengine ambayo huathiri kwa kiasi kikubwa matatizo haya kama vile kutofika kileleni ambapo mtu anapata msisimko kama kawaida anafanya tendo vizuri lakini hafiki kileleni. Lingine ni maumivu wakati wa tendo.

Mwanaume anaumia uume na mwanamke anaumia ukeni, vilevile wengine huugua baada ya tendo hasa pale wanapofikia kileleni mfano mwili wote kuuma na kuchoka, kuumwa kichwa. Matatizo haya tunakuja kuyazungumzia kwa undani katika mada yake.

NINI CHA KUFANYA?
Endapo unahisi una matatizo kama haya, basi muone daktari wa masuala ya uzazi katika hospitali ya mkoa. Mengine tayari tulishayazungumzia katika makala zilizopita juu ya utatuzi wake kwa hiyo unaweza pia kupitia katika tovuti yetu  makala za afya.

Kuhonga Sio Ticket ya Kupendwa...Wanaume Shtukeni Acheni Kujipa Moyo Mtazidi Kufa Kwa Presha


Jamani tuongee ukweli,kuhonga hakuongezi kupendwa palipo penzi la dhati. Penzi la muda mfupi au la siku moja kuhonga kutaweza kukusaidia lakini kwa mwanamke au mwanaume anayekupenda haihitaji kuhonga. hii sio kwa wanaume tu hata wanawake wanaohonga.

Kwa uzoefu wangu huu penzi la kweli halipatikani kwa kuhonga bali kuridhiana na kupendana.
Usijidanganye wala kujipotezea muda na pesa zako kuhonga kutafuta penzi la dhati utajuta bure.

Ndio Mwisho wa siku mnakuja kufa kwa Presha Shtukeni wanaume

Karibuni wadau kuongezea elimu au kuniweka sawa. 

Ukipata Mwanamke Mwenye Sifa Hizi 16 Usimwache


Hizi ni sifa halisi za mwanamke wa kweli

1. Ni nguvu ya mwanaume
2. Ni jasiri
3. Mchapakazi
4. Mwenye kujiamini
5. Tegemeo la familia
6. Mwalimu wa watoto na familia yake kiujumla
7. Mlinzi wa mwanaume.
8. Chanzo cha baraka ya familia.
9. Adui wa maadui wa familia.
10. Sauti ya familia.
11. Mponyaji wa familia yake na taifa.
12. Mlezi wa huduma.
13. Mkombozi wa familia na taifa.
14. Msaidizi wa Mungu tumfanyie msaidizi wa kufanana naye.
15. Mwombezi wa familia, huduma na taifa.
16. Mficha siri wa Mungu

Madhara Ya Kuangalia Video Za Ngono Na Namna Ya Kuacha


Kuangalia video za ngono sio jambo jipya kwa jamii yetu, kimsingi ni watu wachache sana wanaweza kujizuia kujichua au kupiga punyeto baada ya kuangalia video za ngono.

Bahati mbaya tabia ya kuangalia video hizi watu wengi huipata wakiwa wadogo sana na usipokua makini tabia hii itakufanya vibaya sana kisaikolojia.

Tabia ya kujichua sasa iko wazi kwa jinsia zote yaani wanawake na wanaume japokua imekua ikiathiri zaidi wanaume sababu ya maumbile yao.

Japo wengi hufanya kwa siri na kuficha ili wasijulikane na wengine. Vijana wengi wamekuwa wakiangalia video hizo wakiwa wamejificha wenyewe chumbani, na hasa nyakati za usiku.

Kuangalia video za ngono kuna madhara mbalimbali ya kiafya na kisaikolojia. Haya hapa ni baadhi ya madhara unayoweza kuyapata kama utaangalia sana video za ngono.
Kuishiwa hamu ya tendo la ndoa na nguvu za kiume

Usipitwe na Habari Muhimu, Install App  Yetu


Android ===>  Bofya hapa

Kuangalia sana video za ngono hukufanya ushindwe kusisimuliwa na mwanamke au mwanaume wa kawaida, video za ngono zina wanawake na wanaume wazuri sana ambao wako vile sababu ya kufanyiwa upasuaji mbalimbali wa kuongeza makalio na matiti, hata wanaume hufanyiwa upasuaji wa kuongeza uume hivyo mwanamke anayeangalia atatamani uume mkubwa kama ule au mwanaume anayeangalia atatamani mwanamke kama yule ambaye katika mazingira ya kawaida hayupo.

Sasa wanaume wanao angalia video za ngono hawawezi kusisimka au kuamsha uume hata mwanamke wa kawaida akipita uchi na hii huweza kuathiri sana mahusiano yao na kuonekana hawana nguvu za kiume kwani wao hutegemea video hizo kuamsha uume.

Kujichua au kupiga punyeto sana
Video za ngono zina wanawake na wanaume tofauti, kila video nzuri unayoangalia utaenda kujichua huku ukimuwaza wanaume au mwanamke husika. Hii itakufanya ujichue hata mara kumi kwa siku kama unaziangalia mara kwa mara. Kuishiwa nguvu za kiume, kusahau sana, kushindwa kumpa mwanamke mimba, kuchoka sana na kufika kileleni haraka wakati wa tendo la ndoa ni moja ya madhara makuu ya punyeto.

Kushindwa kudumu kwenye mahusiano
Kuangalia video za ngono hukufanya uwaze kujiridhisha mwenyewe tu na hata mwenza wako akitaka kulala na wewe unakua hutaki tena. Lakini hata kwa vijana ambao hawako kwenye mahusiano hujikuta wanakua waoga sana kuwafuata wanawake au wasione sababu ya kua kwenye mahusiano. Vile vile wanaume hushindwa kuwaridhisha wenza wao na wanawake kusingizia kuchoka kila siku.

Kuanza kufanya ngono ambazo sio za kawaida
Hivi karibuni idadi kubwa ya wanawake wamekua wakijihusisha sana na mapenzi ya kinyume na maumbile. Hii imesababishwa sana na kuangalia video za ngono na kuona ni kitu cha kawaida wakati kina madhara mengi. Wanawake waliozoea kuingiliwa nyuma hata wakiolewa huendelea kufanywa na wanaume wa nje hasa kama waume waliowaoa hawajawahi kujihusisha na tabia hiyo. Aina zingine za ngono ambazo zinababishwa na tabia ya kuangalia video hizi ni ushoga, usagaji, au mwanamke kulala na wanaume zaidi ya mmoja au mwanaume kulala na wanawake zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.

Inawezekana wewe unayesoma hapa tayari hii tabia inakuumiza sana kwa sasa na umeshindwa kuiacha, kuna mambo ya msingi unaweza kufanya ili uweze kuacha kuangalia video hizi..

Ondoa zana zote za kuangalia video hizi
Kama una tarakilishi (computer) au simu futa video zote, futa tovuti (website) zote za video ambazo unazitumia kuangalia. Kuna watu wamo kwenye makundi ya WhatsApp ya kutumiana video za ngono, ondoka kabisa huko kwani unajiharibu.

Anza kufanya mazoezi
Ni mazoezi pekee yanayoweza kumfanya mtu aweze kuachana na tabia zote ambazo sio za kawaida ambazo alikua anazifanya kipindi cha nyuma. Unapofanya mazoezi utatumia nguvu nyingi na mwili wako utachoka na kupata usingizi. Vilevile ufanyaji wa mazoezi hukuepusha na kukaa bila shughuli yoyote.

Jijengee tabia ya kukaa na marafiki zako muda mrefu au kufanya shughuli nyingine zitakazokuweka ‘busy’

Kama una tabia ya kuangalia video hizi basi, fanya mpango uwe unafanya mambo mengine muda ambao umekua ukiangalia hizi video, ikiwemo kusoma vitabu au kuongea na watu. Hii itakusaidia kusahau video hizo na kuacha kabisa.

Pata ushauri wa kitaalamu na matibabu
Unaweza kumuona mtaalamu wa ushauri wa kisaikolojia ili kukusaidia ushauri wa namna ya kufanya ili kuepukana na tabia hiyo. Kama umeshapata madhara kiafya, basi waone wataalamu wa afya hasa masuala ya uzazi ili wakushauri namna ya kulitibu tatizo lako.

Jenga mahusiano ya karibu na mpenzi wako
Hii itakusaidia kumuwaza yeye zaidi ya video za ngono na pia pale unapopata hamu ya kufanya mapenzi basi hutoogopa kumwambia ili mfanye. Kuwa karibu na mpenzi wako kutakujengea ujasiri na kuyakuza mahusiano yenu.

Kama hii ni Kweli basi Wanaume wengi Tunachekwa sana Vitandani


Inasemekana kwamba ukiwa unafanya mapenzi / unabaiolojiana na Mwanamke yoyote yule halafu pale unapomaliza mshindo wako / unapiga bao lako la Kichuya au Ajib halafu ukaona Yule Mwanamke hakukumbatii kwa kukubana kwa nguvu kabisa hadi hata unashindwa kupumua vizuri na kutikisa kabisa mwili wako na Fito zako ( miguu ) basi jua ya kwamba hapo 100% hujamfikisha / hujamtosheleza Kimahaba na ulichokifanya Kisayansi wanasema work done zero.Ila ikitokea kinyume chake basi jua kwamba Mwanamume umeshughulika na Mwanamke kafika katika Kilele chake cha Utamu na Raha ya Mkuyenge wako.

Je kuna Wanabaiolojia wenzangu hasa Wanaume wenzangu je hapa kuna ukweli wowtote labda? Hii habari / taarifa nimeipokea kwa mshtuko mkubwa mno hadi nimeshakosa raha kwani kusema kweli Mimi binafsi nakumbuka kabisa mwaka wa mwisho Kukumbatiwa hivyo kama ilivyobainishwa hapo juu nadhani ilikuwa ni mwaka 2000.

Sasa nawaza tu mwenyewe ( Am just thinking aloud ) kwamba kumbe inawezekana kabisa GENTAMYCINE tokea mwaka 2001 hadi sasa 2017 Wanawake / Mademu wote niwaowabandua / ninaobaiolojiana nao nafanya tu hiyo work done zero? Kwani sijawahi Kukumbatiwa hivyo kama hao Wataalam wa Mapenzi / Mahaba wanavyosema hapo juu.

Na sijui kwanini na Mimi niliamua kumuhoji hili swali huyu Mtaalam kwani hayo majibu yake sasa yamekuwa ni maumivu na mateso makubwa sana moyoni mwangu ila moyo wangu utatulia pale labda na Wataalam wengine wa JamiiForums watakapoliweka hili sawa. Yaani nawaza kwahiyo kumbe kujipinda Kwangu kote tokea 2001 hadi sasa 2017 nafanya Kazi bure tu / work done zero mbele ya Mbunye?

Nawasilisha. 

Tabia Ya Kuzoeana Inavyoweza Kuathiri Maisha Yako Ya Kimahusiano


kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja kumfahamu mwenzake, lakini kuzoeana huku kunaweza kuzalisha dharau hususani kwa upande wa mwanamke kwa kutojali usafi wake, mavazi anayovaa, chakula anchopika, nidhamu ya nyumba na mpangilio kwa ujumla.

Matatizo mengi ndani ya nyumba yanaweza kusababishwa na moja au baadhi ya tabia hizo, ambazo huenda ikawa hazitokani na dharau, bali kuzoeana, kwa mfano, siku za mwanzo wa ndoa mwanamke huwa anajali sana usafi wa mwili wake, umaridadi wa nguo anazovaa, usafi wa nyumba na nidhamu ya hali ya juu, upishi wa chakula unaozingatia vionjo na ubunifu, mapokezi yenye bashasha na wakati mwingine hata kumkumbatia mumewe arudipo kutoka kazini.

Lakini baada ya kuzoeana yote hayo hubadilika, mwanamke huhisi kuwa hana jipya la kumuonyesha mumewe, hujiona wameishakuwa watu wazima sasa, na mara nyingi utakuta mwanamke huyu anashinda na sare (uniform) moja kuanzia asubuhi hadi anapopanda kitandani usiku, mambo ya Hinna, nguo za fashion, salon, manukato, kujipamba na dhahabu huyafanya pale anapotoka kwenda harusini na sio nyumbani. Huku ndio kuzoena, na tafsiri sahihi ni kudharau.

Hivyo ili kulinda kibarua cha chako cha mahusiano ni vyema ukajifunza kila wakati kutofanya vitu ambavyo vimekuwa havijayajengi mahusiano yako.

Vyakula 7 Vizuri Kwa Kuongeza Nguvu Za Kiume

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi.

Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia "booster". Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako.

Sababu za kukosa nguvu za kiume

 Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema, utakuwa bora kama chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili kulinda heshima yako nyumbani?
Vitu vinavyoweza kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume ni kama:
  • Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
  • Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone
  • Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume

Leo napenda tuangalie vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha nguvu za kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda mahusiano na ndoa.

1. Blueberry

Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini. Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za kiume. 

Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.


2. Mtini (Figs)

Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.

3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)

Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za kiume. Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi hupelekea hamu na nguvu zaidi.

Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.

4. Karanga

 
Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.

5. Vitunguu saumu

Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.

6. Ndizi

Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).

7. Chocolate

Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid. Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi.


Vyakula ni bora kuliko madawa makali

Mie binafsi nashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo yako yote ya kiafya. Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona kuna tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa. Kutumia madawa makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa kufanya kazi kama inavyotakiwa. Ni vizuri kama utamuona daktari kama ukiona hakuna kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.

Mara nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko, lakini matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo hutibua mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako. Mie nashauri uangalie jinsi unavyokula, nenda kapime vizuri. Kama jogoo ameshindwa kupanda mtungi, ruksa kuangalia njia mbadala. 

Ni vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na kunyong’onyea. Hii husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri wako katika kufanya shughuli nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi, kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi wakati wewe ndio unajiroga, kuwa makini.

Kama ilivyo ada kwenye mambo mengi ya kiafya, hakuna muarobaini. Ni vizuri ukajaribu kubadilisha chakula unachokula, fanya mazoezi mara kwa mara ili kupata mwili wenye nguvu. Kama utakuwa na swali, weka maoni hapo chini nasi tutakujibu bila kusika hukusu njia zaidi za kutatua tatizo la nguvu za kiume.

Angalia Picha Mwanamke Wa Ajabu Duniani, Atoa Ya Moyoni

Mwanamke mnyanyua vyuma maarufu nchini Urusi, Natalia Kuznetsova amesema kuwa anatamani kuwa na mchumba atakayemuoa baadae lakini wanaume wengi wamekuwa wanamuogopa kumtongoza.
Natalia Kuznetsova

Natalia Kuznetsova (26) ambaye alianza mazoezi akiwa na miaka 14 amesema alishawahi kuolewa na mwanaume ajulikanaye kwa jina la Vladislav Kuznetsov kipindi akiwa na miaka 20 lakini hakudumu nae kwa muda mrefu.
Akieleza sababu za kutodumu nae amesema kuwa rafiki yake huyo alikuwa hapendi watembee pamoja mtaani akiogopa kuchekwa na hiyo ni baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa kuongeza kifua.

“Kila mwanamke duniani ni mzuri siamini kuwa nikiwa mwanamichezo basi nitakosa mwanamme wa kunioa.“amesema Natalia kwenye mahojiano yake na kituo cha runinga cha Raptly TV huku akielezea safari ya mahusiano yake.

“Nilishawahi kuolewa kipindi nikiwa na miaka 20 nilimpenda sana mume wangu lakini haikuwa bahati yangu kwani alikuwa ananionea aibu hakutaka niongozane nae, pengine baada ya kufanya upasuaji wa kuongeza kifua changu. Mimi ni mwanamke kama wengine natamani sana kuwa na mchumba kwa sasa ikibidi tuoane, bado naamini wapo wanaume wengi wananipenda ila labda wanaogopa muonekano wangu nilivyo.“amesema Natalia.

Usipitwe na Habari Muhimu, Install App  Yetu


Android ===>  Bofya hapa
Natalia ambaye mwaka jana alitangaza kustaafu mchezo huo na kubaki kama kocha, wiki hii ametangaza kurudi tena uwanjani kama mchezaji.
Hata hivyo mrembo huyo mwaka 2015 alikiri wazi kuwa anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja baada ya kuishi muda mrefu bila mwanaume.

Mrembo huyo mwenye umbo la kibabe ameshinda tuzo kibao nchini Urusi na nyingine za kimataifa za kunyanyua vyuma vizito.Tazama mahojiano yake na Raptly TV.

Natalia ana kilo 90 na anapatikana kwenye mtandao wa Instagram mfuate kwa jina hilo hilo na hapa chini ni baadhi ya picha zake.
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017