Anthony Joshua wa Uingereza usiku wa kuamkia leo aliingia ulingoni katika Uwanja wa Wembley kupambana na bondia Wladimir Klitschko wa Ukraine katika pambano la uzito wa juu.
Pambano hilo ambalo Joshua mwenye umri wa miaka 27 alimpiga kwa KO round ya 11 kati ya 12 Wladimir Klitschko mwenye umri wa miaka 41 na mataji ya IBF, WBA na IBO katika uzito wa juu.
Joshua ana umri wa miaka 27 tu lakini anaonekana ni miongoni mwa mabondia hatari katika uzito wa juu kwani hadi sasa amepigana mapambano 19 na kushinda yote, tena kwa Knock Out yaani ‘KO’.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini