Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Baada Ya Kupigwa Kibuti..Amber Hatamsahau Young Dee

STORI: ALLY KATALAMBULA | UWAZI | Showbiz
MWANAMUZIKI na muuza nyago kwenye video za Kibongo, anayefahamika zaidi kwa jina la Amber Lulu, hivi karibuni amefunguka kuwa hawezi kusahau kipindi kigumu alichopitia baada ya kuachwa na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Young Dee na kwamba kipindi hicho aliteseka sana kiasi cha kushindwa kufanya mambo yake mengi ya msingi.
Amber Lulu
Akipiga stori na Uwazi Showbiz, Amber alisema Young Dee ni mtu ambaye alimpenda mno lakini kwa kuwa Mungu hakupanga waendelee kuwa pamoja, waliachana lakini kitendo cha kuachana kilimuuma mno na hatasahau maishani mwake.
Young Dee
“Kiukweli kipindi ambacho niliachana na Young Dee nilipitia kwenye mateso makubwa mno, unajua Young Dee ni mtu ambaye nilimpenda sana na wala sikutegemea kama tungedumu kwenye uhusiano kwa kipindi kifupi, hata hivyo kwa sasa nimekwishasahau kila kitu na maisha yanaendelea kama kawaida,” alimaliza Amber Lulu.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017