Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Breaking News: Watu Watano Wafariki Dunia Mkoani Arusha Baada ya Kuangukiwa na Mti


Watu watano wamefariki dunia katika kijiji cha Ngiresi wilaya ya Arumeru mkoani Arusha  baada ya mti mkubwa kuangukia nyumba waliyokuwa wamelala usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa kuanguka kwa mti huo kumetokana na athari za mvua zinazoendela kunyesha.

Amesema kuwa waliofariki dunia ni watoto watatu ambao walikuwa wanafunzi na vijana wa wiwili. Kamanda huyo amesema taarifa zaidi atatoa hapo baadae.


Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017