Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Mkude Aruhusiwa Kutoka Hospitalini, Asema Yuko Vizuri Kabisa

NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude ameruhusiwa kutoka katika hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam alipokuwa amelazwa tangu jana kufuatia ajali ya gari iliyotokea eneo la Dumila mkoani Morogoro.
Akizungumza nasi leo baada ya kutoka hospitalini hapo, Mkude alisema kwamba yuko vizuri na hana tatizo lolote ukiondoa michubuko kidogo.

“Daktari amesema ni mshituko tu baada ya ajali, lakini sijaumia popote na ninaweza kuendelea na ratiba zangu kama kawaida,”amesema.
Jonas Mkude alipokuwa hospitali ya Muhimbili kabla ya kuruhusiwa mapema leo


Mkude na watu wengine watano akiwemo dereva walikuwa kwenye Totota Land Cruiser V8 wakisafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam na walipofika Dumila tairi la mbele likapasuka na gari hiyo kupoteza mwelekeo hadi kwenye pori upande wa kushoto.


Abiria mmoja, Shose Fidelis alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali ya Mkoa wa Morooro, wakati wengine, Jasmin na Faudhia wamelazwa hospitalini hapo, huku dereva ambaye pia ndiye mmiliki wa gari ajulikanaye kwa jina la utani, Rais wa Kibamba anashikiliwa na Polisi.
Shose enzi za uhai wake kabla ya kufariki jana kufuatia ajali ya gari 

Mkude alikuwa anatoka Dodoma, ambako juzi aliisaidia Simba kukata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017