Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

VIDEO: Waziri Ummy Mwalimu Akanusha Taarifa za Kuwepo kwa Ebola Nchini


DAR ES SALAAM: Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Ummy Mwalimu amekanusha taarifa za kuwepo kwa maambukizi ya ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, amesema hakuna mtu aliyehofiwa wala kuthibitika kuwa na maambukizi ya Ebola hapa nchini.
Aidha amesema kuwa serikali ipo makini kuhakikisha watu wote wanaoingia kwenye mipaka ya nchi, hasa kutokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanapimwa afya zao.
Waziri Ummy amesema wamesambaza mashine maalum zilizopo kwenye mipaka ya nchi na kwamba endapo mtu yeyote atahisiwa kuwa na ugonjwa huo, wameshatoa mafunzo ya kutosha kwa madaktari na wasimamizi wa vituo vya mipakani juu ya nini cha kufanya.
Pia ameeleza kwamba kuna utaratibu maalum wa kujaza fomu kuonesha kwamba kila mtu anayeingia nchini kutoka kwenye nchi zenye mlipuko wa ugonjwa huo hatari, amepimwa na yupo salama kiafya.
Kwa upande wa sakata la mwanamke kudaiwa kuibiwa kichanga chake kwenye Hospitali ya Temeke, Waziri Ummy amesema baada ya mwanamke huyo kukataa ripoti ya mganga mkuu inayoonesha kwamba hakuwa na watoto mapacha, ameamua kuunda kamati maalum itakayohusisha jopo la wataalam ambapo watatoa majibu baada ya siku 14.


Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017