Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kauli Ya Mwisho Ya Mzee Ndesamburo Muda Mfupi Kabla Hafariki Dunia


“Nasikia uliwekwa ndani kwa ajili ya rambirambi za watoto wa Lucky Vicent, sasa nakupa hizi kawakabidhi wafiwa, wakikukamata tena nipigie simu.”
Hiyo ilikuwa ni kauli ya mwisho aliyoitoa Mzee Philemon Ndesamburo wakati walipokuwa akisaini hundi kwa ajili ya kutoa mchango wake wa rambirambi kwa wafiwa wa ajali ya basi Lucky Vicent jijini Arusha.
Ndesamburo alitoa kauli hiyo akiwa ofisini kwake na Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro aliyemuita ili kumkabidhi rambirambi za watoto 32 waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea mwanzoni mwa mwaka huu Wilayani Karatu.

Akiwa anasaini hundi hiyo, Ndesamburo aliishiwa nguvu, ndipo wakamchukua kumuwahisha Hospitali ya Rufaa KCMC, Moshi na muda mfupi baada alifariki dunia.
Meya wa Arusha alisema kuwa Ndesamburo alikuwa amepanga kutoa Tsh 100,000 kwa kila familia ya mtoto aliyefariki.

Philemon Kiwelu Ndesamburo alizaliwa Februari 19, 1935 na kufariki dunia Mei 31, 2017. Alikuwa ni Mbunge Mstaafu wa Moshi Mjini (2000-2015), na pia Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017