Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kikwete Amtembelea Kardinali Pengo Dubai

Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete amemtembelea Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo, nchini Dubai leo. Kikwete ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter leo(Ijumaa) na kueleza kuwa amemkuta Kardinali Pengo akiwa mwenye siha njema.
Ingawa hajaeleza amemkuta Kardinali Pengo nyumbani au Hospitali lakini askofu huyo mkuu wa jimbo la Dar es Salaam, amewahi kuripotiwa kuwa yupo nje ya nchi kwa matibabu.
“Nikiwa Dubai safarini kwenda Canada, nimemtembelea asubuhi hii Mhadhama Polycarp Kadinali Pengo na nimefarijika kumkuta akiwa na siha njema.” Ameandika Kikwete.
Kikwete amesema amemtembelea Kardinali Pengo wakati akiwa safarini kuelekea Canada.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017