Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Maskini Johari Wa Bongo Movie,Apata Pigo La Maisha

Pole! Staa wa kitambo wa sinema za Kibongo, Blandina William Chagula ‘Johari’ amepata pigo ‘hevi’ baada ya kufiwa na shangazi yake aliyemlea tangu akiwa mtoto, kumsomesha na kumfundisha maisha hivyo kuondoka kwake kumemuachia maumivu na pigo kubwa
Johari, akiwa nyumbani kwao mkoani Shinyanga kuhudhuria msiba huo aliliambia Wikienda kwa njia ya simu kuwa, aliumia mno alipopata taarifa za kifo cha shangazi yake huyo aliyekuwa nguzo muhimu maishani mwake.
“Nimekuja Shinyanga kumzika shangazi yangu, tumeshamzika, lakini kwa kweli ameniacha mpweke sana maana ndiye aliyenilea, kunisomesha na kunifundisha maisha, kiukweli ni pigo kwangu,” alisema Johari.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017