MREMBO mkali wa Bongo Fleva, Maunda Zorro amebwatukia tuhuma za utumiaji wa madawa ya kulevya na kuweka wazi kuwa hajawahi kubwia unga na kuwataka watu waache kupandikiza maneno akidai yupo tayari kwenda kupima.
Akizungumza na Risasi Vibes mwishoni mwa wiki iliyopita, kwa sauti yenye kukwaruza na ya juu zaidi, Maunda alisema amekuwa akitajwa na baadhi ya watu kwamba ni teja, jambo linalompa usumbufu na kuwashangaa watu wanaoshindwa kufanya mambo yao muhimu, badala yake wanajikita kusingizia watu kwa mambo yasiyofaa.
“Jamani, unajua nashangazwa sana na maneno ya watu kuwa natumia madawa ya kulevya, nani alishawahi kunikuta maskani navuta au nani huwa ananinunulia? Mbona tunazushiana mambo ya kijinga? Niko tayari kwenda kwa mkemia mkuu kupimwa kama natumia madawa hayo, au nikuulize, kwenye ile orodha ya waliotajwa ulisikia jina langu? Niacheni jamani, niko bize na maisha mengine na kwa sasa nimeamua kuwa mama wa nyumbani,” alisema Maunda.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini