Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Msanii Aslay Wa Ya Moto Band Ataja Sababu Za Yeye Kufanya Kazi Kivyake

Msanii anayeunda kundi la Yamoto Band kutoka Tanzania, Aslay ameweka wazi sababu zilizomfanya yeye kuamua kufanya kazi zake binafsi nje ya kundi.

Aslay alifunguka hayo katika kipindi cha Friday Night Live na kusema kuwa wao wameamua kuwa kama walivyo wasanii wa kundi la Weusi ambapo msanii anaruhusiwa kufanya ngoma zake mwenyewe na huku bendi nayo ikiendelea kuwa na ngoma zake. 
"Mkubwa Fella alitoa tamko akasema sasa hivi ni ruksa kila msanii kutoa nyimbo zake mwenyewe ukiachana na bendi, ila bendi itaendelea kuwepo, ni kama wanavyofanya Weusi msanii mmoja mmoja anafanya kazi zake na kwenye bendi pia yupo" -  Aslay.
Msanii huyo ameachia video zake tatu mfululizo  "Angekuona",  "Usiitie Doa" na "Muhudumu" ambazo zote zinafanya vizuri.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017