Muimbaji wa muziki wa mduara anayewakilisha pande za Zanzibar, Ally Tall 'AT' amefunguka na kusema katika maisha yake hawezi kumsahau mwanamuziki Ali Kiba kwani pasipo kukutana naye leo hii angekuwa ni mvua samaki kwao.
Akiwa kwenye heshima ya bongo fleva ya Planet Bongo ndani ya East Africa Radio, AT amesema kwamba baada ya kuahidiwa kupatiwa msaada na Adam Juma wa ku 'shoot' video ya wimbo aliomtumia akiwa Zanzibar, alikata tamaa kwa kuzungushwa ndani ya miezi mitatu lakini mwanamuziki huyo aliahidi kumsaidia ikiwa ni pamoja na kuishi nae.
"Ali mimi ni ndugu yangu kwa jinsi alivyoweza kunisaidia. Nilikata tamaa ya muziki na kutaka kurudi kwetu lakini yeye alisimama na mimi na kunisihi hata ka gharama ya pesa yake atakuwa tayari kunisaidia ili kipaji changu kisije kupotea bure. Alikuwa ni rafiki wa kunitia moyo nisikate tamaa na ndiyo maana nathubutu kusema mimi ni Team Kiba. Wengi walinikatisha tamaa lakini yeye alikuwa upande wangu.
Pamoja na shukrani, AT amedai Kiba ni mwanamuziki wa tofauti na asiyependa sifa kwani hata baada ya kuhiti na wimbo wa Cinderela alieendelea kuishi maisha ya kawaida na siyo kama wasanii wasasa wanavyopata tabu ya kusumbuliwa na Ustaa.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini