Klabu ya Simba imetoa kiasi cha shilingi milioni 4.2 kama sehemu ya rambirambi katika msiba wa aliyekuwa shabiki na mwanachama wao, Shose Fidelis aliyefariki dunia Jumapili iliyopita kwa ajali ya gari akitokea Dodoma kuisapoti timu hiyo iliyobeba Kombe la FA.
Shose alifariki dunia kwenye ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Dumila, Morogoro, akiwa na wenzake pamoja na kiungo wa Simba, Jonas Mkude.
Wakati wa kuuaga mwili wa Shose kwenye Kanisa Katoliki Magomeni jijini Dar, leo Alhamisi, Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange maarufu kwa jina la Kaburu alizungumzia juu ya msiba huo.
Kaburu alisema ni pigo kubwa kwao kuondokewa na shabiki wao huyo ambaye alikuwa akijitahidi kuambatana na timu hiyo popote ilipokwenda.
Upande wa Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema: “Familia ya soka, wadau na Simba wamepata pigo kutokana na kifo cha Shose, sisi kama Simba tumempoteza mtu shupavu ambaye alikuwa akifanya mambo mengi mazuri kwa ajili ya klabu.”
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini