WATU tisa wamejeruhiwa na majambazi baada ya kuvamia machimbo mapya ya dhahabu yaliyopo katika kijiji cha Nyakivangala, Isimani wilayani Iringa mkoani Iringa na kupora zaidi ya Sh Milioni 81, dhahabu zaidi ya gramu 400, na baadhi ya mali za wafanyabiashara katika eneo.
Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela anasema tukio hilo lililitokea majira ya saa nne usiku juzi.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini